Home » » NELSON MANDELA AAGA DUNIA

NELSON MANDELA AAGA DUNIA

Written By Unknown on Ijumaa, 6 Desemba 2013 | 04:22



Kuanzia alfajiri ya leo December 06 2013, bendera ya taifa Tanzania pamoja nay a chama cha mapinduzi kinachotawala serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania zinapepea nusu mlingoti kuashiria kuwepo kwa tukio la simanzi au msiba kwa taifa hilo.

Upepeaji huo wa bendera nusu mlingoti ni matokeo ya utekelezaji wa agizo la Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete alilotoa usiku wa kuamkia leo muda mfupi baada ya rais wa Africa kusini Jacob ZUma kutangazia ulimwengu kuwa baba wa Taifa la Africa kusini na afrika Nelson Madiba Mandela amefariki dunia

Pembe zote za Tanzania zimeshikwa na simanzi kubwa kufuatia kifo cha Baba wa Taifa rafiki kwa Tanzania, watanzania wamekuwa na maoni tofauti kuhusu kifo hicho huku wengine wakidiriki kutaja kuwa nuru ya afrika sasa imegeuka giza nene kutokana na kifo cha Nelson Mandela

Kutoka hapa Tanzania eneo la mkoa wa Kigoma nimekutana na baadhi ya waombolezaji ambao hwasiti kutoa hisia zao

“Mandela ni mtu muhimu kwa bara la afrika, amekuwa kiongozi mwadilifu na mwaminifu kwa nchi yake na kwa afrika nzima” Lucas Yona mkazi wa Kasulu

Huyo ni mmoja wa wanaume ambao wanakiri kuwa baba wa taifa lla afrika ambalo hadi anaondoka angependa kuwepo na umoja wenye nguvu ya kisiasa na kiuchumi

Wanawake nao hawako nyuma katika kuenzi mchango wa Mandela katika ustawi wa afrika, huyu hapa ni mwanamke mwanaharakati na kiongozi wa umoja wa wanawake katika eneo la wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma

Grace Mbwiriza ni katibu wa Umoja wa wanawake Tanzania wilayani Kasulu, anamuona Mandela kama kioo cha afrika ambacho kilitumika kujenga hoja ya uafrika na uzalengo kwa waafrika

Chama cha mapinduzi sit u kimeshusha bendera yake nusu mlingoti bali pia viongozi wake ngazi ya taifa wanajipanga kushiriki katika shughuli za kumuenzi Mandela pamoja na kushiriki mazishi yake

Aidha viongozi hao wa chama ambacho kilishirikiana na chama cha ukombozi wa weusi wa afrika kusini ANC kuhakikisha makabulu wanaacha ubaguzi, hapa katibu wa CCM wiiaya ya Kasulu anaeleza hisia zake kuhusu kifo cha Mandela

“Mandela licha ya kuwa mpigania haki alikuwa mwenye upendo na huruma kiasi cha kuwahurumia adui zake na adui wa waafrika yaani makaburu ambao waliwanyonya na kuwanyanyasa waafrika”

Kitendo cha Mandela kuwasamehe bila kuwachukulia hatua za kisheria waliomweka gerezani kwa zaidi ya miaka 20 tena kwa uonevu pamoja na vitendo vya ubaguzi wa rangi, kulimkweza sana Mandela na kudhihirika kweli kama mkombozi wa kweli
Je Chama cha mapinduzi kinasemaje kuhusu msimamo huo wa Mandela? Bw. Minja katibu wa CCM anatanabahisa kuhusu msimamo huo wa hayati Mandela

Kwa niaba ya waandishi wa habari na wawakilishi wa channel afrika katika eneo la maziwa makuu pamoja na familia yangu tunatoa pole kwa wanafamilia ya marehemu Mandela pamoja na taifa zima la afrika kusini kwa kuondokewa na mwasisi wa ukombozi wa watu weuzi nchini afrika kusini, Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe

Kutoka Dar es Salaam kwa hisani ya Facebook, Mwanahabari Erick David anaongeza

FEBRUARY 11, 1990 BAADA YA KUACHIWA KUTOKA GEREZANI MJINI CAPETOWN,BAADA YA AWALI KULETWA HAPO KUTOKA ROBBEN ISLAND ALIKOKAA JEMA MIAKA 18 KATI YA 27 ALIYOKAA GEREZANI.MOJA YA PICHA ZA MWANZO KABISA,SIKU HII ALILALA KWA MSHIKAJI WAKE BISHOP DESMOND TUTU, KWA SIKU 2 KISHA AKAENDA KWAKE SOWETO ORLANDO WEST MTAA WA VILAKAZI, AMBAO NDIO MTAA PEKEE DUNIANI HADI SASA WALIKOISHI WASHINDI WAWILI WA NISHANI YA NOBEL,NAO NELSON MANDELA NA DESMOND TUTU.


Share this article :
 
Shukrani kwa : Harold Dickson | Prosper Kwigize | 0752490120
Copyright © 2013. KWIGIZE NEWS AND COMMUNICATION - Haki zote zimeifadhiwa
Email us: kwigizenews@gmail.com
0764243377