Vyama vyote 21 vyenye
uwakilishi na visivyokuwa na uwakilishi bungeni nchini, kikiwamo Chama Cha
Mapinduzi (CCM), vimeanza kujipanga kuwa na maridhiano ya kitaifa ili
kuhakikisha vinakuwa na msimamo mmoja katika kujadili rasimu ya katiba mpya,
kabla ya Bunge Maalumu la Katiba kuanza.
Hatua hiyo imeanza kuchukuliwa chini ya uratibu wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), kwa kuzingatia moja ya mambo mawili, ambayo Rais Dk. Jakaya Kikwete na viongozi wakuu wa vyama sita vyenye uwakilishi bungeni, walikubaliana walipokutana Ikulu, jijini Dar es Salaam, Oktoba 15, mwaka jana.
Jambo la kwanza, ambalo pande mbili hizo zilikubaliana, ni vyama vyote vya siasa vyenye mawazo, maoni na mapendekezo ya kuboresha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2013, kuyawasilisha haraka serikalini ili kutafuta namna ya kuyashirikisha katika marekebisho ya sheria hiyo.
La pili, vyama vya siasa nchini, kama wadau muhimu katika mchakato wa Katiba Mpya, viangalie namna ya kukutana na kujenga mfumo wa mawasiliano na maridhiano wa jinsi kwa pamoja vitakavyosukuma mbele mchakato mabadiliko ya katiba ya nchi kwa maslahi mapana ya nchi na mustakabali wa taifa.
Viongozi, ambao Rais Kikwete alikutana nao Ikulu kwa mazungumzo hayo wanatoka vyama vya CCM, Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi, TLP na UDP.
Katika makubaliano hayo, TCD ilipewa jukumu la kuratibu jambo hilo, ikiwa ni pamoja na kuandaa mkutano wa vyama hivyo na wadau wengine nchini.
Katika kuanza kujipanga kuhusu suala hilo, TCD ilikutana na viongozi wakuu wa vyama hivyo jijini Dar es Salaam ili kujadili suala hilo.
Baada ya mkutano huo, Mbatia alivitaka vyama hivyo kuanza mara moja kuichambua rasimu hiyo na kuwasilisha misimamo ya kila chama kwenye kamati ya ufundi ya TCD.
Katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam chini ya uenyekiti wa Msemaji Mkuu wa TCD, James Mbatia, vyama visivyo na uwakilishi bungeni, viliwakilishwa na Mwenyekiti wa UPDP, Fahmi Dovutwa.
Mbatia alisema mwisho kwa vyama hivyo kutoa na kuwasilisha misimamo yao kwa kamati hiyo kuhusu rasimu ya katiba mpya ni Januari 31, mwaka huu.
Alisema baada ya vyama kuwasilisha misimamo yao, kamati hiyo itatengeneza ‘bango kitita’, ambalo litaiweka (misimamo hiyo) pamoja ili kuona msimamo wa kila chama kuhusu rasimu hiyo.
Alisema baadaye, kati ya Februari 8 na 14, utaitishwa mkutano wa maridhiano ili kupata msimamo wa vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu kuhusu rasimu hiyo kabla ya kuingia kwenye Bunge hilo.
Mbatia alisema jambo la pili, ambalo liliifanya TCD ikutane na viongozi wakuu wa vyama hivyo jana, ni kuelezana kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura.
Alisema wanataka uboreshaji wa daftari hilo ufanyike kabla ya hatua ya kupiga kura ya maoni kuamua ama kuikubali rasimu hiyo au kuikataa.
Hivyo, alitumia fursa hiyo kuitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuanza mara moja mchakato wa uboreshaji wa daftari hilo na kuisisitiza serikali kusaidia suala hilo ili kuhakikisha linafanyika.
Kwa upande wake, Dovutwa alisema vyama vya siasa ndiyo wadau wakubwa katika mchakato wa upatikanaji wa katiba, hivyo ushiriki wao utasaidia kupatikana haraka katiba mpya Tanzania.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, alisema kuna faida kubwa sana viongozi wa vyama vya siasa kukutana na kujadili mambo makubwa ya kitaifa kwa sababu inaondoa hofu katika siasa.
Pia alisema jambo hilo linasaidia kujadili na kuondoa tofauti mbalimbali zinazojitokeza katika siasa na katika Bunge.
Hata hivyo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alikataa kuzungumza lolote alipotakiwa na waandishi wa habari kutoa maoni yake akisema kwa jana asingeweza kuzungumza chochote kwa kuwa kikubwa kilichochajadiliwa kilikuwa katika mkutano wao.
Katika mkutano huo, CCM iliwakilishwa na Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara, Philip Mangula na Kinana.
Wengine walioiwakilisha Chadema ni Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, Mwanasheria Mkuu, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo, John Mnyika.
CUFMwenyekiti, Profesa Ibrahim Lipumba na Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara, Julius Mtatiro.
NCCR-Mageuzi Kaimu Katibu Mkuu, Mosena Nyambabe, wakati UDP na Isack Cheyo.
Ilielezwa kuwa viongozi wakuu wa vyama hivyo walikutana Ikulu mwaka jana na Rais Kikwete katika mazingira ya maelewano na mwafaka.

CHANZO: NIPASHE