Rais Kikwete akiwa amebeba kombe la dunia lilipozuru nchini m |
Raisi Jakaya Kikwete wa Tanzania leo analipokea kombe harisi la dunia katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za shirikisho la soka Tanzania kuhamasisha watanzania kuupenda mchezo huo wa mpira wa miguu
Tayari wakati tunaingia mitamboni Rais Kikwete ameingia katika uwanja huo ambao umefurika maelfu ya watazamaji na atakabidhiwa na wawakilishi wa shirikisho la soka duniani FIFA ambao waalitembeza kombe hilo katika mataifa mbalimbali kabl aya kuelekea Blazil mwakani
ujio wa kombe hilo nchini Tanzania unatazamwa kama kichocheo kwa wapenda soka nchii kuendelea kujitoa na kufanya vizuri katika masindano mbalimbali
Wakati kombe hilo likizuru Tanzania, jana Nov 28 Timu ya Taifa ya Tanzania Kilimanjaro Stars imeondoka uwanjani na sare ya kufungana bao moja kwa moja na timu ya taifa ya Zambia Chopolopolo, wakati juzi Zanzibar Heroes ikiitwanga magoli mawili kwa moja timu ya taifa ya Sudani kusini katika mashindano ya Challenge yanayoendelea nchini Kenya.