Wanasiasa kutoka mkoa wa Singida, Dr. Kitila Mkumbo na Tundu Lisu, tayari wametumika kuisambaratisha Siasa ya CHADEMA mkoani Singida, huku Lissu akibeba lawama kubwa ya kummlaiza mwenzake kisiasa badala ya kumjenga
Ni katika kila kona ya viunga vya mji wa Singida, Ikundi na Kiomboi kauli za laana dhidi ya Lissu zinasikika zikivuma kwa kishindo huku baadhi yao wakisema LISU AMEMALIZA MKUMBO
Ni dhahiri kuwa jamaa hawa wawili wote ni wenyeji wa mkoa wa Singida mmoja mnyiramba na mwingine Mnyaturu, kimila inatajwa kuwa LISSU ni Mtani wa MKUMBO, mie sijui, Je Kitendo cha Lissu kumshughulikia ndugu yake Mkumbo nao ni UTANI?
Lakini ipo haja ya kujiuliza je, Migogoro hii ambayo imepelekea maelfu ya Kadi na bendera kuchanwa nchi nzima, kunakijenga chama hicho ambach siku moja tu baada ya kamati kuu yake kuwavua madalaka kumekishusha ngazi kadhaa za umaarufu, kinaweza kuendelea kuwa tishio kwa CCM
Je! wale viherehere waliokuwa wakidhani wao kuwa chadema ni chama chao wataendelea kuamini na kuishi hisia zao hizo?
Huu ni mjadala mpana na wa wazi hebu tujadili
+ comments + 1 comments
Kwa maoni yangu,Mkumbo alikuwa na hoja sahihi kabisa,ila alipaswa kuipeleka kwenye vikao halali zijadiliwe badala ya kwenda under ground jambo linalomfanya aonekane kama ni mtu aliyepanga usaliti.Sasa juu ya Zitto bado nimeshindwa kuelewa ni kwa namna gani ameweza kuingia kwenye mpango wa hatari namna hiyo?Siamini hoja eti alikuwa hajuwi,alikuwa anajuwa.Kitendo cha yeye kutokanyaga ofisini miezi sita hilo nalo linatia mashaka uaminifu wa Zitto kwenye chama chake.