Na.
Nathanael Limu
Singida
WAZAZI/walezi wa wanafunzi wa shule ya msingi Ikungi
mchanganyiko,wamehimizwa kuwa makini wakati wakichagua kamati ya shule,ili
pamoja na mambo mengine,kupata wajumbe wenye uwezo na sifa ya kuiendeleza shule
hiyo kongwa katika wilaya ya Ikungi.
Hayo yamesemwa jana na mwalimu mkuu wa shule hiyo,Olivary
Kamilly,wakati akizungumza na wazazi/walezi wa kijiji cha Mbwajiki kata ya
Ikungi juu ya zoezi la kuchagua kamati ya shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1944.
Alisema jukumu la kamati ya shule ni kuhakikisha shule husika
inakuwa na wazingira mazuri ya kufundishia na ya kujifunzia.
Mwalimu Kamilly alisema kuwa kutokana na umuhimu huo,wajumbe wa
kamati ya shule wanapaswa kuwa ni watu wabunifu,wenmye uwezo wa uongozi na
wenye shawishi.
"Kazi ya kamati ya shule yop yote haina posho wala
mshahara,ni kazi ya uwakilishi tu na ya kujitolea kwa asilimia zaidi ya mia
moja"alisema mwalimu Kamilly ambaye pia ni kaimu mratibu elimu wa kata ya
Ikungi.
Alisema kwa hiyo, mgombe ye yote ambaye ana tamaa au ana matarajio
ya kunufaika kwa njia yo yote ile,huyo hafai kuwa katika kamati ya shule.
Akifafanua zaidi,alisema ili kuhakikisha shule inapata kamati
bora,uchaguzi wa safari hii hautafanyika makao makuu ya kata na badala yake
unafanyikia huko waliko wazazi/walezi.
"Nichukue fursa hii,kuwasihi ndugu zangu
wazazi/walezi,kwamba chagueni wagombea ambao ni waumini wazuri wa elimu.Watu
ambao wataisaidia shule yetu kuinua taaluma zaidi ili shule hii kongwe iweze
kuongoza katika wilaya ya Ikungi,mkoa na ikiwezekana,hata ngazi ya
kitaifa",alisema mwalimu Kamilly.
MWISHO.