HABARI MPYA
blink

WANNE WAUWAWA KWA BOMU BAADA YA KUTEKWA NA MAJAMBAZI MPAKANI MWA BURUNDI

Written By Unknown on Ijumaa, 22 Agosti 2014 | 05:27

Eneo la mpaka wa Tanzania na Burundi, Manyovu wilayani Buhigwe mkoani Kigoma



WATU wanne wamepoteza maisha na wengine watano wamejeruhiwa kufuatia bomu la kurusha kwa mkono lililotupwa kwenye gari la abiria na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi kutoka nchi jirani ya Burundi.

Habari zilizopatikana kutoka eneo la tukio na baadaye kuthibitishwa na Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Kilelema, Benedict Samson zinaeleza kuwa tukio hilo limetokea mapema jana asubuhi kati ya kijiji cha Kilelema na Migongo wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa alipata taarifa za kuwepo kwa tukio majira ya asubuhi na baadaye kwenda eneo la tukio ambapo anasema kuwa katika tukio hilo watu watatu ambao wanasadikiwa kuuawa huku wengine sita wakijeruhiwa miongoni mwao wawili wakijeruhiwa vibaya.

Alisema kuwa baada ya kuenea kwa habari hizo muda mchache baadaye waliwasili wanajeshi kutoka katika vikosi vilivyopo maeneo ya mpakani ambao walitoa msaada wa dharula na baadaye kuwachukua maiti na majeruhi na kuwapeleka hospitali ya wilaya ya Kasulu kwa matibabu ya dharula.

Kwa upande wake,Augustino Mkuvata Mwalim katika shule ya Msingi Kilelema ambaye alikuwa mmoja wa abiria kwenye gari aina ya Toyota Hiace waliyokuwa wakisafiria anasema kuwa kabla ya bomu kurushwa kwenye gari awali walisimamishwa na mtu aliyesimama kati kati ya barabara akiwa na bunduki.

Mkuvata alisema kuwa baada ya mtu huyo kusimamisha gari dreva alibaini kwamba mtu huyo anaweza kuwa jambazi na kwamba badala ya kusimamia na kwa kuwa kulikuwa hakujapambazuka aliwasha taa na kuzizima jambo lililomchanganya jambazi huyo na kusogea pembeni ambapo dereva aliongeza mwendo ili kukimbia.

Akisimulia tukio Mwalim kuvata alisema kuwa baada ya kitendo hicho abiria walilala chini ya viti vya gari wakihofia kupigwa risasi lakini alijitikeza mtu mwingine mbele ya gari na kurusha bomu ambalo lililipua gari hilo.

Mkuu wa polisi wilaya ya Buhigwe,Frank Utonga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kwamba kwa sasa wako eneo la tukio wakishughulikia jambo hilo na kwamba taarifa ya nini kimetokea zitatolewa baadaye.

Kamanda wa polisi mkoa Kigoma, Jafari Mohamed hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo kwa kile kilichoelezwa na wasaidizi kwake ameelekea eneo la tukio.

MAONESHO YA WANASAYANSI CHIPUKIZI (YOUNG SCIENTISTS) TANZANIA YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

Written By Unknown on Alhamisi, 21 Agosti 2014 | 09:22


Sanamu ya Ndege iliyoungwa na mmoja wa wanasayansi chipukizi wa Tanzania

Na. Mwandishi wetu 
Dar es Salaam

Maonesho pamoja na sherehe ya kuwatunukia zawadi washindi wa wanasayansi chipukizi au Young Scientists Tanzania (YST) yalifanyika  tarehe 13 hadi 14 mwezi Agosti katika ukumbi wa Aghakhan Diamond Jublee. 


Maonesho haya walifadhiliwa na British Gas Tanzania pamoja na Irish Aid kwa matarajio kuwa vijana hawa wakiendelezwa tatizo la afrika kukosa wana sanyansi litakwisha


Mgeni rasmi wa maonesho hayo alikua Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohammed Gharib Bilal akifuatana na  Balozi wa Ireland nchini Tanzania Finneoula Gilsenan pamoja na Waziri Prof. Makame M. Mbarawa ambao pia walihudhuria maonesho hayo
Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal akisalimiana na meneja wa kampuni ya British Gas Bw. Adam Prince wakati wa Maonyesho hayo

Wanafunzi 200 na walimu kutoka mikoa mbalimbali Tanzania walikusanyika jijini Dar es Salaam kuonyesha miradi yao ya utafiti mwaka huu. 

Ongezeko la msaada unaotolewa na  BG(British Gas) Tanzania na Ireland Aid (Shirika la msaada la Ireland),kumewezesha  maonyesho ya wanasayansi chipukizi   kuwafikia wanafunzi  vijana kwa wingi zaidi ndani ya mwaka huu  2014.

Maonyesho ya( YST ) 2014 ni muendelezo wa mafanikio yaliyofikiwa miaka ya nyuma kutoka shule 4 mwaka 2011 hadi kufikia shule  100 mwaka huu.

Robn Damas na Michael Laurent wanafunzi kutoka Ilboru sekondari wakifurahia tuzo
Programu ya YST ilitokana na jitihada za Ireland ambayo ilitumia mfumo wa maendeleo ya elimu kupitia (CDPC) Combat Diseases of Poverty Consortium. (Kundi  la kupambana na maradhi yanayotokana na umaskini.

Wanafunzi watakaoshinda watawezesha shule zao kukua kisayansi na maendeleo. Zawadi zilizomo ni laptops, fedha, scholarships, pamoja na vitabu kwa maktaba za shule. Washindi wa jumla  wa YST 2014 wataalikwa kuhudhuria maonyesho ya BT Young Scientists na Teknolojia yatakayofanyika nchini Ireland mnamo Januari 2015. 

Kila mwaka maonyesho YST yanalenga  kuongeza mafanikio katika jitihada za  kuinua kiwango cha elimu ya sayansi katika shule za sekondari Tanzania . 

Maonyesho  yanaelezea   miradi kutoka makundi mbalimbali ya sayansi, kibaiolojia na ikolojia; fizikia na kemia; masomo ya kijamii na kitabia; na teknolojia.

Young Scientists Tanzania inatoa wito kwa shule zote nchini kujipatia fursa ya kukua kisayansi na kubadilisha mfumo wa kujifunza masomo ya Sayansi kwa kupitia mashindano hayo. Mashinda hayo hufanyika kila mwaka jijini Dar es Salaam na huhusisha zaidi ya shule 100.

WALIMU MKOANI SINGIDA WAPEWA MAFUNZO YA RIADHA

Written By Unknown on Jumatano, 20 Agosti 2014 | 08:11

 
Na. Elsante John
Singida
 
MRADI wa michezo 'TTU-Education through sports', kupitia ufadhili wa nchi ya Finland, unaendesha mafunzo ya siku tano ya mchezo wa riadha kwa walimu wa shule za msingi na Sekondari Mkoani Singida.
 
Meneja mradi huo Anold Bugado amesema mafunzo hayo, chini ya chama cha walimu nchini (CWT), ni mwendelezo wa taasisi hiyo kutoa elimu ya michezo kwa walimu hao, lengo likiwa ni kuinua michezo mkoani Singida.

Bugado amesema kuwa mafunzo hayo ambayo yatawaimarisha walimu katika kuwaandaa wanafunzi kumudu vyema mchezo huo na mingine ya aina mbalimbali, ameiomba jamii na serikali kutunza vyema vifaa vinavyotolewa na taasisi yake.

Mafunzo hayo yanayofanyika Mjini Singida ambayo yalianza jumatatu yatafungwa kesho ijumaa, yanashirikisha walimu 12 kutoka wilaya Mkalama, Iramba, Manispaa Singida, Manyoni, Ikungi na Singida vijijini.
MWISHO.
 
Shukrani kwa : Harold Dickson | Prosper Kwigize | 0752490120
Copyright © 2013. KWIGIZE NEWS AND COMMUNICATION - Haki zote zimeifadhiwa
Email us: kwigizenews@gmail.com
0764243377