Kulia katika picha ni Rhys Torrington: Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Ltd |
Habari zimeandikwa na Khadija Mahamba na Lucy Ngongoseke
Dar es Salaam
Huduma
za matangazo ya AzamTV zilianza kupatikana hewani Kuanzia Ijumaa Desemba 6,
2013 kwa kuwawezesha wateja waliounganishwa kwenya kisimbuzi kungalia bure hadi
hii leo ambapo huduma kwa malipo inaanza rasmi kwa ada ya shilingi 12,500 kwa
mwezi.
Kwa
kuanzia huduma ya AzamTV itahusisha chaneli 50 zinazojumuisha chaneli maarufu
za kimataifa, chaneli maarufu za ndani na chaneli tatu maalumu za Azam ambazo
ni:
· Azam
One – burudani kwa familia kutoka Afrika, sehemu kubwa ya matangazo itakuwa kwa lugha ya Kiswahili.
· Azam
Two – vipindi maalum kutoka sehemu mbalimbali za dunia
· SinemaZetu
– Chaneli maalumu kwa tamthilia za kitanzania kwa saa 24.
Kwa pamoja, chaneli
tajwa zitawapa wateja wigo mpana wa kufaidi matangazo bora ya michezo,
tamthilia, watoto na maisha.
Kundi la T-Afica
likituwa burudani wakati wa ufunguzi wa ofisi ya AZAMTV siku ya jumatatu tarehe
16 Desemba 2013
|
Ofisi ilifunguliwa
rasmi na Bw. Yusuf Bakhresa: Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Ltd.
“Ofisi hii ya makao
makuu ambayo kwa hakika ni ya kuvutia ni kielelezo cha nia thabiti ya Azam
Media kufanya kazi kwa umakini katika shughuli ya utangazaji hapa Tanzania.
Dira yetu ni kutoa burudani ya kiwango cha juu kwa familia kwa bei nafuu kote
nchini, na baadaye kote barani Afrika. Hili ni jambo ambalo kila mmoja hapa
nchini anapaswa kujivunia.” Alisema Bakhresa
Rhys Torrington: Afisa
Mtendaji Mkuu wa Azam Media Ltd alisema: “Naona faraja kubwa kwamba leo hii
AzamTV ipo sokoni kwa ajili ya kila mtanzania. Tutahabarisha, kuelimisha
na zaidi ya yote tutaburudusha watu kote nchini. Huduma yetu inapatikana kwa
watu wote – situ katika ofisi hizi lakini pia kupitia mtandao wetu unaohusisha
zaidi ya mawakala 50 katika kila mkoa. AzamTV ni ya kudumu”
Azam Media pia inawekeza
katika utayarishaji wa vipindi vipya kupitia kampuni yake tanzu, Uhai
Productions, kwa kushirikiana na watayarishaji wa vipindi wa hapa Tanzania.
Azam Media Ltd. Ni
kampuni tanzu ya kundi la makampuni ya Salim Said Bakhressa (SSB).
Azam TV, ni warushaji
wa matangazo ya satelaiti kwa mfumo wa digiti ambayo itawapatia wateja wake
burudani ya kiwango cha juu kwa familia kwa bei moja nafuu. Makao Makuu yapo
Dar es Salaam, Tanzania amabako ilianzishwa mwaka 2013 malengo yakiwa kusambaa
katika nchi nyingine za Afrika hapo baadaye.
Dira ni kuwa na
vipindi tofauti vya kimataifa na pia vya ndani ya nchi vifaavyo kwa
familia, wapenzi wa michezo na watanzania wote wa rika mbalimbali.
Watazamaji wanaweza
pia kurekodi wakati wa kuangalia kwa kutumia USB. Ni utaratibu wa kawaida
kwamba kisimbuzi kinakuja na na sehemu ya kuunganisha kwa mfumo wa HDMI
ili kupokea picha ang’avu kwenye luninga.