Ni
ukweli usio na upinzani kuwa mkoa wa Kigoma unawasanii wa pekee sana katika
anga la muziki wa dance na sasa kizazi kipya yaani Bongo flavor
Ni
Kigoma ambayo hadi sasa imejizolea sifa kwa kuwa na wasanii wenye mvuto,
mashairi, midundo na sauti zinazovutia kusikiliza kila mara
Kigoma
ndiko unakoweza kukutana na wasanii wakongwe kama vile Linex, Baba levo, Banana
zoro na wanafamilia wenzake akiwemo Zahir Ally Zoro, Biziman (Bhizimana),
Rachel, Ali kiba na mdogo wake Abdul
Kiba, Msechu, Chege na wengine wengi wanaovutia majukwaa, vituo vya Radio na
Runinga Tanzania na nje ya afrika mashariki
Ukweli
ni kwamba wapo wengi ambao wanaendelea kuibuka, siwezi kuwasahai Mvyeyi Nembo,
Simple Boys clew wa mjini Kasulu na wengine wengi
Leo
nimekutana na Kijana YOhana kabla ya yote nikamtaka anikumbushe historia yake
na anipe japo singo moja kwa ajili ya msomai wa blog hii na hapa akinipa mambo
Naitwa
YOHANA BANGUZE nilizaliwa wilaya ya kasulu mkoa wa kigoma mnamo mwaka 1986, nimehitimu
elimu ya sekondari 2009 KASULU HIGH School, kazi yangu ni muziki,huu ni wimbo
wangu mpya uitwao NYUMBANI NI WAPI, natarajia kuufanyia video yake mezi wa 12
mwaka huu,KING WALONG ndo jina langu la sanaa,nahitajiushirikiano wakoo ktk
kuutangaza muziki wa tanzania Africa na dunia.
Huyo
ndiye WALONG kuoka Kasulu Kigoam ambaye amekuwa akifuata nyayo za watangulizi
wake LInex na Baba levo, kwa kuimba katika mahadhi ya kiha na kuchanganya lugha
na misemo ya Kirundi na Kinyarwanda ili kuvutia soko la afrika mashariki
Kibao
chake cha SALUFUNE kipo katika blog hii angalia katika ukurasa wa sauti muziki
na habari kwa sauti utaiona au tembelea facebook