Kwa. Hisani ya BBC
Daktari mmoja katika
mkoa wa Kaskazini wa Shanxi nchini Uchina amehukumiwa kifo baada ya kupatikana
na hatia ya kuwaiba watoto saba kutoka hospitali aliyokuwa akihudumu na kuwauza
watoto hao kwa wauzaji watoto.
Hukumu hiyo ya kifo
hubadilika na kuwa kifungo cha maisha baada ya miaka miwili ya mshitakiwa
kubadili tabia
Wakati mmoja daktari
Zhang Shuxia alikuwa mtaalam mashuhuri lakini sasa ni nuhalifu mwenye hatia
aliyejipatia faida kubwa kutokanana na uuzaji wa watoto.
Daktari huyo
aliwadanganya wazazi wapya kwamba watoto wao walizaliwa wakiwa na ugonjwa
mbaya.Aliwahadaa kwamba iwapo wazazi wangeliwachia serikali jukumu la
kuwaangalia basi wangepewa matibabu ya hali ya juu waliohitaji.
Watoto hao wenye afya
njema baadaye waliuzwa kwa bei ya maelfu ya madola kwa wauzaji watoto
wanaohudumu katika mikoa ilio karibu.
Sita kati ya watoto
walioibwa walipatikana na kurudishwa kwa wazazi wao huku mtoto mmoja aliyeuzwa
kwa dola 165 pekee akipatikana ameaga dunia kandokando ya barabara ambapo
alikuwa amewachwa na muuzaji mmoja wa watoto.