Jumuiya ya afrika mashariki inatarajia kutekeleza mpango
mkakati wa maendeleo ya jumuiya kufuatia kupatiwa kitita cha shilingi bilioni
mia moja na tano kutoka Finland
Serikali ya Finland imetangaza hayo mapema wiki hii katika
mkutano wa jumuiya hiyo uliofanyika katika makao makuu ya Jumuiya ya afrika
mashariki mkoani Arusha nchini Tanzania
Katika mkutano huo uliofanyofanyika katika Hotel ya Mount
Meru Mjini Arusha, Finland imeahidi kutoa fedha hizo ili kusaidia jumuiya
ktekeleza shughuli zake kwa ufanisi zaidi
Jumuiya ya Afrika mashariki inatekeleza miradi mbali mbal ya
maendeleo katika eneo lote la nchi washirika ikiwemo ujenzi wa daraja la Mto
Kagera eneo la Rusumo wilayani Ngara
Miradi mingine ni Ujenzi wa soko la pamoja katika eneo la
Namanga mpakani mwa Tanzania na Kenya katika eneo la mkoa wa Arusha pamoja na
miradi mingine ya mazingira katika bonde la ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika.
Miradi ya afrika mashariki baahi yake hufadhiriwa pia na
Benki ya dunia pamoja na benki ya maendeleo ya Africa.
Endapo hakutakuwa na matumizi mabaya ya fedha hizo upo
uhakiki wa kuibuka kwa mapinduzi makubwa katika sekta za kiuchumi na kijamii
kwa wakazi na nchi za afrika mashariki