Tata Madiba (Rais wa kwanza mzaleendo wa Africa Kusini) |
Siku kumi tangu alipofariki dunia, hatimaye Rais wa kwanza wa
afrika kusini Nelson Mandela amezikwa leo katika makaburi ya fanilia katika
kijiji cha Qunu nchini humu huku akiacha hofu kwa wageni wanaoishi nchini humo
Mandela anayeitwa na raia wan chi hiyo kwa jina la TATA
Madiba amezika mapema leoo majira ya mchana na viongozi mbalimbali wan chi za
kiafrika, Mashariki, Ulaya na Amerika wamehudhuria mazishi hayo
Wageni maarufu kama walowezi wanahofu kuwa huenda kuondoka kwa mandela kukaibua hoja za kuwataka wageni wanaoishi nchini humo kuanza kunyanyaswa, kitendo ambacho mandela hakuwa akikubaliana nacho
Hata hivyo waombolezaji kutoka mataifa mbalimbali ambao
walikuwa wakifuatilia runinga ili kushiriki mazishi kwa njia ya picha
hawakuweza kuliona jeneza kutokana na kamera kutoonesha kinachoendelea ndani ya
kaburi
Sambamba na mazishi hayo mizinga 21 imepigwa angani kama
ishara ya heshima kwa Baba wa taifa hilo ambaye alisota jela miaka 27 kufuatia
harakati zake za kupinga ubaguzi wa rangi uliokuwaukisimamiwa na serikali ya
makabulu
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete amekuwa kivutio katika
mazishi hayo pale alipopigiwa makofi mara kadhaa wakati akihhutubia
waombolezaji na kutaja kuwa Mandela na raia wa afrika kusini ni ndugu na kwamba
Tanzania ilishiriki kwa asilimia mia moja kutetea waafrika na kuleta Uhuru wa
nchi hiyo
Katika kupigania uhuru wa nchi mbalimbali za Africa Tanzania
ilitoa ardhi na mafunzo ya kisiasa na kijeshi kwa wapigania uhuru wan chi mbalimbali
akiwemo Nelson Mandela, Joachim Chisano, Samora Machel na wengine wengi kutoka
nchi za Malawi, Zimbabwe, Namibia