UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA BUJUMBURA BURUNDI |
Mheshimiwa Samuel Sitta Waziri wa Afrika Mashariki wa Tanzania akiwa nchini Burundi katika ziara ya Kikazi kuimarisha mahusiano ya afrika mashariki hususani baina ya Tanzania na Burundi |
BY. Prosper Laurent Kwigize
Kuimarika kwa usalama na kurejea kwa wakimbizi wa Burundi
waliokuwa wakihifadhiwa nchini Tanzania pamoja na ujirani mwema uliopo baina ya
nchi hizo kumetajwa kuwa kichocheo cha ukuwaji wa uchumi wa afrika mashariki
hususani mikoa inayopakana na nchi jirani
Hata hivyo licha ya kuwepo kwa tumaini hilo baina ya watanzania
na warundi, tatizo la miundombinu inayoziunganisha nchi hizo limekuwa
likikwamisha juhudu za raia wake kujiletea maendeleo
Nchi ya Burundi licha ya kuwa mzalishaji mkubwa wa kahawa na
chai, kupakana na ziwa Tanganyika na upande wa pili kuwa jirani na mashariki
mwa DRC penye madini ya aina mbalimbali, nchi hiyo mpya ya afrika mashariki
imekuwa ikiitegemea sana Tanzania katika biashara na uchumi kwa ujumla
Wafanya biashara wa Burundi wamekuwa wakitegemea bandari ya Dar
es Salaam inayounganisha mataifa mbalimbali duniani kiuchumi pamoja na bandari
ya Kigoma katika ziwa Tanganyika ambayo huziunganisha nchi za Tanzania, Zambia,
Burundi na jamhuri ya kidemokrasia ya kongo.
Baada ya Burundi kujiunga na nchi za afrika mashariki na
kuhama kutoka katika nchi za afrika ya kati ambazo ni DRC, Congo Brazaville na
jamhuri ya afrika ya kati, juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanywa ili kufungua
milango ya kiuchumi baina ya Burundi na Tanzania
Jana waziri wa afrika mashariki wa Tanzania Bw. Samuel Sitta
alizuru nchi ya Burundi ambapo pamoja na mambo mengine anakutana na viongozi wan
chi hiyo kujadil namna ya kuboresha mahusiano ya kisiasa na kiuchuami miongoni
mwa nchi hizo
Ni katika ziara hiyo, waziri sitta anabaini ukweli kuwa, bado
kuna vikwazo vingi baina ya nchi hizo katika kukuza uchumi na hasa katika suala
la miundombinu ya mawasiliano na uchukuzi
Anakirii kuwa endapo barabara za uhakika na viwanja vya ndege
vitajengwa pamoja na wafanyabiashara kubadili mifumo na mitazamo ya kiuchumi,
ni dhahiri afrika mashariki itakomaa kiuchumi
Akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa
Bujumbura jana, Waziri sita anasema ziara yake nchini Burundi inalenga
kuzungumizia kufunguka kwa milango ya kiuchumi baina ya Tanzania, Burundi na
jamhuri ya kidemokrasia ya kongo kama sehemu ya mpango wa soko la pamoja
Waziri sitta anaeleza kuwa ukosefu wa barabara ya lami pamoja
na usafiri wa ndege kutoka Kigoma hadi Bujumbura ni kikwanzo kwa uchumi wa eneo
hilo huki akitoa mfano kuwa yeye amelazimika kusafiri kutoka Dar es Salaam
kwenda Bujumbura kupitia Nairobi Kenya badala ya kupita Kigoma ambapo
ingechukua dakika 20 kufika Bujumbura
Huyo ni waziri wa masuala ya afrika mashariki wa Tanzania akizungumza
na waandishi wa habari mapema jana jijini Bujumbura kuhusu ukuaji wa
ushirikiano wa kijamii na kiuchumi baina ya tanzania na Burundi.
Pamoja na matumaini hayo mapya wakazi wa mikoa ya Kigoma na
Kagera wamekuwa na maoni tofauti juu ya ushirikiano wa kiuchumi baina ya
Tanzania na Burundi, huku wengi wakidai kuwa kumekuwepo na vikwazo vingi vya
kibiashara hususani ushuru na kodi mbalimbali
Kwa upande wao Raia wa Burundi hasa kutoka mikoa ya Ruyigi,
rutana, makamba, chankuzo na Buruli wanailaumu Tanzania kwa kuwa na mbinyo
mkubwa kwa raia wa Burundi wanaoingia nchini humo kwa shughuli za kibiashara
Bidhaa ambazo wafanya biashara wa Burundi kuzihitaji kutoka
Tanzania ni pmaoja na zile za viwandani na mashambani hasa Magodoro, ngano,
chumvi, bidhaa za elektroniki, na bidhaa za plastiki
Nyingine za mashambani ni mazao ya chakula hususani mahindi,
Mihogo, maharage pamoja na ndizi ambazo hulimwa katika ukanda wa nyanda za juu
mkoani Kigoma
Aidha watanzania huhitaji kutoka Burundi nguo aiana ya
vitenge maarufu kama wax ambavyo hutengenezwa nchini Nigeria na kuingizwa
afrika ya kati na baadaye afrika mashariki
Kusikiliza habari hiyo kwa sauti, angalia chini upande wa
kushoto sehemu ya muziki na habari