HABARI MPYA
blink
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Events. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Events. Onyesha machapisho yote

HOFU YATANDA KUHUSU EBOLA MKOANI KIGOMA

Written By Unknown on Jumanne, 2 Septemba 2014 | 10:52


Kanali Issa Machibya, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma 



Kutokana na kuwa jirani na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambayo imeripotiwa kuwa na wagonjwa wanaodhaniwa kuugua Ebola, mkoa wa Kigoma umeanza kuchukua tahadhari kuzuia ugonjwa huo usiingie Tanzania

Mkuu wa mkoa wa Kigoma kanali mstaafu Issa Machibya amebainisha hayo wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu hofu na tahadhari hiyo baada ya serikali ya DRC na shirika la afya duniani WHO kukiri kuwa raia kadhaa wa DRC walioambukizwa virusi vya Ebola.

Kanali machibya amebainisha kuwa kutoka katika eneo linalohofiwa kuibuka kwa ebola nchini DRC hadi mkoani nchini Tanzania eneo la mkoa wa Kigoma ni kiasi cha kilomita arobaini na tano pekee upande wa ziwa Tanganyika.

Aidha amezitaka mamlaka za afya Kinga pamoja na idara za uhamiaji kushirikiana kuhakikisha wageni wanaoingia nchini Tanzania kutoka DRC , Burundi na Zambia kuchunguzwa kwa umakini na atakayetiliwa shaka hatua za haraka zichukuliwe ili kuepuka maambukizi nchini Tanzania.

Naye katibu tawala mkoa wa Kigoma mhandishi John Ndunguru amesisitiza kuwa, mkoa kwa kushirikiana na idara ya afya umeanza kutoa elimu wa wananchi

Pamoja na maagizo hayo wananchi wanaofanya shughuli za uvuvi na biashara katika bandari ndogo za Kibirizi na Ujiji mkoani Kigoma wameikosoa serikali kwa kutotoa mafunzo ya kutambua dalili za ebora pamoja na namna ya kujikinga na maambukizi.

Katibu wa chama cha wavuvi na wamiliki wa mitumbwi mkoa wa Kigoma Bw. Muhamed Kasambo ameeleza kuwa, bandari ndogo hizo hupokea wageni kutoka DRC na Burundi kila siku na serikali haijaweka kituo cha afya ili kuwachunguza wageni hao

Kwa upande wake Bw. MPOROGOMYI SALUM Ambaye ni mvuvi na msafirishaji wa bidhaa za ziwa Tanganyika kutoka Kigoma kwenda Burundi, DRC na Zambia amesema serikali ya Tanzania inapaswa kutoa elimu kwa wananchi wake hususani wasafirishaji katika ziwa Tanganyika ili wafahamu dalili na namna ya kujikinga na ebola.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wetu katika mwalo wa Kibirizi na Ujiji hakuna matangazo yaliyofafikia wavuvi wala vipeperushi kuhusu tahadhari ya Ebola, licha ya mkuu wa mkoa wa Kigoma kanali Machibya kuagiza matangazo kufanyika.

WAZIRI WA FEDHA WA TANZANIA AFARIKI DUNIA

Written By Unknown on Alhamisi, 2 Januari 2014 | 01:00

Marehemu Dr. William Mgimwa, aliyekuwa waziri wa fedha

Waziri wa fedha wa serikali ya Tanzania dr. William Mgimwa amefariki dunia jana nchini afrika ya Kusini alipokuwa akitibiwa kwa muda kitambo

Taarifa kutoka Idaya ya Habari maelezo inataja kuwa serikali inafanya utaratibu wa kuusafirisha mwili wake kutoka Pretoria Africa kusini kuja Tanzania
Mgimwa anatajwa kusumbuliwa na maumivu ya kichwa, na inatajwa kuwa Kipanda uso ndicho kimechogharimu uhai wake

Mungu amlaze Marehemu Mgimwa mahali pema peponi amina
Kwigize news and communication network, tunatoa pole kwa Rais Jakaya Kikwete pamoja na Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kumpoteza waziri mchapa kazi wa wizara nyeti ya fedha


Kufuatia kifo hicho sasa serikali ya Tanzania ina upungufu wa mawaziri watano baada ya wengine wanne kujiuzuru kufuatia kashfa ya operesheni Tokomeza

SALAAM ZA NOELI NA MWAKA MPYA

Written By Unknown on Jumanne, 24 Desemba 2013 | 12:23


Kampuni ya PLEN Media and Entertainment Network kwa pamoja na mtandao wa  Kwigize News tunawatakia wasomaji wetu wote heri ya sikukuu ya Kuzaliwa kwa YESU Kristo Iwe siku ya amani na furaha kwenu, aidha tunawatakiwa heri na baraka tele wakati wa kuupokea na kuuishi mwaka mpya

PLEN Media and Entertainment Tunatarajia kuwa mwaka 2014 utakuwa mwaka wa mafanikio, na tunatarajia kusajili kituo kipya cha RADIO kitakachojulikana kwa jina la PLEN RADIO FM KASULU Radio hii itakuwa ni mkombozi kwa vijana, wazee na akina mama kwakuwa malengo yake yatakuwa kwa ajili ya kubadili fikra za jamii katika maendeleo

MUNGU AWE PAMOJA NASI SOTE

AMINA

ZITTO AMLIPUA MBOWE -POSHO ZA BUNGE NA MASHANGINGI

Written By Unknown on Jumapili, 22 Desemba 2013 | 10:11


Mbunge wa Kigoam Kaskazini Zitto Kabwe amelipua kwa wananchi Mwenyekiti wake wa Taifa Freeman Mbowe kwa kukiuka taratibu na kanuni za Bunge kwa kujipatia fedha za kazi za Bunge na kisha kuzitumia kwa anasa

Hayo yametajwa na Zito Kabwe wakati akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Kasulu akijibu hoja za kamati kuu kumvua madaraka yake ya kichama

Zitto amesisitiza kuwa viongozi wake wa chama wanajaribu kuyumbisha hoja muhimu kama vile, kuchukua fedha za bunge na kwenda kutanua, kukataa mahesabu ya chama kukaguliwa, kuchukua mashangingi na kupokea posho kinyume na makubaliano na kanuni za chama chao.

amesisitiza kuwa kamwe hata kaa kimya na kwamba ataendelea kupinga jambo lolote ambalo linaenda kinyume na maadili ya CHADEMA na hataondoka katika chama hichou licha ya kuwepo kwa shinikizo kubwa

"chama chetu tumehangaika kukijenga, sasa wapo wambao waliingia kwa hiyari CHADEMA na wapo ambao walifukuzwa CCM, au walikosa kura za Maoni CCM ndipo wakaja katika chama chetu na hao ndio wanataka wao waonekane wanakijua chama na wana uchungu nacho kuliko sisi tulioingia kwa hiyari na mapenzi yetu kwa demokrasia" alisisitiza Kabwe

Ikumbukwe kuwa Katibu mkuu wa CHADEMA Dr. Wilbroad Slaa kabla ya kujiunga na chama hicho alikuwa mgombea wa CCM na alikimbilia huko baada ya kushindwa katika kura za maoni katika uchaguzi wa ndani ya CCM Jimbo la Karatu

SANAMU YA MANDELA YATAWALA DUNIA KWA UKUBWA WAKE

Written By Unknown on Jumatatu, 16 Desemba 2013 | 10:49


Siku moja tu baada ya mazishi ya aliyekuwa Rais wa kwanza mweusi na mpigania Uhuru wa Africa kusini Nelson Mandela, Sanamu kubwa zaidi duniani inayomuonesha akihamasisha umoja na maridhiano imezinduliwa katika mji mkuu wa Afrika kusini Pretoria

Sanamu hiyo iliyotengenezwa kwa shaba ina urefu wa mita tisa na ina uzani wa tani nne unusu. Ilizinduliwa katika bustani la majengo ya bunge na inaonyesha Nelson Mandela akihimiza umoja na maridhiano.

Sanamu hiyo yenye mikono ya Mandela ikiwa wazi ilinuiwa kuonyesha Mandela alivyoliungaisha taifa zima kwa mapenzi yake.

Familia ya Madiba , viongozi wa ANC , viongozi wa Afrika na maafisa wengine wakuu walihudhuria mazishi hayo katika kijiji cha Qunu mkoani Cape Mashariki.

Mandela anakumbukwa kwa juhudi zake za kupatanisha wananchi na kupigia debe msamaha miongoni mwa watu na ndio maana leo ikawa siku iliyotengwa kwa ajili ya uzinduzi wa sanamu hiyo.

Wakati wa utawala wa wazungu, terehe 16 Disemba ilijulikana kama siku ya kuwakumbuka mashujaa wa Afrikaners walioshinda vita dhidi ya jeshi la Zulu mwaka 1883.

Zaidi ya karne moja baadaye mwaka 1961, Mandela alizindua jeshi lake la Umkhonto we Sizwe kupigana dhidi ya utawala wa wazungu.

Kuanzishwa kwa jeshi hilo la wazalendo chni ya uongozi wa Mandela kuliongeza hasira ya wazungu kumsaka na hatimaye kumkamata na kumhukumu kifungo cha maisha jela kwa kosa la uhaini


MANDELA AZIKWA RASMI KWA HESHIMA KUBWA

Written By Unknown on Jumapili, 15 Desemba 2013 | 03:45

Tata Madiba (Rais wa kwanza mzaleendo wa Africa Kusini)

Siku kumi tangu alipofariki dunia, hatimaye Rais wa kwanza wa afrika kusini Nelson Mandela amezikwa leo katika makaburi ya fanilia katika kijiji cha Qunu nchini humu huku akiacha hofu kwa wageni wanaoishi nchini humo

Mandela anayeitwa na raia wan chi hiyo kwa jina la TATA Madiba amezika mapema leoo majira ya mchana na viongozi mbalimbali wan chi za kiafrika, Mashariki, Ulaya na Amerika wamehudhuria mazishi hayo

Wageni maarufu kama walowezi wanahofu kuwa huenda kuondoka kwa mandela kukaibua hoja za kuwataka wageni wanaoishi nchini humo kuanza kunyanyaswa, kitendo ambacho mandela hakuwa akikubaliana nacho

Hata hivyo waombolezaji kutoka mataifa mbalimbali ambao walikuwa wakifuatilia runinga ili kushiriki mazishi kwa njia ya picha hawakuweza kuliona jeneza kutokana na kamera kutoonesha kinachoendelea ndani ya kaburi

Sambamba na mazishi hayo mizinga 21 imepigwa angani kama ishara ya heshima kwa Baba wa taifa hilo ambaye alisota jela miaka 27 kufuatia harakati zake za kupinga ubaguzi wa rangi uliokuwaukisimamiwa na serikali ya makabulu

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete amekuwa kivutio katika mazishi hayo pale alipopigiwa makofi mara kadhaa wakati akihhutubia waombolezaji na kutaja kuwa Mandela na raia wa afrika kusini ni ndugu na kwamba Tanzania ilishiriki kwa asilimia mia moja kutetea waafrika na kuleta Uhuru wa nchi hiyo


Katika kupigania uhuru wa nchi mbalimbali za Africa Tanzania ilitoa ardhi na mafunzo ya kisiasa na kijeshi kwa wapigania uhuru wan chi mbalimbali akiwemo Nelson Mandela, Joachim Chisano, Samora Machel na wengine wengi kutoka nchi za Malawi, Zimbabwe, Namibia

MANDALA'S BODY ARRIVES IN HIS VILLAGE

Written By Unknown on Jumamosi, 14 Desemba 2013 | 07:09


The body of Nelson Mandela has arrived at his ancestral home village of Qunu in South Africa's Eastern Cape ahead of the anti-apartheid icon's state funeral that will take place on Sunday.

The coffin carrying the remains of South Africa's first black president was driven in a hearse from Mthatha airport, 700 km (450 miles) south of Johannesburg after it arrived in a military plane. It was given a ceremonial military escort and cheered by crowds lining parts of the road as it made its way to the village where he grew up.

Mandela, whose coffin was draped with the national flag, will be laid to rest in a private affair barred to the public and the media.

The journey to the small village started on Saturday shortly after the governing ANC paid its last respects to the man who led it to power, becoming the country's first black president after a long and painful struggle against racist, white-minority rule.

Al Jazeera's Haru Mutasa, reporting from East Cape, said many people in the province viewed Mandela, who rose from a humble background to lead Africa's most powerful nation, as a "source of inspiration" and were eagerly awaiting the arrival of his coffin.

In a keynote address delivered in Pretoria in honour of Mandela, President Jacob Zuma hailed Madiba, the clan name by which the Nobel laureate was known, as a "man of action".

"Since the day our leader passed on, we have remembered him in a very special way. We have received messages of condolences from around the world," Zuma said.

He said Mandela, who joined the ANC in his early 20s, was able to "combine theory and practice", making it easy for him to practise what he preached.

Earlier, Mandela's grandson, Mandla, gave a speech about the former president's long struggle for freedom.

Mandela, who was battling a chronic lung infection for months, died last Thursday at the age of 95.


On Sunday, some 5,000 people, including foreign dignitaries, are expected to participate in a formal, two-hour ceremony beginning at 8am (0600 GMT).
The funeral procession from the airport to Qunu will be led by the armed forces and Mandela will receive a 21-gun salute and a flyover by the South African Air Force.
Saying goodbye
Since his death at his Johannesburg home on December 5, South Africans have turned out in pouring rain and blistering sunshine to say goodbye to the man they viewed as a liberator.
Tens of thousands packed a soaked stadium in Soweto for a memorial service on Tuesday, which was attended by more than 70 world leaders.
Up to 100,000 people filed past Mandela's open-casket for the three days it was displayed at the Union Buildings in Pretoria, the seat of government where he was inaugurated two decades earlier.

Special Edition
For a unique look at the life of the world's most famous prisoner-turned-president, download our Mandela magazine.

Mandela was jailed for 27 years on Robben Island by the white-minority racist regime which he opposed, emerging from prison in 1990 and becoming president after the country's first multi-racial elections in 1994.
A year before he was elected president, he won the Nobel Peace Prize along with FW de Clerk, South Africa's last apartheid-era president who helped negotiate the end of racial segregation with Mandela.
Around 3,000 members of the media have already descended on Qunu where a special stage and marquee have been erected for the invited guests, who include Britain's Prince Charles.
The funeral will be held according to traditional Xhosa rites overseen by male members of Mandela's clan.
The slaughtering of an animal - a ritual performed through various milestones of a person's life - will form a crucial part of the event.
During the ceremony, Mandela will be referred to as Dalibhunga, the name given to him at the age of 16 as he entered adulthood.
Although Mandela never publicly declared his religious denomination, his family comes from a Methodist background.
Source:
Al Jazeera

GAZETI LA MWANANCHI 30, NOV

Written By Unknown on Jumamosi, 30 Novemba 2013 | 07:57

HABARI KUU

Mishahara ya vigogo ‘hailingani na ufanisi’

Posted 15 hours ago
Ripoti mpya ya utafiti imebainisha kuwa mishahara mikubwa wanayolipwa viongozi wa juu serikalini na wanasiasa hailingani na utendaji wao wa kazi....
 
Shukrani kwa : Harold Dickson | Prosper Kwigize | 0752490120
Copyright © 2013. KWIGIZE NEWS AND COMMUNICATION - Haki zote zimeifadhiwa
Email us: kwigizenews@gmail.com
0764243377