Pichani ni Jengo la Halmashauri ya wilaya ya Iramba mkoani Singida, Iramba inasifika kwa kuw ana mikakati mahili ya kuboresha afya za wananchi kupitia katka kuchangia mfuko wa afya ya jamii CHF
Na. Prosper Kwigize
Halmashauri ya wilaya ya Iramba imepongezwa kwa kuwa ya
kwanza kitaifa katika ukusanyaji wa michango na idadi ya wananchama nchini
Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa takwimu na uhai wa bima
ya afya taifa Bw. Michael Mhando wakati akitoa maelezo ya hali ya mfuko wa
taifa wa bima ya afya katika kongamano linalofanyika mkoani Singida kujadili
maendeleo ya mfuko huo
Bw. Mhando amebainisha kuwa hadi june mwaka huu mkoa wa
Singida umesajili wanachama wachangiaji 12,537 na idadi ya wanaonufaika ni 68,
210
Aidha amewataka waajili wote kuhakikisha wanawahamasisha
watumishi wao kujiunga na kuchangia mfuko wa bima ya afya na mfuko wa afya ya
jamii ili kuondokana na changamoto za kupata matibabu wanapougua.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dr. Parseko Kone amesema viongozi
wengi hawajatimiza wajibu wao wa kuwahamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa
afya ya jamii CHF mkoani Singida
Dr. Kone amebainisha kuwa katika kipindi cha January hadi
septemba 30 mwaka huu jumla ya kaya 45,575 kati ya 259251 sawa na asilimia
17.6% wamejiunga ma mfuko wa afya ya jamii mkoani Singida
Kutokana na idadi ndogo ya wanachama Mkuu huyo wa mkoa
ameagiza wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Singida kuhakikisha wanapatia taarifa
kila baada ya miezi miwili ikionesha ni wanachama wangapi wapya wamejiunga na
mfuko huo wa afya ya jamii CHF
Aidha Dr. Kone amemuagiza mganga wa mkoa Dr. Doroth
kuhakikisha anaitisha kikao cha waganga wote wa wilaya kabla ya tarehe 30 mwezi
huu ili kujadili na kuamua namna bora ya kuandikisha wanachama wapya na utoaji
wa huduma bora kwa wanachama
Ameonya pia tabia ya waganga kutowathamini wanachama katika
kuwapa huduma na kujali wanaolipa esa tasilimu dirishani na kusisitiza kuwa
kitendoo hicho kina tafsiri ya ufisadi kwa pesa zinazolipwa na wasio wanachama
wa mifuko ya afya ya jamii
Kufuatia hali hiyo Dr. Kone ametoa wito kwa wanachama
watakaobaguliwa katika vituo vya afya na hospitali pindi wanapohitaji matibabu
kutoa taarifa kwa kiongozi yeyote wa serikali ili madaktari hao wachukuliwe
hatua