JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
OFISI YA MBUNGE, JIMBO LA NZEGA
Mhe.
Dkt. Hamisi A. Kigwangalla (MB),
Mwenyekiti,
Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
KUMB. NA. MP/PR/001/2014
Tarehe: Feb 14, 2014
TAMKO LANGU KWA UMMA KUHUSU MCHAKATO WA KUANDIKA KATIBA MPYA
YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Ndugu wanahabari na waTanzania wenzangu,
Nimekuwa nikilazimika kujibu maswali mbalimbali kutoka kwa
wanahabari, ndugu, jamaa na marafiki kuhusiana na namna mchakato wa kuandika
katiba mpya ya Taifa letu unavyoenda; wengi wakipenda kujua nini mtazamo wangu
kuhusu mambo mengi, haswa hili la serikali mbili
ama tatu kwenye muungano wetu. Mara nyingi nimekuwa nikikwepa kusema msimamo
wangu ni nini kwa sababu niliona ni vema nikajipa muda wa kutafakari kabla ya
kuamua kujenga msimamo yangu. Ila kwa kuwa wakati wa kwenda Bungeni umefika na
mimi nimepata bahati ya kuwa miongoni mwa wajumbe wa Bunge hili la kihistoria
nimeona leo nitoe mtazamo wangu.
Kwanza, nianze kwa kuonesha wasiwasi wangu kama tutaweza
kufika salama huko tuendako. Si kwa sababu za kitabiri kama mnajimu, la, ni kwa
sababu za kisayansi, ambazo nitaziweka wazi hapa kama ifuatavyo:
(i.)
Pamoja na kwamba tume imefanya kazi
nzuri ya kukusanya maoni na kuyaweka katika nyaraka ambayo tutapaswa kuifanyia
kazi, napata shida kama walikuwa makini katika kuendesha zoezi hili. Kivipi,
binafsi napata shida na methodology iliyowawezesha kufikia ‘conclusion’
madhubuti kwamba watanzania asilimia 61 walitaka serikali tatu. Kwa sababu za
kisayansi naona tume ya Mhe. Jaji Warioba imepotoka na kwamba kusema hivyo ni
kutaka kulazimisha uhalali wa hoja hii nyeti kwenye dokumenti ya Rasimu ya
Katiba tunayopaswa kuipitisha bila kuwa na msingi wa kitakwimu unaotokana na
njia (methodology) za kisayansi za kukusanya ‘data’ na kutafuta ‘validity’ na
‘generalizability’ ya taarifa husika. Nilidhani hili milikuwa na muda wa kutosha kama chama na kama
wabunge kulitizama. Inasikitisha sana kusikia kuwa leo ndio linaonekana.
(ii.)
Kwa jinsi mchakato ulivyo ni ngumu
kusema kuwa leo tutaweza kubadili jambo nyeti kama la ‘Muundo wa Muungano’ kuwa
uwe ni wa Serikali mbili, ama moja, wakati mapendekezo ya Tume, ambayo ‘yanaelezewa’
na Tume kuwa yanatokana na ‘maoni’ ya wananchi walio wengi, 61% na pili
mabaraza ya katiba [cf. Muundo katika mchakato huu ni wa pyramid, kwamba
unaanza na maoni ya wengi huku chini kwenye kitako, baadaye mabaraza ya katiba
hapo katikati na mwisho Bunge la Katiba, kabla ya kura ya maoni]. Hivi
inawezekana wapi Bunge Maalum la Katiba, kwa hapa tulipofikia, likafanya
mabadiliko kwenye mambo yanayohusu ‘muundo’ (structure) wa Katiba? Yaani,
kwamba inawezekana vipi wajumbe hawa 640 wabadilishe jambo zito la kimuundo
kama hili? Kimantiki haingii akilini. Uhalali huo unatoka wapi? Lakini pia hapa
hatuwezi kuondoa ukweli kwamba malalamiko na manung’uniko ya baadhi ya watu
yana mashiko, kuwa hivi kama hoja ya Chama Cha Mapinduzi ilikuwa ni kuilinda
‘status quo’ ya muungano wa serikali mbili na kama walifanya kazi ya
kuwaelimisha wanaCCM nchini, na wanaCCM walikuwa wengi zaidi kwenye mabaraza ya
katiba ya wilaya [walishinda kwa zaidi ya asilimia 65, inatokeaje asilimia 61
watake muungano wa serikali 3?]. Maana yake ni kuwa
hata wanachama wa ccm ngazi ya wilaya walichagua serikali tatu. Au inawezekana
kuwa walitumwa kutoe hiyo elimu /maelekezo hawakuwa na nguvu (mbinu na weledi)
ya ushawishi. Lakini pia ni somo kuwa sio sawa kuamini kuwa wanachama wa ccm
ngazi ya wilaya hawawezi kutafakari na kuchagua, eti wao ni wa kupewa elimu na
kufuata tu.
Nini tafsiri ya haya yote? Kwamba ukisema unabadili leo muundo wa
Muungano ukaleta wazo tofauti na lile linalotokana na mapendekezo ya tume, kama
yanavyosomeka kwenye Rasimu (sura ya 6), mfano ukasema, ziwe serikali mbili tu
badala ya tatu zinazopendekezwa, maana yake unaongelea kuanza upya kutengeneza
vifungu vipya vya ‘kimuundo’ vya serikali za mitaa, wawakilishi wa wananchi, mambo
ya wakuu wa mikoa ama majimbo(provinces) – jambo ambalo litakuwa cumbersome!
Vurugu mechi bila uwepo wa rasimu! Swali la kujiuliza hapa ni kwamba – hivi
tume hawakuliona hili? Pengine wangeweka chaguzi (option) pembeni, maana maoni
yote haya wanayo, ila kwa sababu ya muundo wa Muungano ‘waliouchagua’
hawakupenda kuelezea mambo binafsi ya serikali hizi ‘mbili’ za ‘iliyokuwa
Tanganyika’ na Zanzibar kwa madai kwamba jukumu lao ni kuandaa rasimu ya Katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kinachoonekana hapa ni kwamba
walikwishaamua kuwa ziwepo serikali tatu kwa madai kuwa ndiyo maoni ya wananchi
na kwa kuzingatia msingi wa hoja kwamba Bunge la Katiba haliwezi kuwa na
uhalali wa kubadili mambo ya msingi ya kimuundo wa katiba, kama hili la Muundo
wa Muungano, bali ‘kuboresha’ tu yale yaliyomo. Mtu makini atahoji kuwa ni kwa
nini wamekwepa kuzungumzia ukweli kwamba ‘Tanganyika’ hayupo? Na nini itakuwa
hatma ya Katiba yake? Na ni lini wabia hawa wa Muungano walikaa wakakubaliana
washirikiane kwenye mambo yapi kwenye huo muungano wa Shirikisho? Hili la tanzanyika kwa ujumla wake halikuwepo katika ToR na
pia unajenga hoja kwa kuhisi tu hasa unaposema alikuwa “wameshaamua”.
Sasa wabunge wa Bunge maalum la katiba tukiukataa huu muundo wa serikali
tatu nini kitatokea? Maana yake sehemu kubwa ya rasimu hii italazimika
kubadilishwa. Hakika ! Lakini kama ulivyosema wewe
mwenyewe watapata wapi hayo mamlaka?
Jambo lingine ambalo
litatusumbua ni kuwa, vipi kama wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba tukiamua
tujenge msimamo kwenye hoja ya Serikali Moja itakuwaje? Maswali mengi yataibuka
bila kupata majibu hapa, kuwa ni nani atakuwa ‘Mpatanishi’ kwa niaba ya Tanganyika
(ama Tanzania bara)? Maana Zanzibar yupo na ana uhai wake kamili, Tanganyika
yuko wapi hapa? Hakika ! Lakini kama ulivyosema wewe
mwenyewe watapata wapi hayo mamlaka? Na kama mkiamua hivyo mnatakiwa muwe na
majibu ya hayo maswali na pia hamtahitaji siku 70 huko!
(iii.)
Mhe. Jaji Joseph Warioba na wenzake
wanapaswa wajibu maswali haya:
1. Ni
njia (methodology) ipi ya kisayansi na kitakwimu walitumia kufikia ‘conclusion’
hiyo madhubuti kabisa kuwa 61% ya watanzania walitaka Muundo wa Serikali Tatu?
Watueleze watanzania sample size, sampling technique, sampling frame na namna
walivyowafikia na kuwahoji watu hao. Hili jibu lake
wanalo na hata wewe unajua watalijibu vizuri sana. Ingawa aliewapatia ToR
anatakiwa kujua zaidi, vilevile ninashangaa ilikuwaje mkakubali rasimu ya
kwanza bila kujua methodology nk ?
2. Watueleze
ni nani aliyewatuma kwenda kubadilisha Muundo wa Muungano? Hapa nadhan kaka
umesahau kuwa hawa jamaa walitumwa kukusanya maoni kuhusu Muungano, kimsingi
unawezaje kuzungumzia muungano bila kuzungumzia muundo, na kama ukiuzungumzia,
unawezaje kukwepa watu kuutolea maoni?
3. Ni
nani sasa atakuwa na mamlaka ya kuandika Katiba ya Serikali ya Tanganyika (ama
Tanzania Bara – ambaye aliishakufa?), kama tukiamua kwenye Bunge la Katiba
kupitisha Rasimu hii yenye Muundo wa Muungano wa Serikali tatu? Tunaanzia wapi
kumfufua Tanganyika?
Hili ni swali zuri
sana kaka, ila ninashangaa kwa nini wizara na mkuuw a nchi hajajibu mpaka sasa.
Hili ni swali ambalo ninyi wabunge mlitakiwa kuliona kabla na kuhoji, ila kwa
sababu mnazozijua ninyi hamkuhoji na leo unatoa tamko tu badala ya kuhoji
wahusika…Kimsingi ukiwa mwenyekiti wa kamati ya TAMISEMI na ukijua kuwa ninyi
ndio mhimili wa serikali na katiba ya Tanganyika na mpaka leo mnaona sawa tu
kuendelea na mchakato bila majibu ya “iko wapi serikali ya mitaa na
vijiji?”
Maoni
yangu: Mtu yeyote mpenda demokrasia ataona wazi kwamba kuna utata
uliogubikwa na ukungu wa presha za kisiasa za kuona zoezi hili linakamilika.
Utata wa uhalali wa Bunge la Katiba kubadili hoja za msingi kwenye rasimu ni
jambo zito, na mashaka kwamba pengine Jaji Joseph
Warioba na wenzake walikuwa na ajenda yao ya siku nyingi ya kuleta serikali
tatu kinyume na matakwa ya Chama Tawala, CCM, ni jambo zito zaidi.
Hivyo, kuondoa mamlaka na madaraka ya wananchi (kama kweli yapo kama inavyosema
tume) kwenye jambo zito la kimsingi kama Muundo wa Muungano ni jambo
linalotishia usalama wa mchakato na ni jambo lisilokubalika kwa kuwa linaondoa
haki, wajibu, mamlaka na madaraka ya wananchi kufanya maamuzi kuhusu katiba yao
(an act of popular sovereignity). Mkanganyiko huu unatia mashaka zaidi ya kuleta
mwangaza wa mabadiliko ya kutokea kwa maridhiano. Jaji
Warioba na wenzake walilijua hili na wameleta ‘chaos na frustration’ kwa
maksudi kwa kujificha chini ya kivuli cha ‘uhalali’ wa Bunge la katiba HAO WENZAKE NI KINA NANI AMBAO HATA WAKO TAYARI KUWA KINYUME
NA CCM ? HII INATISHA KIDOGO (yaani ‘legitimacy of rule or of law is
based on the consent of the governed’) na nadharia pana ya demokrasia yenye
msingi kwenye kanuni za ‘popular sovereignity’ wakijua kabisa wabunge
tutashindana, tutatofautiana!
Mimi nina maoni kwamba, ili mchakato uishe
salama, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete aingilie
kati, atumie mamlaka yake kusitisha mchakato huu mpaka itakapoundwa tume
nyingine ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu suala la Muundo wa Muungano na
kisha ipigwe kura maalum ya maoni kuhusiana na jambo hili ili watanzania
washiriki kikamilifu na waamue na siyo kufanya maamuzi ya kubadilisha Muundo wa
Muungano bila kutupa fursa ya kujadiliana na kushiriki kufanya uamuzi kuhusu
jambo hili. Ni jambo lisilo na busara hata kidogo
kwenda kujadili Rasimu ya Katiba bila kuwa na suluhu inayokubalika kuhusu
Muundo wa Muungano wetu. HAPA KAKA UMETUMIA
MANENO MAKALI KIDOGO, YAANI HUONI BUSARA ? ANYWAY MIMI NINADHANI NDIO MAANA YA
KWENDA KUJADILI UNLESS UNA WASIWASI NA UWEZO WA HAO WANAOTAKIWA KUJADILI…. ILA
KAMA UNATAKA KUPATA “SULULU INAYOKUBALIKA” BILA KUJADILI SIDHANI KAMA UNAWEZA
KUIPATA.
Kama kuna presha ya muda wetu wa miaka
mitano kuisha kuna dirisha la kutokea; tusogeze mbele muda wa uhai wa Uongozi
wa awamu hii ama turudi nyuma tufanye mabadiliko ya sehemu za katiba
zinazohusiana na Tume ya Uchaguzi tu. Hatuna namna ya kukwepa moja kati ya
mambo haya kwa sababu hata tukifanikiwa kufunika kombe mwanaharamu apite,
tukapitisha Katiba hii, INAONESHA KUWA HAKA
KATABIA KAPO NA HUENDA KAMELETELEZA MKANGANYIKO AMBAO UNAUONA LEO, LAITI
MSINGEKUWA MNAFUNIKA KOMBE LEO USINGEPATA SHIDA….bado tutahitaji kufanya
mabadiliko makubwa ya Sheria mbalimbali nay a kitaasisi kutokana na Katiba mpya
itakayokuwa imepatikana, zoezi ambalo kwa kila namna litahitaji muda wa kutosha
na sioni kama upo! Demokrasia ni gharama na haikwepeki!
Maswali ni mengi zaidi ya Majibu. Wasiwasi
ni mwingi kuliko uhakika. Tutafika salama kwenye kupata Katiba hii kweli? Ni
bora tukawie kuliko kuvurunda. Tusikimbie kwa kasi bila kutazama tuendako,
tutambae lakini macho njiani na mbele tunakoelekea.
Tamko hili limetolewa na Ofisi ya Mbunge,
Jimbo la Nzega.
HK (Nimesaini)
Dkt.
Hamisi Kigwangalla, MB.