Viongozi wa serikali ya Mseto, Katikati ni Angela Markel aliyeshinda katika uchaguzi uliomalizika hivi karibuni |
Kwa mara ya kwanza katika historia chama cha upinzani cha SPD
ambacho kilishindwa katika uchaguzi mkuu wa Ujerumani uliofanyika hapo mwezi wa
Septemba kiliwataka wanachama wake wapige kura kuridhia chama hicho kujiunga
katika serikali ya mseto chini ya uongozi wa Kansela Angela Merkel
Chama cha Angela Merkel kilishinda katika uchaguzi mkuu
huo.Matokeo ya kura hiyo ingelikuwa ya "hapana" ingelibidi kufanyike
mazungumzo mapya ya kuundwa kwa serikali hiyo ya mseto.
Katika
ngazi ya kitaifa ya serikali ya Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani kulikuwako
mara mbili kwa serikali za muungano mkuu.Kwa mara ya kwanza serikali hiyo
iliundwa kati ya vyama ndugu vya CDU/CSU na chama cha SPD hapo mwaka 1966.
Mara ya pili serikali hiyo ya muungano mkuu iliundwa hapo mwaka
2005 hadi 2009 na kuungozwa na Kansela Angela Merkel.