Kiongozi wa chama cha upinzani cha Ukombozi wa Wanyarwanda ULDR nchini
Rwanda Bw. Hakiza Pauline ameitupia lawama mahakama ya kimataifa
inayoshughuikia mauaji ya kimbali ya Rwanda ICTR iliyoko mkoani Arusha
kwa kuendesha shughuli zake kwa mlengo wa ukabila
Akiongea na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar salaam ambapo
yupo kwa ajili ya kusaka uungwaji mkono, Hakiza ambaye anishi
uhamishoni nchini Afrika kusini, amesema ICTR imekuwa ikiwaandama
wahutu pekee kwa tuhuma za mauaji ya watusi na kuongeza kuwa, vita vya Rwanda vya mwaka 1994 vilihusisha makabila yote
Pamoja na madai hayo ya Hakiza wa chama cha ULDR, kwa upande wake
mahakama ya ICTR imekanusha vikali madai hayo na kusisitiza kuwa
hakuna upendeleo wa kikabila katika usikilizaji wa kesi
Mkuu wa kitengo cha habari cha mahakama hiyo Bw. Danford Mpumilwa
ameiambia channel Africa kuwa hizo ni hisia za kibinadamu, katika line
ya simu Danford mpumilwa tuambie kuna ukweli wa madai hayo ya ubaguz
na ukabila mahakamani hapo
Bw. Mpumilwa amekanusha madai hayo na kusisitiza kuwa mahakama hiyo inazingatia sheria za kimataifa za makosa ya jinai na hakuna vitendo vya ubaguzi katika mahakama hiyo.