Mkuu wa mkoa wa Morogoro ndg. Joel Bendera |
Wananchi katika eneo la Kibaoni wilayani Mvumero mkoani
Morogoro ambao wamekuwa katika heka heka za siku nyingi wakilalamikia ardhi yao
kupokonywa na kupewa mwekezaji, leo wanafanya sherehe baada ya ekali 500
kurejeshwa mikononi mwao
Hayo yametibitishwa na uongozi wa mkoa wa Morogoro ambao hivi
karibuni umeshuhudia vurugu na vita kali kati ya wakulima, wafugaji na
wawekezaji wambao wanatajwa kuteka sehemu ya kilimo na ufugaji
Watu kadhaa waliripotiwa kupoteza maisha kutokana na migogoro
ya ardhi mkoani Morogoro katika kipindi cha June hadi octoba mwaka huu
Maoni yetu ardhi kwa sasa haipaswi kusababisha vita, si
Tanzania hatulilii ardhi kama wenzetu wa Kenya na Uganda, Nurundi na Rwanda,
kinacholeta shida ni kukosekana kwa sera nzuri ya ardhi inayoweza kuongoza
matumizi yake na mahitaji ya wananchi hususani wakulima na wafugaji