Na. mwandishi wetu
Kigoma
Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM
limeanza kutoa mafunzo ya siku tatu kwa waandishi wa habari na wadau wengine wa
mawasiliano mkoani Kigoma
Kwa mujibu wa IOM mafunzo hayo
yanalenga kuwawezesha wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari mkoani Kigoma
kuwa na ufahamu na ujuzi wa masuala ya Uhamiaji na wakimbizi
Ifahamike kuwa mkoa wa Kigoma
unahifadhi idadi kubwa ya wakimbizi kutoka jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC
wanaohifadhiwa katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani
humo
Shirika la IOM limekuwa likitoa
usaidizi na kusaidia wakimbizi wanaopata nafasi ya uhamiaji katika nchi ya tatu
maarufu kama Resettlement katika nchin nyingine baada ya taratibu nyingine
kufuatwa katika kuidhinisha ukimbizi wa nchi ya tatu
Aidha IOM hushirikiana na shirika la
umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR katika kutoa huduma kwa wakimbizi
na wahamiaji
Zaidi ya waandishi wa habari na
watangazaji 20 wanashiriki mafunzo hayo kwa matarajio ya kuboresha weledi
katika kazi zao za kuhabarisha jamii kuhusu wakimbizi na wahamiaji.
Hivi karibuni serikali ya Tanzania imeanzisha
operesheni Kimbunga ambayo inawaandama wahamiaji wote ambao wanaishi Tanzania
bila kufuata taratibu zinazolinda haki za wahamiaji pamoja na usalama wan chi husika