Watu bilioni 1.7 duniani huugua
ugonjwa wa kuhara kila mwaka kutokana na kutozingatia matumizi sahihi ya vyoo
pamoja na kutonawa mikono baada ya kutoka chooni
Katibu wa kampeni ya kitaifa ya usafi
wa mazingira kutoka wizara ya afya na usitawi wa jamii Bw Anyitike Mwakitama
amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini singida wakati wa
kilele cha siku ya usafi wa mazingira, matumizi bora ya choo na kunawa mikono
Aidha ameongeza kuwa watu milioni 1.8
hupoteza maisha kila mwaka kutokana na magonjwa ya kuhara sawa na watu elfu
sita kila siku,huku idadi kubwa ya wanaopoteza maisha ni watoto wadogo ambao ni
chini ya miaka mitano
Kwa upande wa Tanzania amesema watu
elfu 30, hupoeza maisha kila mwaka kutokana na magonjwa yanayotokana na uchafu,
kutotumia vyoo bora na ukosefu wa kunawa mikono baada ya kutoka chooni
Kulingana na utafiti uliofanywa na benki ya duninia
shilingi za kitanzania bilioni 300 hutumika kila mwaka kuwatibu watu wanaougua
magonjwa ya kuhara nchini Tanzania
Kutokana na hali hiyo Wananchi wametakiwa kufanya usafi wa mazingira pamoja
na vyoo ili kuepuka magonjwa ya mlipuko.
Waziri wa afya na ustawi wa jamii Dr. Hussein Mwinyi
katika hotuba yake ya kilele cha maadhimisho hayo iliyosomwa kwa umma na Mkuu
wa mkoa wa Singida Dr Parseko Kone amesema hayo katika kililele cha maadhimisho
ya siku ya usafi duniani yaliyofanyika kitaifa leo mkoani Singida.
Dr. Mwinyi amesema kuwa afya bora ndio msingi wa kila jambo
hivyo amewataka wananchi kufanya usafi wa mazigira pamoja na kujenga vyoo bora
ili kuinua kiwango cha usafi nchini.
Aidha amewataka wazazi walezi pamoja na walimu kwa
ujumla wametakiwa kuwafundisha watoto umuhimu wa usafi kwa maendeleo yao na
taaluma kwa ujumla ili kufikia katika matokeo makubwa sasa katika sekta ya
elimu nchini.