HABARI MPYA
blink

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI

Written By Unknown on Jumatano, 17 Septemba 2014 | 07:13



MPANDA RADIO FM
Jengo la Kituo cha Matangazo cha Mpanda Radio FM 97.0 MHz mkoani Katavi

Iliyoko mjini Mpanda Mkoani Katavi, inatangaza nafasi za kazi kwa vijana wenye elimu, taaluma na kipaji cha uandishi wa habari na utangazaji. Muombaji anatakiwa awe na uzoefu wa angalau miaka miwili kazini.
Anayependa kufanya kazi Mpanda Radio atume maombi na wasifu wake akiambatanisha na nakala ya kazi (word and voice clips 2) alizofanya ndani ya mwezi mmoja uliopita.
Maombi yatumwe kwa emaili manager.mpandafm@gmail.com

WAHANGA WA MVUA 2013 WATELEKEZWA KIGOMA

Written By Unknown on Jumapili, 14 Septemba 2014 | 09:42

Na. Emanuel Senny, Kigoma. 
Bi. Bahati Luseba akiwa na wanawe katika eneo ilipokuwa nyumba yake


WAHANGA 100 wa mafuliko yaliyotokea mwaka 2013 maeneo ya katosho, kata ya Kibirizi katika manispaa ya Kigoma Ujiji wameachwa bila msaada wowote huku wakiishi maisha ya kutangatanga sambamba na kutotakiwa kujenga upya kutokana na eneo hilo kutengwa ili kupisha ujenzi wa bandari ya nchi kavu. 

Akifafanua hilo Mjane Bahati Luseba alisema yeye ni miongoni mwa wahanga ambapo alipoteza nyumba yake na anaoishi kwa kutangatanga kutafuta mahali pa kuishi hali inayowalazimu watoto wake watano wakiwemo wawili wa kike walale katika nyumba isiyosalama huku akisubiri fedha za fidia ambazo hajui atapewa lini. 

 Alisema aliishi hapo zaidi ya miaka 40 ndipo Desemba ,2013 walipokutwa na mafuriko, ambayo yalibomoa nyumba yake na kumlazimu alale nje zaidi ya miezi kumi akisubiri hatma ya malipo ya fidia kutoka serikalini ili aondokane na adha ya kutangatanga . 

Baada ya nyumba yangu kuharibika, mganga wa zahanati ya jibulenu alinipa chumba kwa muda katika zahanati yake , na kwasasa nimesaidiwa na mwalimu Gombea baada ya kutoka kutoka katika Zahanati kwani ni mahari pa wagonjwa tu alisema Luseba. 
Mabaki ya nyumba ziliezuliwa na Kimbunga wakati mvua kali
 Aliongeza kuwa taarifa zilizotoka Halmashauri kuwa kuna nyumba alitaftiwa kwaajiri ya makazi sio kweli pia mahema ambayo inasemekana walipewa baadhi ya wahanga hakuziona kwahiyo taarifa sio za kweli kwani yeye bado anatangatanga. 

Dkt. wa Zahanati ya Jibulenu Abu Rashid alikiri kumhifadhi katika chumba kimoja katika zahanati kutokana na mvua zilizokuwa zikiendelea. 

Nilishindwa kuendelea kumhuhifadhi kutokana na sheria,kanuni na taratibu za kikazi kuwa, zahanati si makazi rasmi kwa asiye mgonjwa aliongeza Rashidi. 

Aidha Kagu Jumanne ambaye ni mmoja wa wahanga wa mafuriko alisema kuwa baada ya tukio viongozi walienda eneo husika na kuahidi kutoa msaada kwa waathirika wote ila mpaka sasa hakuna walichopewa na wanaendelea kuhifadhiwa kwa majirani. 

Akijibia malamiko hayo Diwani wa kata husika Rashid Yunus ambaye pia ni Kaimu Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji alisema changamoto ya kushindwa kuwasaidia wahanga wa mafuriko inatokana na idadai kubwa ya walengwa na walitoa tulubai 52 kwa kaya 9 sambamba na kuyafungia mabati ili kuepusha lawama kwa umma kutokana na hali duni za wahanga hao. 

Hata hivyo Yunus alisema kuwa manispaa, ilitoa mabati chakavu 70, ili wapewe wananchi wenye maisha duni , lakini kutokana na ukubwa wa familia hizo wameamua kuyafungia katika ofisi ya serikali ya mtaa wa kahabwa katosho wakisubiri mchakato wa kufidiwa kwa wahanga hao ambao eneo lao limeteuliwa kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa Bandari kavu.

WALIMU 50 WILAYANI MOSHI WAADHIBIWA

Written By Unknown on Alhamisi, 11 Septemba 2014 | 04:13



Na. Frida Peter
Moshi



Zaidi ya waalimu wakuu 50  katika shule za msingi katika halmashauri za wilaya ya moshi mkoani Kilimanjaro wamevuliwa madaraka na  wengine wakihamishwa kutokana na  sababu mbalimbali ikiwemo uwezo mdogo wa utawala.

Hayo yamebainishwa na afisa elimu ya msingi wa wilaya ya Moshi Bw. Simoni Sheshe wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua ya serikali kutoa adhabu wa walimu hao

Bw. Sheshe amebainisha kuwa uchunguzi uliofanywa na idara ya elimu umebaini kuwa walimu hao wamekuwa na desturi ya kujipatia kipato kinyume cha sheria kwa kutoza fedha za vyeti kwa wanafunzi wanaohitimu darasa la saba

Sheshe amesema kuwa kufikia kwa hatua hiyo  kulitokana na malalamiko ya muda mrefu  ya wazazi na wananfunzi wa shule hizo  na kwamba tume ya utumishi ya walimu na idara ya elimu imekuwa ikitoa onyo mara kadhaa lakini walimu hao walikaidi.

Amesema waalimu wakuu hao walikuwa na tabia ya kuwatoza kiasi cha elfu kumi kila mzazi anaye fika shuleni hapo kwaajili ya kuchukua cheti cha darasa la saba jambo ambalo ni kinyume na utaratibu na kwamba cheti hicho hutolewa bure bila ya malipo yoyote.

Hata hivyo, licha ya adhabu hiyo kupongezwa na wazazi, mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Moshi Bw Moris Mokoi amesema kuvuliwa madaraka peke yake haitoshi na na ameagiza mkurugenzi wa halmashauri kuchukua hatua zaidi za kisheria dhidi ya waalimu watakao bainika kufanya hivyo.

MWANAFUNZI ABAKWA KIGOMA

Written By Unknown on Jumatano, 10 Septemba 2014 | 10:16



Na Emanuel Michael, Kigoma.

MWANAFUNZI wa darasa la saba miaka 14 amebakwa mapema wiki hii kabla ya kuanza mtihani wa kumaliza elimu ya msingi katika kijiji cha Bukuba, Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma.

Akizungumza na waandishi wa habari, Bi. Anisia Enock ambaye ni mama wa mtoto huyo, alisema kuwa mtoto wake alibakwa na Amoni Samwel (25) mkazi wa Mwanga B na kuhatarishiwa hatimayake ya kufanya mtihani.

Alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 12 jioni wakati mwanye huyo alipokuwa akielekea dukani kuchukua simu, mbani ndipo wazazi walipohoji uchelewaji huo na mwanaye akaeleza alichotendewa na Amoni Samwel.

“Binti yangu aliponisimulia nilichanganyikiwa kwani anatarajiwa kufanya mtihani  Jumatano na nilipomchunguza  alikuwa akitokwa na damu zilizotapakaa kwenye makalio ndipo nikaamua kumpigia simu baba yake  kabla ya kwenda kwenye vyombo vya sheria” alisema Bi. Enock.

Aidha Enock alisema kuwa alienda kutoa taarifa polisi na baada ya kuandika mashtaka alipewa PF3 kwaajiri ya kwenda  Hospitali na walipofika binti yake akafanyiwa vipimo sambamba na kupatiwa matibabu.

“Siku ya jumatatu Maafisa usitawi wa Jamii walifika na kumfanyia vipimo upya na kumpatia dawa tena ili kumpa nguvu ya kufanya mtihani” aliongeza

Kwa upande wa mwanafunzi aliyebakwa jina linahifadhiwa,  alisema kuwa baada ya kutumwa na mama yake alikutana na mwanafunzi mwenzake wa kiume na kumuomba amuelekeze walichofundishwa darasani na ndipo Amoni Samweli alipowakuta.

Aliongeza kuwa baada Mbakaji kuja aliwauliza walichokuwa wanafanya, nao  wakamjibu kuwa wanasoma lakini yeye akakataa na kuanza kumpiga makofi yule mvulana sanjari na kumwambia aondoke eneo mlile.

“Baada ya kumfukuza mwanafunzi mwenzangu alinambia nivue nguo mimi nikakataa ndipo akanibeba na kunipeleka kwenye shamba la ndizi na kunifumba mdomo ili nisipige kelele huku akinitishia kunichoma kisu hapo ndipo akanibaka” aliongeza.

Nae Afisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya ya Buhigwe, Godfrey Kapaya alisema kuwa walifika nyumbani kwa mwanafunzi huyo na kumfanyia vipimo vilivyothibitisha tukio hilo na alikuwa na maumivu sehemu za siri.

“Baada ya hapo tulimpa dawa za maumivu, dawa za kuzuia maambukizi ya magonjwa ya zinaa pamoja na mimba” alisema Kapaya.

Kapaya aliongeza kuwa kwakuwa mwanafunzi alitakiwa kuingia kwenye mtihani walimpa  ushauri wa kumuondolea hofu  ili afanye mtihani akiwa katika hari nzuri ya kimawazo.

Pamoja na hayo Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma, Japhari Muhamed alithibitisha tukio hilo na kuongeza kuwa mtuhumiwa tayari yuko mahabusu na hatua za kumfikisha mahakamani zinaendelea.

“Kitendo hiki ni kibaya sana na sisi tunakilaani kwani ndio tunaolinda watoto na wananchi kwa ujumla sasa ili iwe fundisho kwa wengine lazima mtuhumiwa ahukumiwe” alisema Muhamed.

Muhamed aliwataka wananchi kuwawaelimishe watoto wao wasitembee sehemu zisizo salama wakiwa peke yao hasa mida ya usiku pia na wazazi wawe makini kuwaacha watoto zao peke yao sambamba na kutoa taarifa pindi wanaposikia matukio kama haya.

Mwisho.

MBUNGE WA MUHAMBWE KIBONDO ANUSURIKA KIFO

Written By Unknown on Ijumaa, 5 Septemba 2014 | 11:43

Mhe. Felix Mkosamali Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Kibondo
Mbunge Felix Mkosamali wa Jimbo la Muhambwe Nccr mageuzi amenusurika kifo baada ya gari alimokuwa akisafiria kutoka Dodoma kwenda Kigoma kupata ajali

Kwa mujibu wa Polisi mkoani Dodoma Mkosamali amepata ajali katika wilaya ya Bahi baada ya gari lake kuligonga kwa nyuma roli lililokuwa limeegesha pembeni ya barabara

Kwa mujubu wa taarifa hizo, watu watatu waliokuwemo ndani ya gari la Mbunge huyo wamejeruhiwa 

inaelezwa kuwa chanzi cha ajali hiyo ni uzembe wa dreva wa gari la Mbunge huyo ambaye alishindwa kufuata alama za barabarani na kuwa katika mwenzo mkali uliosababisha ashindwe kulimudu gari hilo.

8 WAPOTEZA MAISA AJALINI KATAVI


Habari zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa watu wanane wamepoteza maisha katika ajali ya gari iliyotokea mchana mkoani Katavi

ajali hiyo imehusisha Roli la mizigo ambao watu kadhaa walipanda wakitokea wilaya ya Mlele kwenda mjini Sumbawanga

Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa ajalii hiyo na kwamba imetokea katika mlima Katete ambapo lilishindwa kupanda na kupinduka.

Hadi tunaingia mitamboni askari wa usalama walikuwa eneo la tukio wakijaribu kuokoa majeruhi.

36 WAPOTEZA MAISHA BUTIAMA

Watu 36 wamefariki dunia katika ajali ya magari mawili ya abiria wilayani Butiama mkoani mara mapema leo

Habari kutoka kwa jeshi la polisi mkoani  Mara zinasema kuwa ajali hiyo imehusisha mabasi ya kampuni ya Mwanza Coach na J4 yanayofanya safari kutoka Butiama kwenda Mwanza

Imeelezwa kuwa ajali hiyo imetokea leo asubuhi katika eneo la sabasaba ambapo watu wengine 79 wamejeruhiwa na wanapatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Butiama
 
Jeshi la polisi linafanya uchunguzi zaidi kuhusu chanzo cha ajali hiyo

BREAKING NEWS- HOFU YATANDA MJINI KASULU, BODABODA WAANDAMANA

Written By Unknown on Alhamisi, 4 Septemba 2014 | 03:59



Hofu imetanda katika mji wa Kasulu kufuatia vurugu zinazofanywa na madreva pikipiki maarufu kama Bodaboda ambao wanafanya maandamano kuelekea kituo cha polisi kushinikiza wenzao wanaoshikiliwa waachiwe huru.

Hali hiyo imeanza majira ya saa sita mchana baada ya kile wanachodai kuwa askari wa usalama barabarani tangu asubuhi  wamekuwa wakikamata bodaboda na kasha kuwapiga bila makosa.

Barabara kuu ya mjini Kasulu itokayo maeneo ya makaburini hadi kituo cha polisi imefurika pikipiki zinazoendeshwa kwa fujo kuelekea mtaa wa mlimani kwa ajili ya kushinikiza polisi kuwaachia wenzao waliokamatwa

Hata hivyo habari zinaeleza kuwa, mtu mmoja leo amegongwa nagari eneo la soko kuu kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni msongamano wa pikipiki zinazopaki katika makutano ya barabara hali inayosababisha upishanaji wa watembea kwa miguu, magari na pikipiki kuwa wa shida.

Mzee huyo ambaye jina lake hadi sasa halijajulikana amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kasulu.
 
Shukrani kwa : Harold Dickson | Prosper Kwigize | 0752490120
Copyright © 2013. KWIGIZE NEWS AND COMMUNICATION - Haki zote zimeifadhiwa
Email us: kwigizenews@gmail.com
0764243377