Ya Mungu mengi, wakati waafrika tukiamini kuwa wazungu wanampenda na kumthamini Mungu, na wakati wakristo waafrika wakithamini uwepo wa wazungu katika makanisa yao, Huku ulaya makanisa sasa yamefungwa na kugeuzwa kuwa nyumba za kuishi watu ...(nyumba za kupanga)
Baadhi ya Parokia na Parish sasa ni vituo vya kulelea watoto pamoja na maeneo ya biashara.
Leo nimetembelea katika Mji mmoja unaoitwa Bussum katikati ya nchi ya Holland nimeshangaa, kanisani nimekuta wazee na vikongwe tu tena hata robo ya kanisa hawajalijaza.
Udaku wangu haukuishia hapo nikaona ipo haja ya kujua kulikoni, ndipo nikaambiwa kuwa vijana na watu wenye umri wa kati aahhh makwao wakipumzika na kujiandaa na suluba za wili kuanzia kesho, jioni viwanja kula raha.......
Du ulikotoka umissionary ndiko kifo cha kanisa kinakoanzia. Jengo hilo la kanisa pichani sasa ni makazi ya watu si la ibada tena, nani aingie humo kusali?
Du kweli ulistaajabu ya musa utaona ya filauni, Kanisa zuri kama hili lingehamia Kasulu hata watoro wangerudi kupata neon
Yote haya nayashuhudiwa wakati Afrika tukihangaika kujenga makanisha baada ya yale ya awali kukosa nafasi, waumini tunaongezeka.
Mwenyezi Mungu aendelee kuleta neema na Baraka kwa waumini wake ili hatimaye amani na upendo, furaha na matumaini viendelee kuwepo miongoni mwa wannadamu
Mungu Ibariki nchi yetu Tanzania ambako bado tunakuthamini na kukuheshimu.
makala hii pia itakuijia kwa lugha ya kiingereza,