HABARI MPYA
blink
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo michezo. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo michezo. Onyesha machapisho yote

MUZIKI WA MSANII DIAMOND NA MAUDHUI YAKINIFU

Written By Unknown on Jumamosi, 12 Aprili 2014 | 01:43


Msanii wa muziki nchini Tanzania Diamond anatajwa kuwa miongoni mwa wasanii wenye mvuto mkubwa kwa watanzamaji na wasikilizaji wa nyimbo zake, hii ni kutokana na mashabiki kuyakubali mashairi na miondoko yake katika uimbaji



Muziki ni moja kati ya sanaa muhimu sana ambazo zimekuwa kivutio katika burudani miongoni mwa jamii ndani na nje ya Tanzania.

Muziki umekuwa pia ukitumika katika kuibua mjadala, kuchochea maendeleo pamoja na kueneza habari Fulani kwa jamii.

Wanasiasa pia wamekuwa wakiwatumia wasanii katika kueneza sifa zao na propaganda za vyama vyao ili kushawishi wananchi kuzikubali sera zao na kuwachangua katika nafasi wanazoomba.

Nchini Tanzania muziki umekuwa ukibadilika siku hadi siku ukihama kutoka katika ushairi wa kawaida wa kuelimisha jamii na kuhamia katika mapenzi zaidi, baadhi ya wasanii huimba mapenzi tu na wengine huchanganya mapenzi na masuala mengine ya kijamii.

Wasanii wengine huimba tu ilimradi waamshe hisia za kucheza hata kama wimu unaoimbwa hauna maudhui yoyote zaidi ya kukolezwa na vyombo vya kisasa vya kutengeneza milindimo na vionjo vitamu.

Katika makala haya nimevinjali baadhi ya nyimbo za Diamond kutoka Tanzania na kupata hoja ya kukueleza.

Wasanii kote Tanzania wameaminishwa na wapenzi wao (wasikilizaji na watazamaji wa muziki) na sasa wanadhani nyimbo nzuri ni ile inayoimba mapenzi na kutonesha ama kidonda cha penzi au kuanzisha hisia mpya ya mapenzi.

Ni kwa sababu hiyo wengi wao wamekuwa  wakitunga na wakiimba nyimbo za mapenzi tu, na kwa bahati mbaya wanasahau mambo mengine ya kijamii.

Diamond katika wimbo wake wa Mbagala, alifanya muziki wenye muonekano na vionjo vya mapenzi lakini ndani yake kuna jambo muhimu sana la kijamii, ambalo nina hakika ndilo linabeba maudhui yote ya wimbo wake.

Diamond anamkosa mrembo aliye mpenda sana kwa sababu mazingira anapoishi ni machafu na hatari kwa afya za wakazi wa maeneo ya Mbagala
Angalia video hii na utume maoni yako  bofya hapo kwenye neno mbagala uone kisha tutumie maoni yako kuhusu wimbo huo na maudhui yake, anuani yetu ni plen.media@gmail.com


MAVAZI YA NUSU UCHI NA PICHA ZA NGONO MARUFUKU UGANDA

Written By Unknown on Jumatano, 19 Februari 2014 | 04:33



Rais Yoweri Museveni ametia saini mswada wa sheria kali dhidi ya picha za ngono ambao unapinga pia uvaaji wa mavazi yasiyo ya heshima

Sheria hiyo inatajwa kulenga kukomesha uvaaji wa nguo nusu uchi, kwa wavulana na wasichana nchini humo kama sehemu ya kuendelea utamaduni wa taifa hilo na wa kiafrika

Wanaotajwa kuguswa zaidi na sheria hiyo na ngono na mavazi ni wana mitindo, wanavuziki ambao wanatajwa kuwa vinara ya kutembea uchi hasa nyakati za maonesho ya kazi zao na wawapo katika hafla mbalimbali za kijamii

Nguo hasa yanayovaliwa na wanamziki na picha za watu wakiwa uchi. Mwandishi wetu wa Kampala Leylah Ndinda na taarifa zaidi. Kusikiliza taarifa hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Wakazi wan chi ya Uganda wanaopenda kuvaa nguo fupi, zinazobana au zinazoonyesha sehemu za mwili ambazo zaweza kuwafanya watu wa jinsia nyingine kusisimka na kutamani kushiriki ngono nawe, basi jua kuwa unachungulia jela.

MSANII LULU AKIRI KUMUUA KANUMBA

Written By Unknown on Jumatatu, 17 Februari 2014 | 07:33


Katika hali isiyotarajiwa na wengi, msanii maarufu Elizabeth maarufu LULU leo amekiri katika mahakama kuwa alimuua bila kukusudia msanii marufu Tanzania Steven Kanumba

Mbele ya Jaji Rose Temba, Lulu akiongozwa na wakili wake, amesema kulitokea ugonvi baina yao uliopelekea tafulani na kifo cha Kanumba

Lulu ameieleza mahakama kuwa, Kanumba licha ya kuwa bosi wake alikuwa pia mpenzi wake na kwamba ulipotokea ugomvi na lulu kumpiga na kitu kizito Kanumba, alitoa taarifa kwa shemeji yake (mdogo wa Kanumba) kabla ya kukamatwa na polisi

wakili upande wa serikali Monica Mbogo amesema mashahidi kadhaa wapo tayari kutoa ushahidi juu ya Lulu kumua Kanumba kwa makusudi

Lulu alifikishwa kwa mara ya kwanza mahamani April 11 mwaka 2012 ambapo alisomewa shitaka la mauaji na kulazimika kukaa rumande kwa miezi sita kabla ya kupata dhamana

AFRICAN NATIONS CHAMPION RESULTS

Written By Unknown on Alhamisi, 16 Januari 2014 | 11:28


Uganda 0 Zimbabwe 0

UGANDA Cranes edged closer to qualifying from Group B after a goalless draw against Zimbabwe Warriors at Athlone Stadium on Thursday afternoon.

Uganda put up a below standard performance compared to their opening match against Burkina Faso but managed to secure a goalless draw to keep clean sheet and keep top of the group B pushing Zimbabwe to a must win situation in their last group stage match.

Cranes failed to test George Chigova in the Zimbabwe goal and had to rely on Benjamin Ochan who pulled off a couple of saves to keep 'The Warriors' at bay.




Cranes' best chance fell to Yunus Sentamu in the first half but he blazed his effort wide.
Uganda play Morocco while Zimbabwe face Burkina Faso in final group matches .

RONALDO MCHEZAJI BORA WA DUNIA 2013

Written By Unknown on Jumanne, 14 Januari 2014 | 01:47



Mchezaji machachari wa ulaya kutoka nchini Ureno Christian Ronaldo ametangazwa kuwa mchezaji Bora wa mwaka 2013 baada ya ushindani mkali baina yake na Mesi Reonel na Gareth Bale waliokuwa wakifukuzana kuwania taji hilo muhimi la dunia katika viwango vya FIFA

Ronaldo ambaye alinyakuwa tuzo hiyo ya mchezaji bora wa dunia kwa mara kwanza mwaka 2008 alitangazwa kunyakua tuzo mwaka 2013 baada ya kupigiwa kura na makocha, manahodha na waandishi wa habari.
Kwa mujibu wa matokeo Ronaldo alipata kura 1365 akimshinda Messi aliyepata kura 1,205 na Ribery akiambulia kura 1,127.
Kwa upande wa wanawake golikipa wa Ujerumani Nadine Angerer alinyakuwa tuzo ya fifa ya mchezaji bora wa soka kwa upande wanawake huku aliyekuwa kocha wa Bayern Munich Jupp Heynckes akinyakua tuzo ya kuwa kocha bora wa dunia.


 
Shukrani kwa : Harold Dickson | Prosper Kwigize | 0752490120
Copyright © 2013. KWIGIZE NEWS AND COMMUNICATION - Haki zote zimeifadhiwa
Email us: kwigizenews@gmail.com
0764243377