Home » » IDD AMINI DADA RAIS KATILI ALIYEKUWA NA NDOTO NZURI

IDD AMINI DADA RAIS KATILI ALIYEKUWA NA NDOTO NZURI

Written By Unknown on Jumanne, 25 Machi 2014 | 12:27

HAYATI IDD AMINI DADA

Idi Amin Dada alikuwa rais wa Uganda tangu mwaka 1971 hadi 1979
Alikuwa mwanajeshi mahili aliyekuwa na uwezo mkubwa wa kijeshi pamoja na elimu ndogo aliyokuwa nayo.
Utawala wa Uingereza ulimuingiza katika jeshi la afrika mashariki kabla ya Uhuru na aliwahi kutumikia jeshi hilo nchini Barma, kutokana na maguvu alikuwa bondia aliyepata umaarufu na hivyo akapanda haraka ngazi za kisheshi na kuwa jenerali na mkuu wa jeshi la Uganda.
Mwaka 1971 alimpindua rais Milton Obote akajitangaza kuwa rais mpya, lakini wengine hawakumtaka.
Mara moja alianza kuwatesa wafuasi wa Obote na watu wote waliompinga. Kuna makadirio ya kwamba jumla ya watu 100,000 hadi 500,000 waliuawa katika miaka minane ya utawala wake.
Aliharibu uchumi wa Uganda kwa ufisadi na majaribio ya kuongoza biashara. Hatua kubwa ya uharibifu ilikuwa kufukuza watu wote wenye asili ya Kihindi na kugawa maduka na biashara yao kwa ndugu au wafuasi wa rais. Takriban watu 80,000 walipaswa kuondoka kwao wakihamia Uingereza, Marekani au Canada
Pamoja na usheni huo, Iddi Amini alikuwa na ndoto za kuhakikisha Lugha ya kiswahili inakuwa lugha kuu katika mataifa ya Afrika Mashariki na kati, akizitaka serikali zote za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC wakati ule ikijulikana kwa jina la ZAIRE.
Aidha Amini (Nduli) alitangaza kuwa Uganda inaungana na Wamarekani weusi kudai uhuru dhidi ya wazungu, kupinga Ukatili, udharirishaji na ubaguzi wa Rangi nchini Marekani (USA). Alitangaza pia kuwa ili weusi hao wawabane vizuri wazungu ni lazima waanze kujifunza na kutumia lugha ya Kiswahili kama lugha yao.
Mwaka 1975 alifanya mahojiano na waandishi wa habari wa shirika la utangazaji la Ufaransa akatangaza kuwa msimamo wa serikali yake ya kijeshi ni kuhakikisha Lugha ya Kiswahili inakuwa lugha ya ukombozi kwa wamarekani weusi na pamoja na afrika nzima.

Alitangaza pia ndoto yake kuwa “Siku moja wamarekani weusi wataitawala Marekani” akisisitiza kuwa waafrika wana akili nyingi kuliko wazungu. Ndoto hii imetokea kuwa kweli baada ya Barack Obama kushinda kuwa Rais wa kwanza mweusi marekani.

Iddi Amini alipenda sana michezo, hususani Ngoma za asili, Soka, Masumbwi,, kuogelea pamoja na karate (angalia picha)



Wengi hawajui kuwa IDD AMINI alikuwa na ndoto hiyo na aliitangaza mwaka 1975. Aidha Martine Luther mmarekani mweusi na mwana harakati naye aliwahi kutangaza kuwa na ndoto hiyo na historia inamkumbuka yeye baada ya Obama kuwa Rais wa USA.

Pamoja na ndoto nzuri hizo za IDD AMINI DADA (NDULI) bado hakuwa muungwana hata chembe, aliendeleza ubabe na kukumbatia falsafa za kikatili dhidi ya raia, wanasiasa na viongozi wa Uganda, na polepole alianza kuwa na hamu ya kuuvusha ukatili wake kwa majirani
Mnamo Oktoba 1978 Amin alianzisha vita dhidi ya Tanzania kwa kuvamia sehemu za mkoa wa Kagera. Rais Julius Nyerere wa Tanzania aliamua kumwondoa kwa njia ya mtutu wa bunduki na jeshi la Tanzania likatwaa Kampala mnamo tarehe 11 Aprili 1979.
IDD Amin alitorokea Libya, halafu Irak na mwishowe Saudia alikopewa kimbilio kwa masharti ya kutoshughulikia siasa tena.
Alikufa mjini Jeddah tarehe 16 Agosti 2003.


Share this article :
 
Shukrani kwa : Harold Dickson | Prosper Kwigize | 0752490120
Copyright © 2013. KWIGIZE NEWS AND COMMUNICATION - Haki zote zimeifadhiwa
Email us: kwigizenews@gmail.com
0764243377