Baadhi ya mabasi yakiwa katika kituo cha Gairo nje kidogo ya mji wa Gairo kwa ajili ya mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na safari ndefu kuelekea kanda ya kati, magharibi, kanda ya ziwa na nje ya nchi. Picha na. Prosper Kwigize
Kwa msafiri yeyote aliyewahi kusafiri kutoka Kigoma, Mara, Mwanza, Kagera na hata nchi jirani hataacha kamwe kuifahamu GAIRO,
Gairo ni wilaya Mpya katika mkoa wa Morogoro, wilaya ambayo inazungukwa na wakulima wa mazao mbalimbali ikiwemo vitunguu, nyanya. alizeti na miwa
Katika ukurasa huu, ninakusudia kuzungumza au kukushirikisha kuhusu kituo cha basi na hoteli ya Gairo ambapo maelfu ya wasafiri hupita na kupata ama chai, chakula cha mchana na usiku
Ukifika Gairo hutashangaa kuona purukushani za wasafiri kusaka mlo, na wengine kutafuta mahala pa kusitili miili yao kwa huduma za vyoo.
Hakika Gairo ni kituo kikubwa ambacho kila mtu awapo njiani safarini kwenda Mbeya, morogoro, Dar es Salaam, Mtwara na hata Zanzibar, hulazimika kupumzika hapo kwa dakika chache ili kudhibiti njaa
"Jamani abiria wetu, Hapa ni GAIRO, tutapumzika kwa dakika kumi tu kwa ajilii ya chakula na kuchimba dawa" Ni kauli ya kondakta ambaye mara tuu gari linaposimama yeye hutangulia kwa kazi moja tu kupata chakula, kuchimba dawa na wakati mwingine kutafuta abiria wapya.
Kinachonisukuma kuzungumzia kituo hiki muhimu kwa wasafiri wa ndani na nje ya Tanzania si uzuri wa madhari, majengo mazuri ya kitalii, huduma ya uhakika ya maji na chakula bali pia ni idadi kubwa ya mabasi na wasafiri ambao hupita na kujikimu
pamoja na hayo ninashawishika kuhoji, je halmashauri ya GAIRO kwaoo hichi ni chanzo cha mapato? kama ndiyo ni nani anawajibika kukusanya ushuru wa biashara zinazofanyika hapo pamoja na ushuru wa maegesho kwa magari yanayosimama na kupata huduma hapo, au ni kazi ya mmliki wa hoteli hiyo nzuri?
lakini pia tujiulize vyakula vinavyouzwa hapoo vina ubora uliohakikiwa na wataalamu wa idara ya afya ili kumhakikishia mlaji usalama wake?
Nasema hivyo kwa sababu, baadhi ya abiria siku hizi wakifika Gairoo wanashuka na kuchimba dawa tu (haja ndogo) na hawajishughulishi hata kidogo na kugombania masahani katika hotel hiyo, ukiuliza je! wao hawana njaa? majibu mepesi watakujibu "Usalama wa vyakula vya hapa ni mdogo sana, na isitoshe vikilala wanachanganya na vipya, ilimradi tu wasipate hasara"
Je Kauli hii anaifahamu mmliki wa Hteli hiyo muhimu kwetu wasafiri kutoka nje ya pwani? kama hajui basi mtandao huu wa www.kwigizenews.com, unamuasa kuchunguza usalama na uadilifu wa wauza vyakula ambao sina shaka wengi wao ni wapangaji
Hongera, kwa kuwajari wasafiri.
GAIRO KITUO KIKUU CHA MABASI KANDA YA KATI, ZIWA NA MAGHARIBI
Written By Unknown on Jumanne, 9 Julai 2013 | 09:49
Labels:
Events,
News in picture