Home » » KAMATI KUU YA CCM YAANZA KUWAHOJI MAWAZIRI

KAMATI KUU YA CCM YAANZA KUWAHOJI MAWAZIRI

Written By Unknown on Ijumaa, 13 Desemba 2013 | 22:23

Mwenyekiti wa Chama chaMapinduzi CCM Dr. Jakaya Kikwete (kushoto) akiwa na Katibu mkuu wa CCM Abdulahiman Kinana

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete, imeanza kuwahoji mawaziri waliotajwa ni ‘mzigo’ kwa Serikali.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, jana alilithibitishia gazeti dada la Mwananchi, The Citizen juu ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu (CC), lakini hakuwa tayari kuingia kwa undani kuhusu ajenda.
Nape Nnauye Katibu wa itikadi na Uenezi CCM

Hata hivyo, habari za ndani zilieleza kwamba miongoni mwa ajenda kuu za CC ni kuwahoji mawaziri wanaolalamikiwa na wananchi, kwamba wameshindwa kutekeleza majukumu yao.
Wakiwa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, Nape aliwatupia lawama mawaziri wakati akielezea changamoto zinazowakabili wakulima ambao ni asilimia 80 ya Watanzania, huku mawaziri husika wakikaa kimya.
Mawaziri waliotajwa mzigo ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa; Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza na Naibu wake, Adam Malima, kwamba wameshindwa kazi na alipendekeza wang’olewe.
Hata hivyo, gazeti hili jana lilishuhudia mawaziri kadhaa wakifika na kuingia kwenye mkutano wa CC, taarifa zingine zilisema mawaziri waliofika kwenye kikao hicho walihojiwa na wajumbe wa CC.
CHANZO. Mwananchi
Share this article :
 
Shukrani kwa : Harold Dickson | Prosper Kwigize | 0752490120
Copyright © 2013. KWIGIZE NEWS AND COMMUNICATION - Haki zote zimeifadhiwa
Email us: kwigizenews@gmail.com
0764243377