Siku chache baada ya Rais wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo
Joseph Kabila kusaini mkataba wa amani na kikundi cha waasi cha M23 katika
hafla iliyohudhuriwa na marais Yoweli Museveni wa Uganda na Joyce Banda wa
Malawi jijini Nairobi, Raia wa kongo walioko Tanzania pamoja na viongozi wa
vyama vya upinzani nchini DRC wamepinga mkataba huo
Wakiongea na channel africa kwa nyakati tofauti raia hao
wametaja kuwa M23 hawakupaswa kuingia mkataba wa aina yoyote na DRC kwa kuwa ni
kikundi kilichoshindwa katika vita na kwamba tangu awali hawakuhitaja suluhu
Venance Wialango Katibu Mkuu MNC Lumumba |
Venance Wialango ni katibu mkuu wa chama cha MNC/Limumba
anayeishi uhamishoni nchini Tanzania hapa anasisitiza kuwa M23 wameshinda vita
na hawakuwa tayari kuingia mkataba wowote na serikali ya Joseph kabila kabla ya
kupigwa kijeshi na majeshi ya SADC chini ya dhamana ya umoja wa mataifa
Kwa upande wao wakimbizi kutoka DRC walioko Tanzania nao
wamekuwa na maoni hasi juu ya mkataba huo huku wakiwatuhumu kuwa M23 ni raia wa
Rwanda na Uganda wanaojaribu kuikalia nchi yao
Kutokana na mkataba huo, wakimbizi wamesisitiza kuwa
hawatarejea nchiini mwao kama Rais Kabila ataendelea kuwaruusu wanyarwanda
kuingia katika jeshi la taifa pamoja nakuacha wageni kuyakalia maeneo na ardhi
ya DRC
Mkataba wa amani baina ya serikali ya DRC na waasi wa M23
ulisainiwa jijini Nairobi baada ya ule wa awali uliokuwa usainiwe jijini
Kampala kukwama