Home » » KIGOMA KAMA SHANGHAI CHINA

KIGOMA KAMA SHANGHAI CHINA

Written By Unknown on Jumatano, 20 Novemba 2013 | 00:20


Hii ni sehemu ndogo ya kitega uchumi katika fukwe za ziwa Tanganyika mkoani Kigoma, madhari na sura ya eneo hili hufananishwa na baadhi ya miji na vitega uchumi vilivyoko nchini China

Hata hivyo wakati kukiwa na vitega uchumi, na vyanzo vingi vya kuwezesha kuinua pato la mwanaKigoma, Bado wakazi wenyewe wa Kigoma hawajajitokeza kutumia rasilimali zao kupambana na Maradhi, Ujinga na Umasikini

Utegemeza wa ajira za Umma, bado ni ugonjwa mbaya ambao unalitafuna kundi kubwa la vijana ambao wanaposoma huwaza ajira za serikali au mashirika pekee badala ya kufikiri kujiajiri na kutumia rasilimali zinazowazunguka

Kigoma ni moja ya mikoa yenye fursa nyingi, lakini mtazamo wa kijamii, kisera na kijiografia vimekuwa kikwazo kwa maendeleo ya mkoa huo ambao unazungukwa na misitu ya asili yenye rutuba, hifadhi ya wanyama pori, ndege na vipepeo adimu duniani

Aidha Kigoma pia ni mkoa wenye uasili wa Tanganyika kwa maana ya uwepo wa ziwa lenye kina kirefu duniani na samaki aina ya Migebuka, Ngege, Nyika pamoja na sato, Kigoma pia wanapatikana binadamu wa kale (sokwe) wanaofanana na binadamu kwa asilimia Kubwa

Ili Kigoma iendelee ni lazima wakazi na wazawa wa Kigoma wenyewe wabadili mtazamo na namna ya maisha ili hatimae wabaini, waone na watumie rasilimali hizo kwa ajilli ya maendeleo yao na taifa, lakini pia ni lazima serikali nayo itambue kuwa kama mikoa yenye fursa za kiuchumi haitafunguliwa kwa kuwekewa miundombinu bado hatuukomoi mkoa bali Taifa litaendelea kukosa mapato ya nje .
Share this article :
 
Shukrani kwa : Harold Dickson | Prosper Kwigize | 0752490120
Copyright © 2013. KWIGIZE NEWS AND COMMUNICATION - Haki zote zimeifadhiwa
Email us: kwigizenews@gmail.com
0764243377