Siku moja tu baada ya
mazishi ya aliyekuwa Rais wa kwanza mweusi na mpigania Uhuru wa Africa kusini
Nelson Mandela, Sanamu kubwa zaidi duniani inayomuonesha akihamasisha umoja na
maridhiano imezinduliwa katika mji mkuu wa Afrika kusini Pretoria
Sanamu hiyo
iliyotengenezwa kwa shaba ina urefu wa mita tisa na ina uzani wa tani nne
unusu. Ilizinduliwa katika bustani la majengo ya bunge na inaonyesha Nelson
Mandela akihimiza umoja na maridhiano.
Sanamu hiyo yenye
mikono ya Mandela ikiwa wazi ilinuiwa kuonyesha Mandela alivyoliungaisha taifa
zima kwa mapenzi yake.
Familia ya Madiba ,
viongozi wa ANC , viongozi wa Afrika na maafisa wengine wakuu walihudhuria
mazishi hayo katika kijiji cha Qunu mkoani Cape Mashariki.
Mandela anakumbukwa
kwa juhudi zake za kupatanisha wananchi na kupigia debe msamaha miongoni mwa watu
na ndio maana leo ikawa siku iliyotengwa kwa ajili ya uzinduzi wa sanamu hiyo.
Wakati wa utawala wa
wazungu, terehe 16 Disemba ilijulikana kama siku ya kuwakumbuka mashujaa wa
Afrikaners walioshinda vita dhidi ya jeshi la Zulu mwaka 1883.
Zaidi ya karne moja
baadaye mwaka 1961, Mandela alizindua jeshi lake la Umkhonto we Sizwe kupigana
dhidi ya utawala wa wazungu.
Kuanzishwa kwa jeshi
hilo la wazalendo chni ya uongozi wa Mandela kuliongeza hasira ya wazungu
kumsaka na hatimaye kumkamata na kumhukumu kifungo cha maisha jela kwa kosa la
uhaini