Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mapumziko mafupi wakati mafunzo yanayohusu uhamiaji na ukimbizi yakiendelea kwa udhamini wa IOM, watatu kutoka kulia ni Bi. Susan Bipa afisa wa IOM
Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM
limeanza kutoa mafunzo ya siku tatu kwa waandishi wa habari na wadau wengine wa
mawasiliano mkoani Kigoma
Kwa mujibu wa IOM mafunzo hayo
yanalenga kuwawezesha wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari mkoani Kigoma
kuwa na ufahamu na ujuzi wa masuala ya Uhamiaji na wakimbizi
Akiongea na Channel Africa mjini
Kigoma afisa wa IOM Bi. Tusa Njwaba Amebainisha kuwa waandishi wa habari ni
kundi muhimu katka kuhakikisha taarifa za uhamiaji zinafahamika kwa usahihi
Kwa upande wake shirika la kuhudumia
wakimbizi Duniani UNHCR limebainisha kuwa shughuli zake huzingatia mkataba wa
umoja wa mataifa wa la mwaka 1951 pamoja na tamko la umoja wa afrika juu ya
utambuzi wa mkimbizi na mhamiaji
Katika hotuba ya ufunguzi wa mafunzo
hayo, mwakilishi wa UNHCR Tanzania Bi Joyce Mends Cole iliyosomwa na Nicholas
Gichubiri afisa wa UNHCR Dar es salaam anasema kuwa mkimbizi ni mtu
aliyeshinikizwa kuiacha nchi yake
Akizungumzia kuhusu makundi ya
wanaoomba hifadhi ambao hawajakubaliwa kuwa wakimbizi wanaoishi nje ya makambi,
UNHCR imesema itawahudumia na kuwapeleka kambini pale tu kamati ya usaili itakapowapa
hadhi ya ukimbizi
Kwa upande wao waandishi wa habari
wanaoshiriki mafunzo hayo wamekuwa na maoni tofauti kuhusu umhimu wa mafunzo
hayo, Shafiru Makosa ni mtangazaji wa shirika la utangazaji la Tanzania TBC,
ana maoni gani kuhusu mafunzo hayo
Ifahamike kuwa mkoa wa Kigoma
unahifadhi idadi kubwa ya wakimbizi kutoka jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC
wapatao 62,000 wanaohifadhiwa katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu wilayani
Kasulu mkoani Kigoma
Shirika la IOM limekuwa likitoa
usaidizi na kusaidia wakimbizi wanaopata nafasi ya uhamiaji katika nchi ya tatu
maarufu kama Resettlement katika nchi nyingine baada ya taratibu nyingine
kufuatwa katika kuidhinisha ukimbizi wa nchia ya tatu
Aidha IOM hushirikiana na shirika la
umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR katika kutoa huduma kwa wakimbizi
na wahamiaji
Zaidi ya waandishi wa habari na
watangazaji 20 wanashiriki mafunzo hayo kwa matarajio ya kuboresha weledi
katika kazi zao za kuhabarisha jamii kuhusu wakimbizi na wahamiaji.
Hivi karibuni serikali ya Tanzania imeanzisha
operesheni Kimbunga ambayo inawaandama wahamiaji wote ambao wanaishi Tanzania
bila kufuata taratibu zinazolinda haki za wahamiaji pamoja na usalama wan chi husika
Ends.
Note. Sauti zinapatikana katika blog
hii unaweza kudownload na kusikiliza