Picha inaonesha mojawapo ya majengo ya hospitali ya Rufaa Singida ambayo inatarajwa kuwa ya kipekee katika eneo la kanda ya Kati, Hospitali hii inahitaji mkopo wa sh. 500 milioni kwa ajili ya vifaa tiba ili ianze mwakani
Na. Prosper Kwigize
Mkoa wa Singida umetuma maombi ya mkopo wa vifaa tiba wenye
thamani ya sh. Milioni 500 ili kuwezesha kuanza kwa hospitali ya rufaa
nayojengwa mkoani humo kwa lengo la kupunguza adha ya wananchi kwenda katika
hospitari za Bugando, KCMC na Mhimbili
Akihutubia katika kongamano la mfuko wa taifa wa bima ya
afya linalofanyika mkoani Singida kujadili changamoto na mafanikio ya mfuko huo
kwa mkoa wa Singida, mkuu wa mkoa wa Sigida Dr. Parseko Kone amesema pesa hizo
zitawezesha hospitali hiyo kuanza kabla ya decemba mwaka huu
Dr. kone ametoa rai kwa mjumbe wa bodo ya NHIF taifa Bi.
Lyida Choma kuyasimamia maombi hayo ili hospitali hiyo ya rufaa ipate vifaa
tiba na kuanza kuhudumia wanachama wa mifuko ya afya kupata matibabu bora
kulingana na michango yao
Wakati huo huo, mfuko wa taifa wa bima wa afya NHIF na mfuko
wa afya ya jamii CHF umetoa mashuska 170 kwa vituo mbalimbali vya afya na
hospitali ya mkoa wa Singida ili kupungiza adha ya mashuka kwa wagonja
wanaolazwa
Akikabidhi msaada huo kwa mkuu wa mkoa wa Singida, mjumbe wa
Bodi ya NHIF Bi. Lydia Choma amesema hospitali zilizopata uhisani huo ni pamoja
na hospitali ya mkoa, hospitali za wilaya za Iramba, Manyoni, pamoja na vituo
biafsi.
Ends.