Rais UHURU KENYATA wa Jamhuri ya Kenya akifunga nati katika reli kuashiria uzinduzi wa Reli kuelekea Uganda, Rwanda na Sudan ya Kusini |
Siku
moja tu baad aya Rais Kikwete wa Tanzania kuzindua ujenzi wa Reli kuelekea
Burundi na baadaye DRC, Kenya nayo imezindua rasmi ujenzi wa njia ya Reli
itakayounganisha kanda ya Afrika Mashariki na eneo la maziwa makuu ujenzi
utakaofadhiliwa na serikali ya China.
wachunguzi wa mambo wanaona matukio hayo kama kizungumkuti cha kuendelea kuchochea mgogoro baina ya nchi tatu zinazotajwa kuwa na nia ya kuzitenga Tanzania na Burundi huku wengine wakidai kuwa nimasuala binafsi ya nchi husika
Hata hivyo kauli ya Kapten John Komba mbunge wa Mbinga magharibi mkoani Ruvuma iliyotolewa Bungeni mwezi octoba ikiitaka tanzania kuanzisha mahusiano mapya na Burundi na DRC huenda ikawa inafanyiwa kazi licha ya Rais Kikwete kudai kuwa hakuna mpango wa Tanzania kujitoa katika jumuiya iliyopo ya afrika mashariki
Aidha Ujio wa Waziri wa mambo ya nje ya Kenya aliyedai kutumwa na Uhuru Kenyata kuunga mkono msimamo wa Tanzania dhidi ya nchi zinazotishia kuunda shirikisho jipya la afrikamashariki, huenda ilikuwa danganya toto kwani baadhi ya watu wanataja kuwa Ujenzi huo wa reli nchini kenya kuelekea Rwanda ni moja ya yale yaliyojadiliwa na kukubaliwa na maraia wa Rwanda, Uganda na Kenya katika vikao vyao vya siri
Reli Reli inayojenga sasa nchini Kenya inatajwa kuwa itaunganisha Kenya na Sudan Kusini, DR Congo na Burundi.
Sehemu ya
kwanza ya njia hiyo ya reli , itaunganisha bandari ya Mombasa na Mji mkuu
Nairobi na kupunguza muda wa safari kati ya miji hiyo kutoka masaa 15 hadi
masaa manne tu.
Huu bila shaka
ndio utakuwa mradi mkubwa Zaidi kuwahi kujengwa tangu nchi hiyo kujipatia uhuru
miaka 50 iliyopita.
Mradi huo
utagharimu dola bilioni 5.2 kiasi kikubwa cha pesa hizo kikitolewa na Uchina.
Baadhi ya
wakenya wanalalamika kuwa tenda hiyo imetolewa kwa kampuni ya kichina kwa njia
isiyofaa.
Rais Uhuru
Kenyatta katika hafla ya uzinduzi huo amesema kuwa mradi huu ndio utakuwa
kumbukumbu kubwa ya utawala wake Kenya.
Mkataba wa
ujenzi wa njia hiyo ya reli, ulifikiwa kati ya Rais Kenyatta na mwenzake wa China
Xi Jinping mnamo mwezi Agosti mjini Beijing.
Pia kuna
matumaini kuwa njia hiyo ya reli itapunguza msongamano mjini Mombasa moja ya
bandari yenye shughuli chungu nzima barani Afrika.
Njia ya reli
iliyoko sasa, ni ile iliyojengwa enzi za ukoloni.
Baada ya
kukamilika kwa sehemu ya kwanza ya reli hiyo mjini Nairobi, mwaka 2017,
itaendelezwa hadi Magharibi mwa DRC hususan mjini Kisangani, Rwanda, Burundi na
Sudan Kusini.
"Tunachokifanya
hapa leo, kitaleta mageuzi makubwa sio nchini Kenya tu bali katika kanda nzima
ya Afrika Mashariki,’’ alisema Rais Kenyatta akitaja mradi huo kama jambo la
kihistoria.
Aliongeza
kusema kuwa mradi huu ni moja ya miradi mikubwa katika maono yake ya maendeleo
itimiapo mwaka 2030 kuboresha hali ya miundo msingi nchini humo.