Home » » RWANDA MATATANI -MGOGORO WA DRC

RWANDA MATATANI -MGOGORO WA DRC

Written By Unknown on Jumanne, 19 Novemba 2013 | 10:58

KAGAME atuhumiwa kuunda njama za kuigawa DRC ili kuwepo na dola ya KIVU au GOMA, atajwa kuchangia uasi Mashariki mwa DRC ili kufanikisha azma hiyo.

Na. Mwandishi wetu, KNC

Chama cha MRC Lumbumba kilichopigania uhuru wa DRC iliyokuwa ikijulikana kama Zaire kimeituhumu nchi ya Rwanda na Uganda kwa kujaribu kuimega nchi ya jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na kuunga mkono vikundi vya uasi vya M23

Katibu mkuu wa chama hicho Bw. Venance Wialango amebainisha hayo katika mahojiano na KNC jijini Dar es salaam na kubainisha kuwa tangu kuuwawa kwa Patrice Lumumba DRC imekuwa ikivamiwa na Rwanda kwa kusapoti wapambanaji wanaojiita wapigania uhuru

Akizungumzia kuhuru kikundi cha M23 na mahusiano yake na Rwanda Bw. Wialango amesema ni masalia ya vikosi vya Rwanda vilivyomsaidia Hayati rais Laurent Kabila ambao hawakuingizwa katika jeshi la serikali

Aidha Katibu huyo mkuu wa chama cha MRC Lumumba Bw. Venance ameipongeza Tanzania kwa kuongoza jeshi la umoja wa mataifa chini ya vikosi vya SADC kuwaondoa wapiganaji wa M23 mashariki mwa kongo na kusisitiza kuwa ipo hata ya mataifa kuamini kuwa Rwanda ndiyo inayowapa nguvu wapiganaji hao


Kuhusu ushirikiano wa afrika mashariki ambapo baadhi ya wabunge wa Tanzania wanadai kuundwa kwa ushirikiano mpya baina ya Burundi na DRC, Bw. Wailango aalikuwa na haya ya kusema
Share this article :
 
Shukrani kwa : Harold Dickson | Prosper Kwigize | 0752490120
Copyright © 2013. KWIGIZE NEWS AND COMMUNICATION - Haki zote zimeifadhiwa
Email us: kwigizenews@gmail.com
0764243377