HABARI MPYA
blink

WAKAZI ZAIDI YA MILIONI MOJA MKOANI GEITA HATARINI

Written By Unknown on Jumamosi, 26 Julai 2014 | 11:44



Sehemu ya kijiji cha Mwasabuka wilayani Nyang'hwale mkoani Geita ilivyoharibiwa kutokana na uchimbaji wa Dhahabu, Nyumba zaidi ya 500 hatarini kutokana na kuathiriwa na milipuko ya fataki za kuvunja miamba ya madini hayo

Asasi ya Okoa Mazingira REMA iliyoko mkoani Geita imeitaka serikali kufanya uchunguzi wa athari za mazingira zinazotokana na uchimbaji mkubwa na mdogo wa madini ya dhahabu mkoani humo ili kunusuru maisha ya wananchi

Rai hiyo imetolewa na katibu mtendaji wa asasi hiyo Bw. Idd Malangula wakati akiongea na Uhuru FM kuhusu athari za mazingira katika eneo la migodi ukanda wa ziwa Victoria

BW. Malangula  amebainisha kuwa asasi hiyo imebeini kuwepo kwa athari kubwa za kimazingira zinazotokana na makampuni ya madini kutozingatia hifadhi kanuni, pamoja na wachimbaji wadogo kutokuwa na elimu.

Amebainisha kuwa wananchi wanaopakana na migodi ya dhahabu mkoani Geita wako katika hatari ya kupoteza maisha kwa kuugua maradhi yanayotokana na matumizi ya maji yaliyochafuriwa na kemikali hatari kutoka migodini

Aidha Bw. Malangula ametaja kuwa utafiti uliofanywa na asasi yake katika bonde la mto Nyakabare wilayani Geita umebaini kuwepo kwa kemikali za baruti, vumbi na viwatilifu hatari ambavyo huenda vikawadhuru binadamu.

Nyakabare ni mto pekee ambao unategemewa na wakazi wa vijiji zaidi ya kumi na vine ambapo maji yake hutumika kwa matumizi ya nyumbani, kilimo na mazingira na maji yake huelekea ziwa Victoria.

Bw. Malangula amebainisha kuwa licha ya makampuni ya madini kutambua athari ya kimazingira na afya kwa binadamu, wameendelea kulipua baruti na kutumia kemikari ambazo kuishia katika mto huo jambo ambalo ni hatari kwa binadamu

Asasi ya REMA inayojishughulisha na hifadhi ya mazingira mkoani Geita ni moja ya makundi ambayo yanapigwa vita na na vikundi vya wachimbaji wadogo, wakubwa na taasisi za umma ambazo zinahusika na uharibifu huo wa mazingira,

WAZEE TANZANIA WALAANI KUTENGWA NA JAMII HUSUSANI VIJANA WAO

Written By Unknown on Ijumaa, 25 Julai 2014 | 10:00




Taasisi ya saidia wazee Tanzania SAWATA imewataka wazee kushirikiana na serikali za mitaa kuunda mabaraza ya wazee katika ngazi za vijiji na mitaa.

Rai hiyo imetolewa na katibu wa SAWATA wilaya ya Kasulu Bi. Cotrida Kokupima wakati akitoa mada juu ya haki za wazee katika semina ya wazee watoa huduma za wagonjwa majumbani.

Bi. Kokupima amebainisha kuwa, kutokuwepo kwa mabaraza hayo kumechangia kukwama kwa juhudi za wazee kudai haki zao hususani upatikanaji wa huduma za afya bure.
Bi. Cotrida Kokupima, Katibu Mtendaji SAWATA KASULU

Aidha wazee waliohudhuria semina hiyo wamekiri kukosa haki nyingi hususani za kiafya na kiuchumi jambo ambalo ni hatari kwa uhai wao, na wameahidi kufuatilia uundwaji wa mabaraza hayo.

Jumla ya wazee 31 wawakilishi kutoka kata za Murufiti na Nyamidaho wilayani Kasulu wamehudhuria semina hiyo ya utambuzi wa haki na wajibu.


Wakati huo huo Wito umetolewa kwa jamii kuwajali wazee kwa kuwapa huduma muhimu za kijamii ili kuwapunguzia msongo wa maisha 

Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti wa asasi ya Saidia Wazee Tanzania wilayani Kasulu Mzee 
Jackson Bukuru wakati akitoa mwongozo wa huduma kwa wazee wasiojiweza wilayani Kasulu


Mzee Bukuru amebainisha kuwa vijana wameacha desturi ya kuwahudumia wazazi wao jambo ambalo linachangia wazee kukata tamaa. 

Amesisitiza kuwa, endapo vijana hawatarejesha moyo wa kujali wazee ni vema nao wasirejee kwa wazee wanapokuwa na matatizo au kuzidiwa kwa ugonjwa

PRESS RELEASE FROM UNITED NATION

Written By Unknown on Alhamisi, 10 Julai 2014 | 05:46






Malaria Prevention during Pregnancy Improves
Health of Mothers and Babies

Roll Back Malaria (RBM) partners launch new report and call for renewed commitment from health & development community

(10 July 2014; New York)  A new report highlighting the impact of malaria interventions on maternal, newborn and child health was launched today alongside the annual High-Level Segment of the United Nations Economic and Social Council (ECOSOC) in New York.

The Contribution of Malaria Control to Maternal and Newborn Health is the latest in the Roll Back Malaria (RBM) Partnership’s Progress & Impact Series to help assess progress towards targets set out in the Global Malaria Action Plan (GMAP) and the United Nations Millennium Development Goals (MDGs).

Co-authored by the Liverpool School of Tropical Medicine, the report includes contributions from various Roll Back Malaria partners and shares evidence that intermittent preventive malaria treatment during pregnancy and the use of insecticide-treated mosquito nets (ITNs) can reduce the risk of death to malaria within the first 28 days of life by 18%. Authors also highlight that these protective tools can decrease low birth weight deliveries by 21%.

“Each year, there are an estimated 125 million pregnancies in areas of high malaria transmission around the world, resulting in some 83 million live births,” noted RBM’s acting Executive Director, Dr. Thomas Teuscher. “Pregnant women in malaria endemic areas have a 50% higher risk of malaria infection during pregnancy than non-pregnant women. We must do everything we can to protect these precious moments and allow all women the opportunity to safely carry and deliver their child without the risk of this killer disease.”   

Between 2009 and 2012, an estimated 94,000 newborn deaths were averted as a result of the scale-up of these malaria interventions during pregnancy. Countries attaining high coverage and use of malaria control interventions during this period saw child mortality rates fall by as much as to 20%. Effective roll-out and use of these proven preventive measures contributes positively to the achievement of the MDGs – especially those related to maternal health improvement and reduction of under-five mortality – while also allowing progress against broader targets by contributing to a healthier and more vibrant society.

Despite these advances, malaria in pregnancy still exerts a heavy toll and contributes largely to maternal and neonatal mortality. In Africa, 10,000 women and between 75,000 and 200,000 children under the age of one are estimated to die annually as a consequence of malaria infection during pregnancy. Malaria is a major cause of anaemia in pregnant women, and can lead to maternal death at delivery due to haemorrhage. It is also responsible for stillbirth, preterm birth, and low birth weight, which increases the risk of death within the first days of the child’s life.

The notable results outlined in the report have been achieved with generally low levels of intervention coverage across sub-Saharan African countries, suggesting the highly effective nature of malaria prevention efforts during pregnancy and the need for greater collaboration to ensure stronger protection among this key population. Authors note that an estimated 300,000 neonatal deaths could have been averted had an 80% coverage of these interventions been achieved between 2009 and 2012.

While launching the report in New York, RBM partners called for renewed commitment and greater collaboration between the maternal health and malaria communities to increase access to interventions and maximize the impact of efforts. With some 500 days until the 2015 deadline of the MDGs and a challenging financial landscape, continued partnership to scale-up delivery of these life-saving interventions will be critical to ensuring mothers and children are able to lead healthy lives and contribute to their communities.

The report will be available online on 10 July at:

# # #



Media Contact:
Mr. Hervรฉ Verhoosel
RBM Representative in New York and Head of External Relations

Mr. Trey Watkins
RBM External Relations Officer


About the Roll Back Malaria Partnership (RBM)
The Roll Back malaria Partnership was founded by UNICEF, WHO, UNDP and the World Bank in 1998 as a global framework to coordinate global action against malaria. Today, RBM is a global public-private partnership made up of more than 500 organizations across sectors that provides a neutral platform for consensus-building, developing solutions to challenges in the implementation of malaria control interventions and strategies, promotes high-level political commitment to keep malaria at the top of the global agenda, and monitors progress towards universal goals.


MWENEZI WA CCM JELA BAADA YA KUTANGAZA UJIO WA MAKAMU MWENYEKITI WA CCM TAIFA

Written By Unknown on Jumatano, 9 Julai 2014 | 11:35

Bw. Philip Mangula (katikati) akiwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dr. Amani Kaborou (kushoto) na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Uvinza Bw. Muhamed Kabambe (kulia)

Ziara ya makamu mwenyekiti wa ChamaCha Mapinduzi CCM Bw. Philip Mangula Imeingia dosari baada ya mmoja wa viongozi wa chama hicho wilayani Uvinza kufungwa jela baada ya kutumia vipaza sauti
 

Mahakama ya Mwanzo Nguruka wilayani Uvinza mkoani Kigoma, imemhukumu kifungo cha mwezi mmoja Jela, katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Uvinza kwa kosa la kuipigia kelele mahakama.

Tukio hilo limetokea leo wakati kiongozi huyo Bw. Majaliwa Zuberi alipotumia vipaza sauti ndani ya ukumbi wa CCM kutangaza ujio wa makamu mwenyekiti wa CCM Taifa Bw. Philip Mangura katika wilaya hiyo

Kufuatia sauti hiyo kusambaa nje ya ukumbi huo, Hakimu William Kamugisha alitoa agizo la kukamatwa kwa Bw. Zuberi na kisha kumhukumu kwenda jela kwa kosa la kuvuruga mahakama.

Hakimu Kamugisha anaeleza kuwa, Bw. Zuberi alikaidi agizo la mahakama lililomtaka apunguze sauti na kwamba alitoa majibu ya jeuri mbele ya mahakama hiyo.

Viongozi wa CCM mkoa wa Kigoma wamepinga vikali hukumu hiyo na kueleza kuwa imegubikwa na hisia za kisiasa.

Wameeleza kuwa mwenezi huyo hakuwa eneo la mahakama hiyo, na wamemtaka Bw. Mangula kuagiza mamlaka za dola kuchunguza uadilifu na utendaji kazi wa hakimu huyo.

MWANAMKE AUWAWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA KIGOMA

Written By Unknown on Jumatatu, 7 Julai 2014 | 06:22

Sehemu ya mji wa Kasulu barabara kuu iendayo Burundi kupitia Kijiji cha Heru juu




Mwanamke mmoja mkazi wa kijii cha Herujuu wilayani Kasulu mkoani Kigoma, amefariki dunia baada ya kushambuliwa na wananchi

Tukio hilo limetokea mapema leo baada ya kundi kubwa la wananchi kuvamia makazi ya mwana mke huyo Bi. Apolonia Bwire na kuanza kumpiga kwa mawe wakimtuhumu kuhusika na vitendo vya kishirikina

Jeshi la polisi wilaya Kasulu limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba limejaribu kumuokoa mama huyo akiwa amejeruhiwa vibaya na kumkimbiza hospitali.

Muuguzi wa zamu katika hospitali ya wilaya ya Kasulu Bi. Agnes Bukombe amethibitisha kufariki kwa mwanamke huyo na kutaja kuwa kifo chake kimetokana na kuvuja damu nyingi.

Nyumba mbili za mwanamke huyo zimeteketezwa kwa kuchomwa moto na mali mbalimbali kuporwa na namia ya wananchi waliozingira makazi hayo.
 
Shukrani kwa : Harold Dickson | Prosper Kwigize | 0752490120
Copyright © 2013. KWIGIZE NEWS AND COMMUNICATION - Haki zote zimeifadhiwa
Email us: kwigizenews@gmail.com
0764243377