TANZANIA, RWANDA NA BURUNDI ZASAINI MKATABA
Baada ya miongo kadhaa bila kutekelezwa kwa makubaliano ya kujenga mradi wa
umeme baina ya nchi za Tanzania, Rwanda na Burundi, na siku chache tu baada ya
kuyumba kwa mahusiano kati ya Tanzania na Rwanda, hatimaye mawaziri watatu
wa nchi za Tanzania, Rwanda na Burundi wamesaini mikataba miwili
inayohusu utekelezaji wa mradi wa kufua umeme wa maji ndani ya mto Kagera
utakaojengwa katika eneo la Rusomo mpani mwa Tanzania na Rwanda
Mkataba huo umeisainiwa jana na mawaziri wa nishati wa nchi za
Rwanda, Burundi na Tanzania katika mji wa Bukoba mkoani Kagera, ambapo mto
Rusumo ambao sehemu nyingine huitwa mto Kagera wenye mchango mkubwa wa maji ya
ziwa Victoria na mto nile umepata matumizi mapya ya nisahati kwa maendeleo.
Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo amesema kuwa
kusainiwa kwa mikataba huo, kumezifanya nchi hizo zitengeneze historia
mpya kwani mradi huo ulianzishwa tangu mwaka 1974 kutokana na sababu
mbalimbalia ikiwemo ukosefu wa fedha
Amebainisha kuwa mradi huo uko katika awamu mbili ambapo awamu ya
kwanza ni kufunga mtambo wa kufua umeme ambao utagharimu kisai cha dolla
za Kimarekani 340 ambazo ni kopo kutoka Benki ya Dunia, huku awamu ya
pili ikiwa ni kujenga njia za usafirishaji wa umeme kutoka Rusumo hadi
Nyakanazi, Rusumo hadi Kigali na Rusumo hadi Burundi
Aidha fedha hizo pia zitatumika kulipa fidia kwa wananchi walioathiriwa na
mradi ambao unagharimu dola milioni 130 za kimarekani kutoka katika Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB) na benki nyingine tatu ambazo ni washirika wa
maendeleoa ya Afrika.
Alisema kati ya hizo dola milioni 130 za kimarekani milioni 30
zinategemewa kufidia wananchi wa nchi za Rwanda na Tanzania ambao wameathiriwa
na mradi huo pale utakapopitia wakati Burundi hawatafidiwa kwani maeneo
unayopita mradi huo hakuna makazi ya watu.
Kwa upande wake Naibu Kamishna msaidizi wa nishati ya umeme Tanzania,
Innocent Luoga, alisema kuwa mradi huo unaratajiwa kuzalisha megawati 80
ambapo kila nchi itapata megawati 27.
Waziri wa Miundombinu wa Rwanda Prof. Silas Rwakabamba na Waziri wa Nishati
nchi ya Burundi Manirakiza C’ome walisema mradi huu umekuja kwa wakati muafaka
na itakuwa chachu ya maendeleo ya uchumi wa nchi hizi tatu kwani utaongeza pato
kwa wananchi wa nchi hizo tatu
Waziri Rwakabamba wa Rwanda hapa anaeleza utayari wan chi yake katika
kuhakikisha mradi huu haukwami pamoja na jitihada nyingine za nchi yake
Mwisho.