HABARI MPYA
blink

BURUANI KATIKA FILAMU- MFAHAMU JET LI

Written By Unknown on Alhamisi, 24 Aprili 2014 | 06:32

Jet Li
Li Lianjie (amezaliwa tar. 26 Aprili 1963) ni mshindi wa Tuzo za Filamu za Hong Kongo, akiwa kama mwigizaji bora filamu wa Kichina. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Jet Li. Jet Li ni mtaalam wa Kung Fu na Wushu. Baada ya miaka mitatu ya mafunzo ya Wushu, Jet Li alipata ushindi wake wa kwanza katika mashindano ya kitaifa ya vikosi vya Wushu kwa mji wa Beijing. Akiwa na umri wa miaka 17, Jet Li aliachana na masuala ya Uwushu na badala yake akaja kuwa mwigizaji wa filamu na akabahatika kutoa filamu yake kwanza mnamo mwaka wa 1982 na filamu ilikwenda kwa jina la Shaolin Temple. Badala ya hapo akawa anaendelea zaidi na maswala ya filamu na hata kuweza kujulikana katika medani hiyo ya uigizaji wa filamu katika China. Akaja kujipatia umaarufu zaidi pale alipocheza katika mfululizo wa filamu za Once Upon a Time in China, ambamo humo alikuwa akicheza kama shujaa wa kiasili - Wong Fei Hung. Kwa upande wa Marekani, Jet Li alianza kucheza kama adui katika filamu ya Lethal Weapon 4 kunako mwaka wa 1998, na kwa upande wa filamu alizocheza Marekani kwa mara ya kwanza na kuwa kama nyota kiongozi ilikuwa katika Romeo Must Die ya mwaka wa 2000. TANZAMA MOVIE ZAKE HAPA

HOTUBA YA RAIS KIKWETE NA JAJI WARIOBA -BUNGE LA KATIBA

Written By Unknown on Jumatatu, 21 Aprili 2014 | 05:02




 chanzo: youtube: Husein Hassan

HOTUBA ZA VIONGOZI KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA MPYA NCHINI TANZANIA NI MOJA YA MAMBO MUHIMU YANAYOTAKIWA KUSIKILIZWA NA WAJUMBE WAJIPE MUDA NA NAFASI YA KUTAFAKARI.

HII NI KUTOKANA NAUKWELI KWAMBA KUMEKUWA NA MIVUTANO KUTOKA KWA MAKUNDI YANAYOKINZANA KIFIKIRA, KIMLENGO NA KIMTAZAMO BILA KUSAHAU ITIKATI ZA KISIASA

KWA KUTAMBUA HAYO UKURASA HUU UNAKULETEA HOTUBA HIZO

Chanzo: MCL

WEMA SEPETU KUMVAA MRISHO NGASA LEO UWANJA WA TAIFA

Written By Unknown on Jumamosi, 19 Aprili 2014 | 06:55

http://kwigizenews.blogspot.nl/2014/04/wema-sepetu-kumvaa-mrisho-ngasa-leo.html


Katika hali inayovuta hisia za wengi, leo msanii maarufu ambaye pia amewahi kuwa miss Tanzania ametangaza kumfuata Mchezaji maarufu anayetajwa kuhama timu za Bongo kuliko wengine Mrisho Ngasa uwajani

Akiongea na vyombo vya habari Wema ametaja kuwa hana tabia ya kwenda kutazama mechi lakini leo atashuhudia mtanange baiana ya Simba na yanga ili baada ya mechi akutane na ngasa na kudai deni lake


Waswahili wanasema, “Ahadi ni Deni”, Wema anataja kuwa anamdai Ngassa ahadi ya mpira.

TAJIRI ATOA MABILIONI KUDHIBITI SILAHA

Written By Unknown on Jumatano, 16 Aprili 2014 | 06:38


Meya mstaafu wa Jiji la New York City nchini Marekani Michael Bloomberg ametangaza kutoa dola milioni 50 mwaka huu kwa ajili ya kujanga mtandao wa  kupunguza kuzagaa na matumizi ya silaha katika uharifu
Mkakati huo mpya ameutangaza katika gazeti la The New York Times, fedha hizo zitatumika katika kuhakiki kwa kina biashara ya silaha katika serikali na nchi kwa ujumla
Amesisitiza kuwa kipaumbele katika uhakiki na udhibiti wa silaha kitaelekezwa kwa wanawake katika mpango mkakati wa nje wa udhibiti wa silaha, na kwamba taasisi mbalimbali zitahusika
Imeelezwa kuwa mkakati huo utawavutia zaidi ya waungaji mkono milioni mbili na laki tano kuchangia
Soma zaidi hapa 

HOJA YA MUUNGANO NA IDADI YA SERIKALI TANZANIA

Written By Unknown on Jumanne, 15 Aprili 2014 | 13:22


Je! marumbano yanayoendelea Bungeni ya juu ya mfumo wa Muungano na idadi ya serikali yanalenga kuwezesha vyama vya upinzani kushinda na kutawala Tanganyika?

Na je Bunge kutekwa na Muungano na idadi ya serikali, Je rasimu ya pili ya Katiba haina hoja nyingine zaidi ya hizo?

Tafadhari piga kura yako, chagua jibu upendalo katika hukurasa huu sehemu ya chini kulia

BUNGENI HALI BADO TETE MMAMUZI YA SERIKALI NGAPI - VIDEO HAPA


Mbunge wa Iramba magharibi Mheshimiwa Mwigulu Nchemba asisitiza kuwa Tanzania itaendelea kuwepo na serikali mbili ndo mwafaka kuepka gharama

Tazama video toka Bungeni kwa Hisani ya TBC na Mwigulu Nchemba

TUNATOA POLE KWA WATANZANIA KWA KIFO CHA MZEE NGURUMO

Written By Unknown on Jumatatu, 14 Aprili 2014 | 09:28

kwigizenews
Mzee Ngurumo enzi za uhai wake akipokea ufuguo wa Gari kutoka kwa Manamuziki Diamond mara alipotangaza kustaafu muziki na kuhitaji misaada kutoka kwa waungwana ili kumudu maisha.

KWIGIZE NEWS .COM Tunatoa pole kwa wanafamilia ya mwanamuziki nguli wa Tanzania marehemu Mzee Maalim Ngurumo kilichotokea jana katika Hospitali ya Taifa mhimbili alikokuwa amelazwa. kwa kumuenzi blog yetu imeweka wimbo (mtanikumbuka) ambao waliutunga na kuimba pamoja na Marehemu TX Moshi, hii ni moja ya kutoa pole kwa Watanzania. bonyeza hapa kutazama video

KABURI LA SHEIKH YAHAYA (MTABIRI MAARUFU) LAVUNJWA

Written By Unknown on Jumamosi, 12 Aprili 2014 | 06:40


Marehemu Sheikh Yahya enzi za Uhai wake.

Ndugu Wanahabari,
Assalam Aleykum
Kama mnavyojua kwamba kumetokea tukio la kusikitisha  la kuvunjwa kwa Makaburi ya Masheikh Wetu, wapendwa wetu,  wazazi wetu na viongozi wetu wa Dini  ya Kiisalam, Marehemu Sheikh Yahya Hussein Na Marehemu Sheikh Kassim Bin Juma, Usiku wa kuamkia tarehe 10/4/2012 katika viwanja vya Makaburi ya Tambaza Jirani na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Tukio hili, licha ya kusikitisha lakini limeziingizia fedheha  Familia hizi mbili za Masheikh Hawa na Kwa Waisalamu kwa Jumla. Kwa Desturi na Sheria, Viwanja vya Makaburi ni mahala panapotakiwa Kuheshimiwa kutokana na ukweli kwamba ni moja wapo ya sehemu za Ibada.

Hivyo basi kutokana na Tukio hilo ni dhahiri kwamba waliofanya kitendo hicho wamekiuka mafundisho ya Dini ya Kiislamu  na hivyo kutenda kosa ambalo kiimani linaweza kusababisha Madhara Makubwa kwao wenyewe, Jamii na Taifa kwa Jumla.

Kwa muktadha huo basi Familia ya Marhum Sheikh Yahya Hussein imeumizwa kwa kiwango cha juu na tukio hilo hasa ikizingatiwa kuwa  Makaburi yaliyovunjwa ni la baba yetu na la aliyekuwa swahiba wake  mkubwa Mzee wetu Sheikh Kassim Bin Juma Pekee.

Hali hii inaonyesha kwamba kuna Chuki Binafsi, Udhalilishaji na Njama  za Kuhujumu familia yetu, Dini yetu na Waislamu kwa Jumla na hivyo kitendo cha aina hii kinaweza kuliingiza Taifa katika migogoro isiyo na Tija, kidini, Kisiasa, kiuchumi na kimaendeleo ya Jamii.

Hata hivyo Familia ya Marhum Sheikh Yahya Hussein imefarijika kuona uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Dar es salaam  Pamoja na Baraza Kuu La Waisalamu wa Tanzania (BAKWATA) chini ya Mufti wa Tanzania Sheikh Mkuu Issa Bin Shaaban Simba kulishughulikia kwa haraka suala hili katika mawanda ya kuthamini, Mila, Desturi na Ibada za Makaburi.

Hatua hiyo inaonyesha ni jinsi gani Jamii nzima ilivyoguswa na kadhia hiyo ambayo inahatarisha Usalama wa Nchi na raia kwa sababu Waumini na wananchi wengine ambao ni wapenzi wa Viongozi hao wa Kidini wanaweza, kutokana imani zao, kujichukulia sheria mikononi.

Hata hivyo uongozi wa Serikali Mkoa wa Dar es salaam na vyombo vyake bado unatakiwa kuwa makini katika maagizo yake na utekelezaji wa kazi zake hasa katika sehemu ambazo zinagusa hisia za watu kama Makaburi na sehemu za Ibada ili kuepuka matukio yenye sura ya Hujuma kama tukio hilo la makaburi ya Tambaza ambayo yanaweza kuleta mtafaruku ndani ya jamii na kuvunjika Amani ya nchi.

Sisi kama Familia Ya marehemu Sheikh Yahya Hussein tunaiomba Serikali na vyombo vyake iwasake na kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote waliohusika na hujuma hizi.

Pamoja na hayo familia inaona kwamba dawa ya kuepukana na matatizo kama haya ni kujenga uzio katika eneo hilo ili kuhifadhi Makaburi hayo. Kwa hiyo tunaiomba Manispaa ya Wilaya ya Ilala ijenge uzio katika  eneo la Makaburi ya Tambaza.

Kwa upande wetu, pamoja na nia nzuri ambayo Serikali imeonyesha ya kutaka kuyajenga tena Makaburi hayo, lakini sisi kama Familia ya Sheikh Yahya Hussein na Sheikh Kassim Bin Juma tumeamua kwamba tutajenga Makaburi  ya wazazi wetu kwa gharama zetu wenyewe.

Wabillahi Tawfiq
Alhajj Maalim Hassan Yahya Hussein
( Kwa niaba ya Familia )

QUEEN DERLEEN NA SHILOLE WAFANYA MAMBO


SHILOLE alimaarufu mama wa viono amefanya mambo mazito katika video ya Queen iliyotoka, hebu jionee vitu vya walembo hawa wa kitanzania wanaowika katika anga la muziki afrika mashariki

Bofya hapa Queen na Shilole

Kazi hii inakuja huku kukiwa na ushindani mkubwa baina yao na Sinura ambaye hivi karibuni ametamba kuwapiga bao kwa mashairi na matumizi bora ya kiuno jukwaani



MUZIKI WA MSANII DIAMOND NA MAUDHUI YAKINIFU


Msanii wa muziki nchini Tanzania Diamond anatajwa kuwa miongoni mwa wasanii wenye mvuto mkubwa kwa watanzamaji na wasikilizaji wa nyimbo zake, hii ni kutokana na mashabiki kuyakubali mashairi na miondoko yake katika uimbaji



Muziki ni moja kati ya sanaa muhimu sana ambazo zimekuwa kivutio katika burudani miongoni mwa jamii ndani na nje ya Tanzania.

Muziki umekuwa pia ukitumika katika kuibua mjadala, kuchochea maendeleo pamoja na kueneza habari Fulani kwa jamii.

Wanasiasa pia wamekuwa wakiwatumia wasanii katika kueneza sifa zao na propaganda za vyama vyao ili kushawishi wananchi kuzikubali sera zao na kuwachangua katika nafasi wanazoomba.

Nchini Tanzania muziki umekuwa ukibadilika siku hadi siku ukihama kutoka katika ushairi wa kawaida wa kuelimisha jamii na kuhamia katika mapenzi zaidi, baadhi ya wasanii huimba mapenzi tu na wengine huchanganya mapenzi na masuala mengine ya kijamii.

Wasanii wengine huimba tu ilimradi waamshe hisia za kucheza hata kama wimu unaoimbwa hauna maudhui yoyote zaidi ya kukolezwa na vyombo vya kisasa vya kutengeneza milindimo na vionjo vitamu.

Katika makala haya nimevinjali baadhi ya nyimbo za Diamond kutoka Tanzania na kupata hoja ya kukueleza.

Wasanii kote Tanzania wameaminishwa na wapenzi wao (wasikilizaji na watazamaji wa muziki) na sasa wanadhani nyimbo nzuri ni ile inayoimba mapenzi na kutonesha ama kidonda cha penzi au kuanzisha hisia mpya ya mapenzi.

Ni kwa sababu hiyo wengi wao wamekuwa  wakitunga na wakiimba nyimbo za mapenzi tu, na kwa bahati mbaya wanasahau mambo mengine ya kijamii.

Diamond katika wimbo wake wa Mbagala, alifanya muziki wenye muonekano na vionjo vya mapenzi lakini ndani yake kuna jambo muhimu sana la kijamii, ambalo nina hakika ndilo linabeba maudhui yote ya wimbo wake.

Diamond anamkosa mrembo aliye mpenda sana kwa sababu mazingira anapoishi ni machafu na hatari kwa afya za wakazi wa maeneo ya Mbagala
Angalia video hii na utume maoni yako  bofya hapo kwenye neno mbagala uone kisha tutumie maoni yako kuhusu wimbo huo na maudhui yake, anuani yetu ni plen.media@gmail.com


NAFASI YA MASOMO ULAYA KWA WAANDISHI WA HABARI

Written By Unknown on Jumanne, 1 Aprili 2014 | 06:48


Kwa waandishi wa habari wanaopenda kuongeza elimu na ujuzi zaidi, Kituocha mafunzo cha radio Netherlands Training Center kimetangaza nafasii za kutosha kwa taaluma mablimbali, wahi na wanatoa ufadhili

tembelea mtandao huu MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI ULAYA
 
Shukrani kwa : Harold Dickson | Prosper Kwigize | 0752490120
Copyright © 2013. KWIGIZE NEWS AND COMMUNICATION - Haki zote zimeifadhiwa
Email us: kwigizenews@gmail.com
0764243377