Mnofu wa Nyama ya Ng'ombe |
Na
Elisante John, Singida
Januari
24, 2014.
TAASISI
ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) imemfikisha mahakamani ofisa mifugo
wa kata Mitunduruni iliyopo katika Manispaa ya Singida Edwin Mtae kwa kosa la
kuomba na kupokea rushwa ya nyama laini kilo 12 za maini, figo na moyo wa
ng’ombe.
Mwendesha
mashitaka mwanasheria wa TAKUKURU Dominic Maganga ameieleza mahakama hiyo chini
ya hakimu mkazi Wilaya Singida Joyce Minde kuwa mshitakiwa alifanya kosa hilo
Septemba 28 mwaka jana, majira ya asubuhi kwenye machinjio ya Mitunduruni,
mjini Singida.
Maganga
amesema kitendo hicho ni kosa na kinyume cha sheria kutokana na kifungu cha 15,
cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2007.
Amesema
mshitakiwa alikuwa anafanya hivyo, vinginevyo mfanyabiashara husika huelezwa
kuwa nyama ya mfugo wake ina dosari na hivyo huamriwa kuiteketeza ili isilete
athari kwa mlaji
Maganga
amesema baada ya taarifa kufika ofisini, TAKUKURU na baadhi ya wafanyabiashara
waliweka mtego uliomnasa mshitakiwa akipokea kilo 12.5 za nyama laini, ikiwa ni
za sehemu ya maini, moyo na figo ya ng’ombe.
Hata
hivyo mshitakiwa amekana shitaka hilo na yupo nje kwa dhamana ya wadhamini
wawili, kwa sharti la kila mmoja kuwa na Sh.500,000 na kesi hiyo itasikilizwa
tena februari 06, 2014
MWISHO.