Wakati serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wahisani
wakipambana na tatizo la maralia nchin, baadhi ya wakazi wa manspaa ya Singida
wanatumia vyandarua kama vifungashio vya machupa chakavu ya plastiki
Uchunguzi uliofanywa na standard radio katika vitongoji vya
mji manspaa ya Singida, umebaini kuwapo kwa shehena kubwa ya machupa na vifaa
vingine vya plastiki vilivyofungashwa ndani ya vyangarua katika eneo la msalaba
mrefu mjini Singida
Wakazi wa eneo hilo lililoko jirani na kanisa la kiinjili la
kiruteli Tanzania KKKT licha ya kushuhudia kero hiyo ya matumizi kinyume ya
vyandarua, hawakuwa tayari kumtaja mhusika wa biashara hiyo
Serikali ya Tanzania kwa msaada wa serikali ya marekani
imekuwa ikisambaza vyandarua kwa kila nyumba nchini ili kuhakikisha watanzania
hususani wanawake wajawazito na watoto wanaepuka ugonjwa wa maralia
Mwezi Novemba mwaka 2012 waziri mkuu wa Tanzania Mizengo
Pinda alizindua kampeni maalum ya kudhibiti maralia
Inakadiriwa
takribani watu milioni 10 hadi milioni 12 wanaugua malaria kila mwaka, na
malaria husababisha vifo vya watu kati ya 100,000 hadi 300,000 kila
mwaka. Aidha zaidi ya asilimia 40 ya wagonjwa wanaohudhuria katika vituo vya
kutolea huduma za afya wanasumbuliwa na ugonjwa wa malaria.