Hayati Patrice Lumumba |
Chama cha MNC Lumbumba kilichopigania
uhuru wa DRC iliyokuwa ikijulikana kama Zaire chini ya Hayati Patrice Lumumba, kimeituhumu
nchi ya Rwanda na Uganda kwa kujaribu kuimega nchi ya jamhuri ya kidemokrasia
ya Kongo na kuunga mkono vikundi vya uasi vya M23
Katibu mkuu wa chama hicho Bw. Venance
Wialango amebainisha hayo katika mahojiano na Channel Africa jijini Dar es
salaam na kubainisha kuwa tangu kuuwawa kwa Patrice Lumumba DRC imekuwa
ikivamiwa na Rwanda kwa kusapoti wapambanaji wanaojiita wapigania uhuru
Amesisitiza kuwa vikosi vya uasi
vinavyojikita mashariki mwa DRC hususani mikoa ya KIVU ni vinavyoundwa na
wanyarwanda na kupewa msaada na serikali ya Rwanda na Uganda
Amesisitiza kuwa waasi hao hawana nia
na amani ya DRC zaidi ya kutumia uasi huo kuvuna mali hususani madini
yaliyosheheni katika eneo la Kivu Kusini na Kaskazini kwa kisingizio cha kutaka
kuingizwa katika serikali ya Joseph Kabila
Akizungumzia kuhuru kikundi cha M23
na mahusiano yake na Rwanda Bw. Wialango amesema ni masalia ya vikosi vya
Rwanda vilivyomsaidia Hayati rais Laurent Kabila ambao hawakuingizwa katika
jeshi la serikali
“Katika harakati za kumwondoa Rais
Mobutu Madarakani, Laurent Kabila alitumia wapambanaji wa aina nyingi miongoni
mwao walikuwa ni hao Wanyarwanda walioko katika misitu ya Kongo na makubaliano
yalikuwa ni baada ya kuchukua nchi wao wangerejea makwao, sasa hali ikawa
kinyume, wakasisitiza kuingizwa katika Jeshi la taifa, alipokataa killichotokea
ni kuuwawa” anasema Wialango
Aidha Katibu huyo mkuu wa chama cha
MRC Lumumba Bw. Venance ameipongeza Tanzania kwa kuongoza jeshi la umoja wa
mataifa chini ya vikosi vya SADC kuwaondoa wapiganaji wa M23 mashariki mwa
kongo na kusisitiza kuwa ipo hata ya mataifa kuamini kuwa Rwanda ndiyo
inayowapa nguvu wapiganaji hao
Hata hivyo ameelezea kusikitishwa na
kitendo cha Rais Kabila kuingia mkataba na M23 ambao wameshindwa katika vita,
na kwamba kitendo hicho kinachochea hisia kuwa Kabila naye ni mfadhili wa uasi
huo mashariki mwa DRC