Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma imeanza
mchakato wa kuhakikisha makusany ya mapato ya ndani yanapanda kutokana na
ushuru wa aina mbalimbali pamoja na kuwachukulia hatua mawakala wasio waaminifu
Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa halmashauri hiyo mpya Bw.
Julius Kondo wakati wa kikao cha Baraza la madiwani wilayani Buhigwe
Aidha katika maazimio hayo mawakala kadhaa wamesimamishwa
kufanya kazi hiyo kutokana na kubainika kutokuwa waaminifu na kuhujumu mapato
ya halmashauri
Mawakala waliosimamishwa ni wanaokusanya ushuru katika njia
za usafirishaji wa mizigo kutoka Tanzania kwenda Burundi katika eneo la mpaka wan
chi hizo
Kwa muda mrefu mawakala wa ushuru wa halmashauri wakiwa chini
ya halmashauri ya wilaya ya Kasulu
wamekuwa wakituhumiwa kuhujumu mapato ya serikali bila kuchukuliwa hatua
Maeneo yanayotajwa kuhujumiwa ni katika vijiji vya Muyama,
Nyamugari, Kilelema, Mnanila na kajana.