Polisi wakipiga doria kulinda waandamanaji ilikusitokee vurugu au uvunjaji wa amani katika manspaa ya Kigoma ujiji (picha kwa hisani ya Hamis full migebuka -Kigoma) |
Mamia ya wakazi wa mji wa Kigoma na vitongoji vyake leo
wameandamana katika mitaa mbalimbali pamoja na kuchoma bendera na kadi za chama
cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kupina ziara ya katibu mkuu wa chama hicho
Dr. wilborad Slaa
Hatua hiyo ya maandamano ni ya pili kufanyika mjini Kigoma
hususani katika jimbo la Kigoma Kaskazini kwa kile kinachotajwa kuwa ni kupinga
kuvuliwa uongozi mbunge wa Kigoma kaskazini Zitto Kabwe
Imeelezwa kuwa maandamano hayo yanasisitiza kutokukubaliana
na uamuzi wa kamati kuu ya CHADEMA kumuondoa Zito katika nafasi ya Naibu katibu
mkuu na naibu kiongozi wa upinzani Bungeni
Katibu mkuu wa CHADEMA Dr. wilbroad Slaa yuko Mkoani Kigoma
tangu juzi na amekuwa akikumbwa na dhahama la mabango na kuzomea katika maeneo
aliyokwenda kuhutubia
Aidha katika hali ya kushangaza, leo amehutubia katika maeneo
ya vijijini na kuruka maeneo yenye watu wengi katika wilaya ya Kasulu ingawa
imeelezwa kuwa jumapili ndipo atahutubia mjini Kasulu
Vuguvugu la kupinga ziara hiyo bado linadhihirisha miongoni
mwa wafuasi cha chama hicho ikiwa ni pamoja na Baraza la Vijana la Chadema
BAVICHA ambao inaelezwa kuwa wamejiandaa kufanya vurugu, kuzomea na kumunyoshea
mabango Dr. Slaa