Picha ya wahamiaji kutoka ethiopia (kwa hisani ya Jamii Fprums)
Na. Prosper Kwigize
Jeshi la polisi Tanzani
alinawashikilia raia kumi na sita wa Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini
kinyume cha utaratibu huku wakitajwa kuwa wahamiaji waliokuwa wakisafirishwa
kwenda uhamishoni nchini afrika Kusini
Tukio hilo limetokea
jana katika kitongoji cha makongo juu jijini dare s salaam ambako vijana hao
kumi na sita walikuwa wakihifadhiwa kwa siri na raia mmoja wa Tanzania kwa nia
ya kutafuta utaratibu wa kuwasafirisha kwenda nchini afrika kusini
Kamanda wa polisi mkoa
wa kipolisi wa kinondoni Jijini Dar es salaam, kamishna msaidizi wa polisi
Ahmed Msangi amebainisha kukamatwa kwa raia hao na kwamba aliyekuwa
akiwahifadhi ambaye ametajwa kwa jina la moshi majungu naye amekamatwa na
anakabiliwa na shtaka la biashara ya binadamu
Hivi karibuni kumeibuka
matukio ya biashara na usafrishaji wa binadamu ambapo Tanzania imekuwa
ikitumika kama njia kwa wahamisji kutoka nchi za Sudan, Somalia na Ethiopia
ambao pindi wanapokamatwa hudai kuwa walikuwa katika harakati za kwenda kusini
mwa afrika kusaka maisha mazuri na ajira
Kamanda msangi
anasisitiza kuwa matukio hayo ni hatari kwa Tanzania kwani huenda wahamiaji hao
wakawa ni maharamia au vikundi vya waharifu wanaojificha katika kivuli cha
Uhamiaji na maisha magumu
Wahamiaji hao wanatajwa
kuktwa na moja ya majengo yanayotumiwa na mpenzi wa bw. Moshi Majungu na kwamba
mpenzi wake aliyetambulika kwa jina moja la SALOME ambaye ndiye aliyekuwa
akiwapelekea chakula kwa siri na kutotakiwa kutoka nje, hali iliyosababisha
wahamiaji hao haramu kujisaidia choo kubwa na ndog o katika chumba hicho
Mwaka 2012 raia wa Ethiopia
wapatao 43 walifariki dunia katika mikoa ya Morogoro na Dodoma wakati
wakisafirishwa kwa sri katika maroli ya mzigo baada ya kukosa hewa
- Katika matukio hayo mawili Vijana 84 wahamiaji kutoka Ethiopia walinusurika kifo ka harakati za kwenda kusinimwa afrika na baadaye walishiriki mazishi ya wenzao arobaini na watatu waliopoteza maisha katika jaribio hilo