Rais Silva Kiir wa Sudan Kusini |
Rais wa
Sudan Kusini Salva Kiir, anasema vikosi vyake vimefanikiwa kutibua jaribio la
mapinduzi, baada ya usiku mzima wa mapigano katika mji mkuu wa nchi hiyo Juba.
Bw. Kiir,
anayetoka katika kabila kubwa zaidi la wa Dinka amewatupia lawama wanajeshi
wanaomtii aliyekuwa makamu wake Riek Machar, anayetoka katika kabila dogo la
Nuer.
Riek Machar aliyewahi kuwa makamu wa Rais wa Sudan Kusini ndiye anayetuhumiwa kuusika na jaribio la mapinduzi |
Aidha Kiir
ametangaza amri ya kutotembea usiku mjini Juba na kusema serikali sasa inaudhibiti
mji huo.
Makundi hasimu
ya wanajeshi walipigana vikali kwa saa kadhaa na kuna ripoti za kuwepo majeruhi
maelfu wakiripotiwa kukimbilia usalama wao.
Milio ya
risasi sasa inaripotiwa kupungua. Kumekuwa na hali tete ya kisiasa nchini Sudan
Kusini tangu mwezi Julai wakati Rais Kiir alipovunja na kuwafuta kazi mawaziri
wote katika baraza lake akiwemo Makamu wa Rais Bw.Machar.