Baada ya sintofahamu ya muda mrefu kuhusu jumuiya ya afrika
mashariki kuwa na sarafu moja, hatimae wakubwa leo wanasaini mkataba wa sarafu
moja ya afrika mashariki
Hatua hii inakuja huku kukiwa na vuguvugu la baadhi ya nchi
kutaka kuzitenga nyingine katika harakati za ukuaji wa uchumi wa afrika
mashariki pamoja mahusiano ya kisiasa miongoni mwao
Katibu mkuu wa jumuiya hiyo yenye makao makuu yake mkoani Arusha
nchini Tanzania Bw. Richard Sezibera amekaririwa na vyombo vya habari mapema
leo akieleza kuwa wakuu wan chi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi wanasaini
mkataba huo katika viwanja vya kilolo au Uhuru mjii Arusha