HABARI MPYA
blink

NAFASI ZA KAZI

Written By Unknown on Jumatatu, 6 Oktoba 2014 | 22:19


KAMA UNASAKA AJIRA ANGALIA HAPA
http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2014/10/vacancies1.jpg

MASJALA YA ARDHI YACHOMWA KUFICHA UOVU

Written By Unknown on Ijumaa, 3 Oktoba 2014 | 08:28



Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kuchoma moto Masijala ya Idara ya Ardhi ya Manispaa ya Kigoma Ujiji na kuteketeza Hati na Nyaraka mbali mbali za idara hiyo

Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma, ACP Jafari Mohamed amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa wanaoshikiliwa watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.

Kamanda Mohamed amewataja watu hao kuwa ni Anna Fanuel (46), mhudumu wa ofisi, Makrina Paul (49),Karani, Saimon Pius (37),mkazi wa Burega na Tumaini Esau (44), mkazi wa Mwasenga, Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Alisema kuwa mnamo Octoba mosi mwaka huu majira ya saa nne na robo usiku Masijala ya Idara ya Ardhi ya Manispaa ya Kigoma Ujiji ilichomwa moto na kuteketeza hati na nyaraka mbali mbali kitendo ambacho ni kinyume cha Sheria.

Inadaiwa kuwa kitendo hicho ni njama ya kupoteza vielelezo nyeti kutokana Idara hiyo kughubikwa na migogoro inayohusiana na ugawaji wa viwanja.

Kamanda Mohamed alisema mbinu iliyotumika ni kuchoma ofisi kwa kutumia mafuta ya Petroli.

MFUMO DUME WAKWAZA WANAWAKE TANZANIA

Written By Unknown on Alhamisi, 2 Oktoba 2014 | 09:07



Imeelezwa kuwa mfumo dume ni moja ya changamoto zinazokwamisha wananwake nchini Tanzania katika harakati za kushiriki uongozi wa kijamii na uchumi.

Hayo yamebainishwa na afisa kutoka shirika la umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO, Bi. Rose Mwalimu katika mahojiano maalumu.

Bi. Rose amebainisha kuwa wanawake wananyimwa fursa kutokana na mfumo dume jambo ambalo linatia shaka kama usawa wa hamsini kwa hamsini utapatikana ifikapo 2015 katika uwakilishi wa vyombo vya maamuzi.

Aidha Bi. Rose amebainisha kuwa licha ya jamii kutegemea vyombo vya habari katika kubadili tabia kwa njia ya habari, bado waandishi wa habari Tanzania havijatoa mchango wake kuondoa mfumo dume na unyanyasaji wa kijinsia

Akielezea juu ya weledi wa waandishi wa habari Tanzania Bi Rose mwalimu ambaye pia kitaaluma ni veteran katika taaluma ya habari, amewatahadharisha waandishi wa habari kuwa makini na waepuke kuandika habari zenye kuchochea migogoro.

Shirika la UNESCO linaendesha mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka katika Radio jamii nchini ili kuwajengea uwezo wa kuandika habari na kuandaa vipindi kwa kuzingatia masuala ya jinsi na jinsia.

Zaidi ya Radio Jamii 11 zimepata udhamini wa mafunzo na kujengewa uwezo na UNESCO ambayo yamefanyika kati ya September 22 na October mosi ambayo yamefanyika mkoani Kigoma pamoja na Mwanza.
 
Shukrani kwa : Harold Dickson | Prosper Kwigize | 0752490120
Copyright © 2013. KWIGIZE NEWS AND COMMUNICATION - Haki zote zimeifadhiwa
Email us: kwigizenews@gmail.com
0764243377