Mkoa wa Singida uko katikati mwa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, ni mkoa maarufu kwa kilimo cha vitunguu na Alzeti, mafuta ya Alzeti yamekuwa maarufu sana nchini na yamejizolea umaarufu mkubwa sana nchini. Cha kusikitisha wakazi wa mkoa wa Singida wanakabiriwa na uhaba mkubwa sana wa maji kiasi cha kuhatarisha afya na ustawi wa mkoa huo
katika picha ni moja ya magati ya kuchotea maji katika manspaa ya Singida ambapo mtu mmoja hulazimika kukaa katika eneo la kupatia maji kwa zaidi ya masaa mawili ndipo apate maji
juhudi zinahitajika kukamilisha mradi wa maji unaoendelea kujengwa katika manspaa hiyo ili kuwasaidia wananchi kupata huduma bora ya maji