Home » » WAGOMBEA URAIS 2015 WAHAHA KUHUSU KATIBA MPYA, WAHOFIA KUCHELEWA

WAGOMBEA URAIS 2015 WAHAHA KUHUSU KATIBA MPYA, WAHOFIA KUCHELEWA

Written By Unknown on Jumatatu, 16 Desemba 2013 | 11:10

Ibrahim Lipumba Mwenyekiti wa Chama cha wananchi CUF, amekuwa akigombea Urais tangu mfumo wa vyama vingi uanze nchini Tanzania

Mchakato wa katiba mpya licha ya kuwa jambo muhimu kwa watanzania na mstakabali wa taifa, mwenendo wa wanasiasa kulalama, kuchangia, kuhimiza wananchi kuunga mkono na wakati mwingine kupinga kumekuwa kukionesha kuwa ipo haja ya kuharakisha kupatikana kwa katiba hiyo

Haraka na mihemko ya wanasiasa hususani wale ambao wamekuwa wakigombea Urais, wenye nia ya kugombea pamoja na viongozi wa vyama vya siasa, kunadhihirisha kuwa harakahraka ya kupatikana kwa katiba mpya kunalenga uchaguzi ujao na si kupata katiba makini ya Tanzania
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba amesema mchakato wa Katiba Mpya una vikwazo vingi na kwamba Katiba haiwezi kupatikana mwaka 2014 kama Rais Kikwete alivyoahidi hivyo, kuna haja ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Bara.
Hii ni mara ya pili kwa Lipumba kutoa kauli hiyo. Mei mwaka huu, alitoa tamko kama hilo alipoonyesha wasiwasi wake kuhusu upatikanaji wa Katiba Mpya akadai ni janja ya CCM kumwongezea muda Rais.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Lipumba alisema kuwa amekuwa akiutafakari kwa kina mchakato wa Katiba Mpya kama unaweza kukamilika mwaka 2014, lakini jibu linalomjia, hakuna.
Alitaja baadhi ya vikwazo ambavyo vinaweza kukwamisha kupatikana kwa Katiba Mpya kuwa ni Daftari la Kudumu la Wapigakura kama halijaboreshwa na kasi ndogo ya utoaji wa vitambulisho vya utaifa ambavyo vitatumika kupigia kura hiyo.
Wakati Profesa Lipumba akisema hayo, tayari Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), imeeleza kuwa haina mpango kwa sasa wa kuboresha Daftari la Kudumu Wapigakura kwa ajili ya kura za maoni kwa sababu muda uliobaki ni mfupi.
Mwenyekiti wa Nec, Jaji Mstaafu Damian Lubuva alisema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita, kuwa itakuwa vigumu kuliboresha daftari hilo kwa ajili ya upigaji wa kura za maoni utakaofanyika mwanzoni mwa mwaka 2014 kwa sababu muda uliobaki ni mfupi na hakuna fedha za kufanya hivyo.
Share this article :
 
Shukrani kwa : Harold Dickson | Prosper Kwigize | 0752490120
Copyright © 2013. KWIGIZE NEWS AND COMMUNICATION - Haki zote zimeifadhiwa
Email us: kwigizenews@gmail.com
0764243377