HABARI MPYA
blink

KIZIMBANI KWA RUSHWA YA NYAMA

Written By Unknown on Jumamosi, 25 Januari 2014 | 02:03

Mnofu wa Nyama ya Ng'ombe



Na Elisante John, Singida
Januari 24, 2014.

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) imemfikisha mahakamani ofisa mifugo wa kata Mitunduruni iliyopo katika Manispaa ya Singida Edwin Mtae kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya nyama laini kilo 12 za maini, figo na moyo wa ng’ombe.

Mwendesha mashitaka mwanasheria wa TAKUKURU Dominic Maganga ameieleza mahakama hiyo chini ya hakimu mkazi Wilaya Singida Joyce Minde kuwa mshitakiwa alifanya kosa hilo Septemba 28 mwaka jana, majira ya asubuhi kwenye machinjio ya Mitunduruni, mjini Singida.

Maganga amesema kitendo hicho ni kosa na kinyume cha sheria kutokana na kifungu cha 15, cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2007.

Amesema mshitakiwa alikuwa anafanya hivyo, vinginevyo mfanyabiashara husika huelezwa kuwa nyama ya mfugo wake ina dosari na hivyo huamriwa kuiteketeza ili isilete athari kwa mlaji

Maganga amesema baada ya taarifa kufika ofisini, TAKUKURU na baadhi ya wafanyabiashara waliweka mtego uliomnasa mshitakiwa akipokea kilo 12.5 za nyama laini, ikiwa ni za sehemu ya maini, moyo na figo ya ng’ombe.

Hata hivyo mshitakiwa amekana shitaka hilo na yupo nje kwa dhamana ya wadhamini wawili, kwa sharti la kila mmoja kuwa na Sh.500,000 na kesi hiyo itasikilizwa tena februari 06, 2014
MWISHO.

AJALI MBAYA YA GARI YAUA 13 MKOANI SINGIDA TANZANIAGARI LAUWA WATU KUMI NKUMI NA TATU

Written By Unknown on Jumatatu, 20 Januari 2014 | 05:31


Na. Mwandishi wetu
SINGIDA

Watu  13 wamepoteza  maisha  baada ya gari aina ya Noah yenye namba T 730 BUX  iliyokuwa ikitoka Itigi kuelekea Singida mjini kugongana  uso kwa uso na Lori lililokuwa likielekea Dodoma.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida Bw. Geofrey Kamwela amesema ajali hiyo imetokea leo katika kijiji cha Isuna wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida
 
Amesema  dereva na konda wa gari aina ya Noah  wote wamepoteza  maisha  na huku dereva  na konda wa Lori  wote  wamekimbia na hawajajulikana majina yao.
  
Bw. Kamwela amesama kati ya abilia 14 waliokuwa katika gari aina ya Noah ni mmoja tu aliyenusurika kifo


Amesema miili ya mrehemu  imehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Singida,  na majeruhi anaendelea kupatiwa matibabu. Taarifa za awali zinaonyesha kuwa mwendo kasi na uzembe kwa madreva wote wawili huenda ndio chanzo cha ajali hiyo

KUELEKEA BUNGE LA KATIBA, VYAMA VYASAKA MWAFAKA

Written By Unknown on Alhamisi, 16 Januari 2014 | 11:46


Vyama vyote 21 vyenye uwakilishi na visivyokuwa na uwakilishi bungeni nchini, kikiwamo Chama Cha Mapinduzi (CCM), vimeanza kujipanga kuwa na maridhiano ya kitaifa ili kuhakikisha vinakuwa na msimamo mmoja katika kujadili rasimu ya katiba mpya, kabla ya Bunge Maalumu la Katiba kuanza.

Hatua hiyo imeanza kuchukuliwa chini ya uratibu wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), kwa kuzingatia moja ya mambo mawili, ambayo Rais Dk. Jakaya Kikwete na viongozi wakuu wa vyama sita vyenye uwakilishi bungeni, walikubaliana walipokutana Ikulu, jijini Dar es Salaam, Oktoba 15, mwaka jana.

Jambo la kwanza, ambalo pande mbili hizo zilikubaliana, ni vyama vyote vya siasa vyenye mawazo, maoni na mapendekezo ya kuboresha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2013, kuyawasilisha haraka serikalini ili kutafuta namna ya kuyashirikisha katika marekebisho ya sheria hiyo.

La pili, vyama vya siasa nchini, kama wadau muhimu katika mchakato wa Katiba Mpya, viangalie namna ya kukutana na kujenga mfumo wa mawasiliano na maridhiano wa jinsi kwa pamoja vitakavyosukuma mbele mchakato mabadiliko ya katiba ya nchi kwa maslahi mapana ya nchi na mustakabali wa taifa.

Viongozi, ambao Rais Kikwete alikutana nao Ikulu kwa mazungumzo hayo wanatoka vyama vya CCM, Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi, TLP na UDP.

Katika makubaliano hayo, TCD ilipewa jukumu la kuratibu jambo hilo, ikiwa ni pamoja na kuandaa mkutano wa vyama hivyo na wadau wengine nchini.

Katika kuanza kujipanga kuhusu suala hilo, TCD ilikutana na viongozi wakuu wa vyama hivyo jijini Dar es Salaam ili kujadili suala hilo.

Baada ya mkutano huo, Mbatia alivitaka vyama hivyo kuanza mara moja kuichambua rasimu hiyo na kuwasilisha misimamo ya kila chama kwenye kamati ya ufundi ya TCD.
Katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam chini ya uenyekiti wa Msemaji Mkuu wa TCD, James Mbatia, vyama visivyo na uwakilishi bungeni, viliwakilishwa na Mwenyekiti wa UPDP, Fahmi Dovutwa.

Mbatia alisema mwisho kwa vyama hivyo kutoa na kuwasilisha misimamo yao kwa kamati hiyo kuhusu rasimu ya katiba mpya ni Januari 31, mwaka huu.

Alisema baada ya vyama kuwasilisha misimamo yao, kamati hiyo itatengeneza ‘bango kitita’, ambalo litaiweka (misimamo hiyo) pamoja ili kuona msimamo wa kila chama kuhusu rasimu hiyo.

Alisema baadaye, kati ya Februari 8 na 14, utaitishwa mkutano wa maridhiano ili kupata msimamo wa vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu kuhusu rasimu hiyo kabla ya kuingia kwenye Bunge hilo.

Mbatia alisema jambo la pili, ambalo liliifanya TCD ikutane na viongozi wakuu wa vyama hivyo jana, ni kuelezana kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura.

Alisema wanataka uboreshaji wa daftari hilo ufanyike kabla ya hatua ya kupiga kura ya maoni kuamua ama kuikubali rasimu hiyo au kuikataa.

Hivyo, alitumia fursa hiyo kuitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuanza mara moja mchakato wa uboreshaji wa daftari hilo na kuisisitiza serikali kusaidia suala hilo ili kuhakikisha linafanyika.

Kwa upande wake, Dovutwa alisema vyama vya siasa ndiyo wadau wakubwa katika mchakato wa upatikanaji wa katiba, hivyo ushiriki wao utasaidia kupatikana haraka katiba mpya Tanzania.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, alisema kuna faida kubwa sana viongozi wa vyama vya siasa kukutana na kujadili mambo makubwa ya kitaifa kwa sababu inaondoa hofu katika siasa.

Pia alisema jambo hilo linasaidia kujadili na kuondoa tofauti mbalimbali zinazojitokeza katika siasa na katika Bunge.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alikataa kuzungumza lolote alipotakiwa na waandishi wa habari kutoa maoni yake akisema kwa jana asingeweza kuzungumza chochote kwa kuwa kikubwa kilichochajadiliwa kilikuwa katika mkutano wao.
Katika mkutano huo, CCM iliwakilishwa na Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara, Philip Mangula na Kinana.

Wengine walioiwakilisha Chadema ni Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, Mwanasheria Mkuu, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo, John Mnyika.
CUFMwenyekiti, Profesa Ibrahim Lipumba na Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara, Julius Mtatiro.

NCCR-Mageuzi Kaimu Katibu Mkuu, Mosena Nyambabe, wakati UDP na Isack Cheyo.
Ilielezwa kuwa viongozi wakuu wa vyama hivyo walikutana Ikulu mwaka jana na Rais Kikwete katika mazingira ya maelewano na mwafaka.  
CHANZO: NIPASHE


AFRICAN NATIONS CHAMPION RESULTS


Uganda 0 Zimbabwe 0

UGANDA Cranes edged closer to qualifying from Group B after a goalless draw against Zimbabwe Warriors at Athlone Stadium on Thursday afternoon.

Uganda put up a below standard performance compared to their opening match against Burkina Faso but managed to secure a goalless draw to keep clean sheet and keep top of the group B pushing Zimbabwe to a must win situation in their last group stage match.

Cranes failed to test George Chigova in the Zimbabwe goal and had to rely on Benjamin Ochan who pulled off a couple of saves to keep 'The Warriors' at bay.




Cranes' best chance fell to Yunus Sentamu in the first half but he blazed his effort wide.
Uganda play Morocco while Zimbabwe face Burkina Faso in final group matches .

UGANDA FORCE IN SOUTH SUDAN CONLICT



By Raymond Baguma
New vision

The army will not reveal details regarding the numbers of Ugandan troops killed in South Sudan as well as identities of the casualties in the ongoing conflict between SPLA government troops and soldiers loyal to former vice president Riek Machar.

UPDF spokesperson Lt. Col. Paddy Ankunda said that revealing the number of casualties and troop deployments could be ‘tactical suicide,’ if the information is released and ends up in the hand of opposing forces.

“We don’t reveal casualties before we inform relatives. It can be devastating to learn about the death of their people through the media. At an appropriate time, government will be brought to account and reveal those numbers,” said Lt. Col. Ankunda.

Ankunda was on Thursday addressing a press conference at the Uganda Media Centre in Kampala.

On Tuesday while in Angola, President Yoweri Kaguta Museveni that the Ugandan army is engaged in direct combat with rebels fighting against the South Sudan government of President Salva Kiir.

Museveni while speaking at the International Conference on the Great Lakes Region (ICGLR) Heads of State summit in Angola, said that UPDF incurred casualties and deaths during a battle about 90 kilometers from Juba.

Narrating the circumstances under which UPDF was attacked; Lt. Col. Ankunda said that UPDF soldiers fell in an ambush laid by the rebels loyal to Riek Machar. However the UPDF was able to beat the ambush.

Ankunda said that Uganda could not stand by as a removal of a government using unconstitutional takes place and UPDF troops would not hesitate to put themselves in harm’s way in order to ensure and prevent a likelihood of genocide in South Sudan.

He said that by Monday, the UPDF has repatriated a total over 40,000 people who include Ugandans since the fighting first broke out in South Sudan.

He said that following the approval of UPDF deployment by parliament recently, the deployment will be formalized with the ratification of a Status of Forces Agreement between Uganda and the Government of South Sudan. The agreement spells out how the UPDF troops are supposed to conduct themselves.

“We are under a bilateral mandate and troops were deployed on the invitation of Kiir who requested Museveni to deploy troops. Salva is frustrated with regional leaders who did not respond to his call.   
 

WALIOCHOMA BASI MKOANI SINGIDA KIZIMBANI-YUMO DIWANI


Na Elisante John, Singida

Januari 16, 2014:WATU 12 akiwemo diwani wa kata ya Unyambwa (CCM) Manispaa ya Singida Shabani Satu (47), wamefikishwa mahakamani mjini Singida jana Ijumaa, kwa shitaka la kuchoma moto basi la Mtei Express, wakati likiwa safarini kutoka Singida Mjini kwenda Mkoani Arusha.

Wengine walioshitakiwa pamoja na diwani huyo ni Salumu Shabani (20), Hashimu Hamisi (20), Hasani Itambu (54), Ahmed Abdarlahaman (24), Shabani Hamisi (29) na Japhet Eliakimu (38) wote wakazi wa Kisasida, katika Manispaa ya Singida.

Pia katika shitaka hilo wapo washitakiwa wengine 11 ambao ni Shamushadini Adamu (32), Ally Jafari (19), Ali Mohammed (29) na Yasini Emmanuel (23) wote wakazi wa Unyambwa katika Manispaa ya Singida na Michael Andrew (30) mkazi wa Unyankhae, Singida vijijini.

Mbele ya hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida Asha Mwetindwa, ilidaiwa na mwendesha mashitaka wa polisi Musa Chemu kuwa washitakiwa walifanya kosa hilo Januari tisa mwaka huu, saa 1:30 asubuhi katika Kijiji cha Kisasida, kata Unyambwa tarafa ya Mungumaji, Manispaa ya Singida.

Chemu alisema kuwa, washitakiwa kwa pamoja wakiwa na nia ovu, walilichoma kwa moto basi la kampuni ya Mtei Express, lenye namba za usajili T 742 ACU Scania, lenye thamani ya Sh. Milioni 70 na kusababisha hasara na uharibifu mkubwa.

Mwendesha mashitaka katika kesi hiyo aliieleza mahakama hiyo kuwa, upelelezi zaidi wa shauri hilo bado unaendelea na kesi hiyo limepangiwa hadi Januari 30 mwaka huu.

Hakimu Mwentindwa aliwaeleza washitakiwa kuwa dhamana ipo wazi kwa kila mmoja kuwa na wadhamini wawili, wenye mali isiyohamishika kwa kila mdhamini awe na thamani ya Sh. Milioni 35, huku mali hizo ziwe zimefanyiwa tathimini na mamlaka husika katika Manispaa ya Singida.

Hata hivyo washitakiwa wote walikana kosa hilo na hadi NIPASHE inaondoka mahakamani hapo  saa tano mchana, hakuna mshitakiwa aliyekuwa ametimiza masharti ya dhamana, hivyo kulazimika kurejeshwa tena mahababusu.
MWISHO.


DAKTARI JELA KWA WIZI WA WATOTO HOSPITALINI

Written By Unknown on Jumanne, 14 Januari 2014 | 02:18


Kwa. Hisani ya BBC
Daktari mmoja katika mkoa wa Kaskazini wa Shanxi nchini Uchina amehukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia ya kuwaiba watoto saba kutoka hospitali aliyokuwa akihudumu na kuwauza watoto hao kwa wauzaji watoto.
Hukumu hiyo ya kifo hubadilika na kuwa kifungo cha maisha baada ya miaka miwili ya mshitakiwa kubadili tabia
Wakati mmoja daktari Zhang Shuxia alikuwa mtaalam mashuhuri lakini sasa ni nuhalifu mwenye hatia aliyejipatia faida kubwa kutokanana na uuzaji wa watoto.
Daktari huyo aliwadanganya wazazi wapya kwamba watoto wao walizaliwa wakiwa na ugonjwa mbaya.Aliwahadaa kwamba iwapo wazazi wangeliwachia serikali jukumu la kuwaangalia basi wangepewa matibabu ya hali ya juu waliohitaji.
Watoto hao wenye afya njema baadaye waliuzwa kwa bei ya maelfu ya madola kwa wauzaji watoto wanaohudumu katika mikoa ilio karibu.
Sita kati ya watoto walioibwa walipatikana na kurudishwa kwa wazazi wao huku mtoto mmoja aliyeuzwa kwa dola 165 pekee akipatikana ameaga dunia kandokando ya barabara ambapo alikuwa amewachwa na muuzaji mmoja wa watoto.


RONALDO MCHEZAJI BORA WA DUNIA 2013



Mchezaji machachari wa ulaya kutoka nchini Ureno Christian Ronaldo ametangazwa kuwa mchezaji Bora wa mwaka 2013 baada ya ushindani mkali baina yake na Mesi Reonel na Gareth Bale waliokuwa wakifukuzana kuwania taji hilo muhimi la dunia katika viwango vya FIFA

Ronaldo ambaye alinyakuwa tuzo hiyo ya mchezaji bora wa dunia kwa mara kwanza mwaka 2008 alitangazwa kunyakua tuzo mwaka 2013 baada ya kupigiwa kura na makocha, manahodha na waandishi wa habari.
Kwa mujibu wa matokeo Ronaldo alipata kura 1365 akimshinda Messi aliyepata kura 1,205 na Ribery akiambulia kura 1,127.
Kwa upande wa wanawake golikipa wa Ujerumani Nadine Angerer alinyakuwa tuzo ya fifa ya mchezaji bora wa soka kwa upande wanawake huku aliyekuwa kocha wa Bayern Munich Jupp Heynckes akinyakua tuzo ya kuwa kocha bora wa dunia.


SIKU YA LORIA YA LEO KATIKA HISTORIA YA DUNIA YA USLAM


Leo ni Jumanne tarehe 12 Mfunguo Sita Rabiul Awwal 1435 Hijria sawa na Januari 14 mwaka 2014.
Siku kama ya leo miaka 1488 inayosadifiana na tarehe 12 Rabiul Awwal miaka 53 kabla ya Hijria, kwa kauli ya baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu akiwemo Masoudi, alizaliwa Mtume Muhammad SAW. Wanachuoni wengine wa Kiislamu wanaamini kwamba Mtume Muhammad (saw) alizaliwa tarehe 17 Rabiul Awwal mwaka huohuo. Kwa msingi huo, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilitangaza kipindi cha kuanzia tarehe 12 hadi 17 Rabiul Awwal kila mwaka kuwa ni Wiki ya Umoja kati ya Waislamu kote duniani. Wiki ya umoja ni fursa nzuri ya kuzikurubisha nyoyo za Waislamu na kuimarisha umoja na mshikamano wao katika kukabiliana na maadui wa ulimwengu wa Kiislamu.
Tarehe 12 Rabiul Awwal mwaka wa kwanza Hijria, Mtume Muhammad (saw) aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa msikiti wa kwanza kabisa katika Uislamu katika kijiji cha Quba kilichoko pambizoni mwa Madina. Mtume (saw) aliweka jiwe la msingi la msikiti huo wa kihistoria wakati aliposimama kwa siku chache katika eneo la Quba akiwa njiani kutoka Makka na kuelekea Madina. Mtukufu huyo alisimama kwa muda katika kijiji cha Quba akimsubiri Ali bin Abi Twalib na jamaa wa familia ya Mtume.
Msikiti wa Quba ambao ni wa kwanza kujengwa katika Uislamu una umuhimu mkubwa na ni miongoni mwa maeneo ya kihistoria ya Waislamu.
Siku kama ya leo miaka 3 iliopita, sawa na tarehe 14 Januari 2011 Rais Zainul Abidin Bin Ali wa Tunisia na dikteta wa nchi hiyo alikimbilia Saudi Arabia kufuatia vuguvugu la mapinduzi ya wananchi. Kwa kuikimbia nchi Zainul Abidin, utawala wa kiimla uliodumu kwa nusu karne wa Habib Bourquiba pamoja na Zainul Abidin Bin Ali ulifikia tamati nchini humo, na wananchi wa Tunisia wakaonja ladha ya uhuru. Zainul Abidin aliingia madarakani mwaka 1987 kupitia mapinduzi ya kijeshi bila umwagaji damu na kumwondoa madarakani Habib Bourguiba aliyekuwa amejitangaza kuwa rais wa maisha wa nchi hiyo. Bin Ali aliiongoza Tunisia kwa mkono wa chuma kwa miaka 23 huku akiendeleza siasa za kutegemea Wamagharibi na kupiga vita Uislamu. Kujichoma moto kijana mmoja muuza mboga katika kulalamikia dhulma na ukatili wa maafisa usalama wa utawala wa nchi hiyo, kuliibua harakati ya wananchi wa Tunisia dhidi ya utawala wa kiufisadi wa Bin Ali na hatimaye kupinduliwa dikteta huyo.

 
Shukrani kwa : Harold Dickson | Prosper Kwigize | 0752490120
Copyright © 2013. KWIGIZE NEWS AND COMMUNICATION - Haki zote zimeifadhiwa
Email us: kwigizenews@gmail.com
0764243377