Home » » BREAKING NEWS - NDEGE YA PRECESION AIR YAPATA AJALI ARUSHA

BREAKING NEWS - NDEGE YA PRECESION AIR YAPATA AJALI ARUSHA

Written By Unknown on Ijumaa, 13 Desemba 2013 | 04:19


Ndege ya shirika la ndege la Precision AIR imepata ajali wakati ikitokea jijini dar es Salaam kwenda Arusha mchana wa leo

Tukio hilo limetokea wakati ikitua katika uwanja wa ndege wa Arusha ambapo manairi yake yote yalipasuka

hadi sasa chanzo cha Ajali hiyo hakijajulikana ingawa baadhi ya abiria waliokuwemo wameelezea kilichoisibu ndge hiyo kuwa ni uchakavu wa matairi


"Nikiwa mmoja wa abiria tuliosafiri na PW kurudi Arusha leo, ndege ya shirika hilo yenye usajili No 5HPWI imepata kizaazaa wakati wa kutua baada ya tairi mojawapo kupasuka kwa kishindo, likufuatiwa na mengine yote ya nyuma ambapo yalipasuka pia na kuacha vipandevipande kwenye njia ya kurukia.

Waliookota vipande hivyo wamesema kuwa wamekuta viraka(pechi, watu wa magari wananielewa zaidi hapa), kitu ambacho si kawaida kwenye usafiri wa jamii hii!

Rubani wa ndege hiyo amejitahidi kuitoa ndege hiyo nje ya njia ili kutozuia ndege nyingine kuruka, japokuwa mwishowe ilimgomea kabisa na kubaki ikisota pembeni mwa njia hiyo.

Kikubwa ni kwamba hakuna madhara yaliyowapata abiria, akiwemo Bwana Lowassa." Ameeleza mmoja wa wahanga wa ajali hiyo na hakuwa tayari kutajwa jina lake


Hata hivyo, viongozi wa kampuni hiyo pamoja na uongozi wa uwanja huo hawajatoa taarifa za ajali hiyo sambamba na sababu zake
Share this article :
 
Shukrani kwa : Harold Dickson | Prosper Kwigize | 0752490120
Copyright © 2013. KWIGIZE NEWS AND COMMUNICATION - Haki zote zimeifadhiwa
Email us: kwigizenews@gmail.com
0764243377