Home » » Tuhuma zang’oa maofisa Maliasili

Tuhuma zang’oa maofisa Maliasili

Written By Unknown on Ijumaa, 29 Novemba 2013 | 13:30



Waziri wa Maliasili ya Utalii, Balozi Khamisi Kagasheki akifungua mkutano wa wadau wa wanyamapori Dar es Salaam, jana. Picha na Emmanuel Herman 
Na Elizabeth Edward, Mwananchi

Posted  Alhamisi,Novemba28  2013  saa 10:23 AM
Kwa ufupi
  • Akizungumza baada ya kufungua warsha ya wadau wa wanyamapori jana, Balozi Kagasheki alisema mapambano dhidi ya ujangili yanakabiliwa na changamoto nyingi kutokana na kuhusisha mtandao mkubwa ambao ndani yake kuna watu wazito na vigogo serikalini.
SHARE THIS STORY
0
Share


Dar es Salaam. Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki amesema wizara yake imewasimamisha kazi baadhi ya maofisa kutokana na kujihusisha na biashara haramu ya ujangili wa meno ya tembo.
Akizungumza baada ya kufungua warsha ya wadau wa wanyamapori jana, Balozi Kagasheki alisema mapambano dhidi ya ujangili yanakabiliwa na changamoto nyingi kutokana na kuhusisha mtandao mkubwa ambao ndani yake kuna watu wazito na vigogo serikalini.
“Biashara hii wacha bwana, ni ngumu kwelikweli, inahusisha mtandao mkubwa… tayari tumewasimamisha baadhi ya watumishi na hivi karibuni nitayaweka wazi majina ya vigogo na watu wengine wanaojihusisha na mtandao huu.
“Haitaishia kuwasimamisha kazi tu, hatua zaidi dhidi yao zitachukuliwa kwani kujihusisha na vitendo vya ujangili ni sawa na kuhujumu uchumi wa Watanzania,” alisema Balozi Kagasheki.
Hata hivyo, Balozi Kagasheki amekuwa akitoa ahadi ya kuwataja vigogo wanaojihusisha na ujangili bila kutekeleza.
Kauli hiyo ya Kagasheki imekuja zikiwa zimepita wiki tatu tangu Rais Jakaya Kikwete kusitisha kwa muda Operesheni Tokomeza, lengo likiwa ni kutoa nafasi kwa Serikali kujipanga na kurekebisha kasoro zilizojitokeza kwenye awamu ya kwanza ya operesheni hiyo.
Balozi Kagasheki alisema rushwa na kukosekana kwa utashi wa kisiasa ndiyo sababu inayochangia kuwapo kwa changamoto kubwa katika vita dhidi ya biashara hiyo haramu, inayohatarisha maisha ya tembo na soko la utalii.
“Hii ni rasilimali ya Watanzania, hivyo hatutaweza kuvumilia watu wachache wanufaike,” alisema.

Share this article :
 
Shukrani kwa : Harold Dickson | Prosper Kwigize | 0752490120
Copyright © 2013. KWIGIZE NEWS AND COMMUNICATION - Haki zote zimeifadhiwa
Email us: kwigizenews@gmail.com
0764243377